Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, January 31, 2013

POULSEN ATANGAZA KIKOSI CHA STARS DHIDI YA CAMEROON


 



KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.

“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam).

Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Katika kikosi hiki, Poulsen hajamuita Jerry Tegete ambaye siku za karibuni amefufua makali yake wakati ameita washambuliaji halisi wawili tu, Ulimwengu na Samatta.  

Nyota wa timu ya taifa ya Cameroon wanaotarajiwa kuja ni pamoja na:

 Charles Itandje, Mayebi Joslain, Allan Nyom, Benedict Angbwa, Benoît Assou Ekotto, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Armel Kana Biyick, Bouba Aminou, Joel Matip, Alexandre Song, Nguemo Landry, Pierre Wome Nlend, Hervé Tchami, Fabrice Olinga Essono, Achille Emana, Eloundou Charles, Jean Makoun II, Samuel Eto'o Fils, Vincent Aboubakar, Jean Paul Yontcha

Tuesday, January 29, 2013

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA COUTINHO

 New signing: Philippe Coutinho poses with a Liverpool shirt ahead of his move being officially being announced
Hatimaye mchezaji Phillipe Coutinho amejiunga rasmi na klabu ya Liverpool kwa ada ya euro milion nane akitokea klabu ya Inter Milan.

QPR YAIBANA MBAVU MAN CITY

 Farewell: Nelsen makes his way down the guard of honour... and Cesar applauds
Klabu ya QPR iliilazimisha sare ya bila kufungana klabu ya Manchester City kwa kutoka sare ya 0-0.Pambano hilo lililopigwa katika uwanja wa Loftus Road.

LAZIO YAITOA JUVENTUS COPA ITALIA

 Lazio celebrating (Coppa Italia, Getty Images)
Klabu ya soka ya Lazio jana iliweza kutinga fainali ya Copa Italia mara baada ya kuifunga klabu ya Juventus kwa magoli 2-1 katika pambano kali na la kusisimua lililopigwa katika uwanja wa Estadio Olimpico.Magoli ya Lazio yalifungwa na Alvaro Gonzales na Sergio Flocari wakati Arturo Vidal alifunga kwa upande wa Juventus

KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUKUTANA KESHO KUJADILI PINGAMIZI ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI


 
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo imepanga kukutana kwa mara kwanza kesho Jumatano, ili kupitia majina yote na pingamizi zilizowekwa kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za TFF.

Wagombea ambao wamewekewa pingamizi ni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, anayewania nafasi ya Bodi ya Ligi, Michael Wambura, anayetaka nafasi ya Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani anayewania Urais, Jamal Malinzi Urais, sambamba na Mugisha Garibona, Vedastus Lufano wanaowania nafasi ya Ujumbe, huku wakiwekewa pingamizi na Paul Mhangwa.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah, alisema Kamati ya Uchaguzi itapitia pingamizi zote zilizowekwa kwa wagombea hao.

Osiah alisema katika kikao hicho cha kujadili pingamizi kitakachoanza saa nne asubuhi, waombaji wote wa nafasi za uongozi na wale walioweka pingamizi wanatakiwa kufika katika tukio hilo.

“Wale walioweka pingamizi kwa wagombea na wanaowania nafasi za uongozi za TFF wote watashiriki kikao hicho cha kujadili pingamizi,” ilisema taarifa hiyo.

Uchaguzi wa TFF umepangwa kufanyika Februari 24 jijini Dar es Salaam, huku wadau mahiri wa michezo wakipigana vikumbo kuzitaka nafasi mbalimbali za Shirikisho hilo nchini.

Nafasi zote zimekuwa na ushindani wa aina yake, huku majina ya wadau kama vile Malinzi, Nyamlani kwa nafasi ya urais, bila kusahau Manji na Wambura wakipigania ubosi wa TFF katika Uchaguzi wa mwaka 2013.

Monday, January 28, 2013

PIRLO MCHEZAJI BORA ITALIA

Andrea Pirlo

Hatimaye kiungo nyota wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Andrea Pirlo amekumbukwa katika tuzo za wachezaji bora katika Ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Tuzo hizo zinazojulikana kama Gran Gara Del Calcio kutoka kujulikana kama Oscar Del Calcio zilishuhudia kura zaidi ya 600 zikipigwa na watu mbalimbali.

Mtiririko wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo.

Best Goalkeeper: Gianluigi Buffon (Juventus)
Best Right-back: Christian Maggio (Napoli)
Best Centre-backs: Thiago Silva (Milan/PSG) and Andrea Barzagli (Juventus)
Best Left-back: Federico Balzaretti (Roma)
Best Midfielders: Andrea Pirlo (Juventus), Antonio Nocerino (Milan), Claudio Marchisio (Juventus).
Best Forwards: Zlatan Ibrahimovic (Milan/PSG), Edinson Cavani (Napoli), Antonio Di Natale (Udinese).
Best Overall Player: Andrea Pirlo (Juventus)
Best Coach: Antonio Conte (Juventus)
Best Young Players in Serie A: Luis Muriel (Lecce/Udinese) and Stephan El Shaarawy (Milan)
Serie B revelations: Ciro Immobile (Genoa), Lorenzo Insigne (Napoli), Marco Verratti (PSG) – all were with Pescara
Best Club: Juventus
Best Referee: Nicola Rizzoli
Lifetime Achievement Award: Pippo Inzaghi

Sunday, January 27, 2013

JUVENTUS YAKAMILISHA USAJILI WA ANELKA

 
Klabu ya Juventus ya nchini Italia imefanikiwa kumnasa mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua Nicolas Anelka.Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Juventus,Anelak atalipwa mshahara wa kiasi cha fedha €600,000 kwa miezi mitano pamoja na bonasi katika mechi.

Saturday, January 26, 2013

YANGA KUANZA KIBARUA KESHO LIGI KUU VODACOM

 
Young Africans Sports Club Mabingwa wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya mechi itakayoanza majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es saalaam.
 
Mara baada ya kuweka kambi ya takribani wiki mbili katika mji wa Antalya nchini Uturuki kikosi cha Young Africans kimerejea kikiwa na morali ya hali ya juu, wachezaji na benchi la ufundi wakihitaji kushinda kila mchezo unaowakabli ili kujiweka katika hali nzuri ya kutwaa Ubingwa wa Vodacom.
 
Katik micheoz miwili ya kujipima nguvu  kabla ya kuanza kwa duru la pili la ligi kuu Young Africans ilishinda michezo yote, mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini kabla ya kushinda tena 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo ya Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika jijini Mwaza. 
 
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa kuwa na alama 29 alama tano zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 24, huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 25 na kufungwa mabao 10 tu katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom
 
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa katika dimba la uwanja wa Sokoine jijini Mbeya timu zilitoka sare ya bila kufungana mchezo ambao pia ulikuwa ni wa waufunguzi  katika araundi ya kwanza.
 
Kocha Mkuu Ernest Brandts amesema kikosi chake kimekamilika, kiakili, kiafya na kimorali hivyo anaamini vijana wake wataibuka na ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Prisons kutoka Mbeya.
 
Kikosi cha wachezaji 27 leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika uwnja wa mabatini kijitonyama huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri ya kimchezo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja. 
 
Timu imeingia kambini leo asubuhi katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani.

Friday, January 25, 2013

KIVUMBI CHA LIGI KUU VODACOM TANZANIA LEO


 
MZUNGUUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL),  kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 26 mwaka huu) kwa raundi ya 14 ambapo timu 12 kati ya 14 za ligi hiyo zitakuwa uwanjani.
Mabingwa watetezi Simba watakuwa wenyeji wa African Lyon katika mechi itakayochezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa kikosi cha Simba tangu kiliporejea kutoka Oman kwenye ziara ya mafunzo.

Mwamuzi wa kimataifa Israel Mujuni ndiye atakayechezesha mechi hiyo ambapo African Lyon inatarajiwa kuongozwa na Kocha Charles Otieno baada ya kusitisha kibarua cha Pablo Velez kutoka Argentina kutokana na kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza.

Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro wenye uwezo wa kumeza watazamaji 8,000 ndiyo utakaohimili vishindo vya mechi kati ya Polisi Morogoro na wenyeji Mtibwa Sugar. Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa VPL ililazimisha suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

Coastal Union ambayo kwenye dirisha dogo imesajili wachezaji sita akiwemo Mzimbabwe Tinashe Machemedze itaoneshana kazi na wana-Tanga wenzao Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Timu zinazo katikati ya msimamo wa ligi, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambapo sheria 17 zinazotawala mpira wa miguu zitakuwa chini ya usimamizi wa refa Dominic Nyamisana kutoka Dodoma.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam baada ya mechi za kirafiki nchini Kenya wanarejea kwenye Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuikaribisha Kagera Sugar ya Kocha Abdallah Kibaden kwenye Uwanja wa Chamazi.

Ni mechi ya kulipa kisasi kwa Kagera Sugar baada ya kulala bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Septemba 15 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Maafande wa Oljoro JKT wanaanza kuchanga upya karata zao katika mzunguko wa pili kwa kuikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, jijini Arusha.

DORTMUND YAIFUNGA NURNBERG BUNDESLIGA

 Borussia Dortmund v 1. FC Nuernberg - BundesligaJakub Blaszczykowski
Klabu ya Borussia Dortmund imeendeleza makali yake katika Ligi kuu ya soka nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.Dortmund walipata magoli yake kupitia kwa kiungo wao shupavu Jakub
Blaszczykowski(Kuba) katika dakika za 18 na 21 huku mshambuliaji Robert Lewandowski naye akifunga goli la tatu katika dakika ya 88.

Thursday, January 24, 2013

BREAKING NEWS: JUVENTUS WAMSAINI LLORENTE


 

Hatimaye klabu ya soka ya Juventus ya nchini Italia imemsainisha mchezaji nyota wa klabu ya Athletic Bilbaoya nchini Hispania Fernando Llorente kwa mkataba wa miaka minne(4) taarifa na mtandao wa Juventus.Llorente atakuwa akilipwa euro milioni 4.5 kwa mwaka.

EDEN HAZARD ALIPOMPIGA TEKE 'BALL BOY' WA SWANSEA CITY



VITA nzima ya Eden Hazard na muokota mipira wa Swanzea City - Charlie Morgan, 17, ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi wa Swansea, Martin Morgan. Charlie alitembea taratibu kuufuata mpira, Hazard akakimbilia kutaka kuwahisha mchezo, dogo akagombea mpira na nyota huyo, kabla ya kumshuti teke la mbavu kama inavyoonekana pichani.

 
 Hapa Hazard akimpapatua Charlie ili auchukue mpira tayari kwa kuendelea na pambano. Ikumbukwe hapo Chelsea ilikuwa ikisaka mabao 2-0 iliyofungwa katika mechi ya awali, ili kusawazisha na kulipeleka pambano katika dakika 30 za ziada 'Extra Time' kuwania tiketi ya fainali ya Capital One 'Carling Cup'. Mechi iliisha kwa sare ya 0-0 na Swanse kutinga fainali.

 
Hazard akauchukua mpira na kurudi nao dimbani akimuacha Charlie akigalala kwa maumivu ya shuti la mbavu. Chezea The Blues wewe dogo!

 
 Mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba ambaye alikiri kumuona Hazard akimpiga teke dogo Charlie, alimfuata dogo kumpa sapoti fulani.
 
 Charlie katikati akiugulia maumivu baada ya kuinuka.
 
  Mwamuzi wa mchezo huo Chris Foy, akashindwa kujizuia na kuamua kumlima Hazard kadi nyekundu ya moja kwa moja kama anavyyonekana pichani.
 
 Hapa Hazard akisindikizwa kuingia vyumba vya kuvalia baada ya kuoneshwa kadi nyekundu.

Picha na matukio toka Habari Mseto Blog

Wednesday, January 23, 2013

AFRIKA KUSINI YAIFUNGA ANGOLA AFCON

South Africa
Magoli mawili ya wachezaji Siyabonga Sangweni na Lehlohonolo Majoro yalitosha kuipa ushindi timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana dhidi ya Angola katika mchezo wa kundi A.Mechi ijayo ni Morroco dhidi ya Cape Verde saa 3usiku.Afrika Kusini 2-0 Angola.

YANGA YAIFUNGA TENA BLACK LEOPARDS JIJINI MWANZA


Magoli mawili ya washambuliaji Said Bahanuzi na Jerry Tegete yalitosha kuipa labu ya Yanga ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya nchini Afrika Kusini.Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

RATIBA YA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU YA VODACOM


 

Januari 26, 2013

African Lyon Vs Simba SC
Mtibwa Sugar Vs Polisi Morogoro
Coastal Union Vs Mgambo JKT
Ruvu Shooting Vs JKT RUVU
Azam FC Vs Kagera Sugar
JKT Oljoro Vs Toto Africans

Januari 27, 2013
Yanga SC Vs TZ Prisons

Januari 30, 2013
Azam FC  Vs Toto Africans

Februari 2, 2013
Yanga SC Vs Mtibwa Sugar
Polisi Moro Vs African Lyon
Mgambo JKT Vs Ruvu Shooting

Februari 3, 2013
Simba SC Vs JKT Ruvu
Coastal Union Vs TZ Prisons
JKT Oljoro Vs Kagera Sugar
Polisi Moro Vs JKT Oljoro

Februari 9, 2013
Mtibwa Sugar Vs Azam FC
Toto Africans Vs Coastal Union
Kagera Sugar Vs Mgambo JKT
TZ Prisons Vs African Lyon
JKT Oljoro Vs Simba SC


Februari 13, 2013
Kagera Sugar Vs Coastal Union
Toto Africans Vs Polisi Moro
Mgambo JKT Vs  JKT Oljoro
Mtibwa Sugar Vs Ruvu Shooting
African Lyon Vs Yanga SC

Februari 20, 2013
JKT Ruvu Vs Azam FC
TZ Prisons Vs Simba SC
Coastal Union Vs JKT Oljoro
Toto Africans Vs African Lyon

Februari 23, 2013
Yanga SC Vs Azam FC
Mgambo JKT Vs  JKT Ruvu
TZ Prisons Vs Polisi Moro
Kagera Sugar Vs African Lyon

Februari 24,  2013
Simba SC Vs Mtibwa Sugar

Februari 27, 2013
Coastal Union Vs Ruvu Shooting
Yanga SC Vs Kagera Sugar
Polisi Moro Vs Mgambo JKT
JKT Ruvu Vs Totot Africans
Mtibwa Sugar Vs TZ Prisons

Machi 6, 2013
African Lyon Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs  Mtibwa Sugar
JKT Oljoro Vs TZ Prisons

Machi 7, 2013
JKT Ruvu Vs Kagera Sugar

Machi 9, 2013
Yanga SC VS Toto Africans
Azam FC Vs Polisi Moro

Machi 10, 2013
Simba SC Vs Coastal Union

Machi  16, 2013
Toto Africans Vs Mgambo JKT
Ruvu Shooting vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Coastal Union

Machi 17, 2013
JKT Ruvu Vs Polisi Moro

Machi 18, 2013
African Lyon Vs   JKT Oljoro

Machi 27, 2013
Azam FC  Vs TZ Prisons
Kagera Sugar Vs Simba SC

Machi 30, 2013
JKT Oljoro Vs JKT Ruvu
Ruvu Shooting Vs Azam FC
African Lyon Vs Coastal Union
Polisi Moro Vs Yanga SC
Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar
Toto Africans Vs Simba SC

Aprili 3, 2013
Toto Africans Vs TZ Prisons

Aprili 10, 2013
Yanga SC Vs JKT Oljoro
Azam FC Vs African Lyon
TZ Prisons Vs  Mgambo JKT
Polisi Moro Vs Ruvu Shooting
Coastal Union Vs JKT Ruvu
Mtibwa Sugar Vs Toto Africans

Aprili 13, 2013
Azam FC  Vs Simba SC
Mgambo JKT Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs JKT Oljoro
TZ Prisons Vs Ruvu Shooting

Aprili 17, 2013
Kagera Sugar Vs Toto Africans
African Lyon Vs JKT Ruvu

Aprili 21, 2013
JKT Ruvu Vs Yanga SC

Aprili 25, 2013
Ruvu Shooting Vs Simba SC

Aprili 27, 2013
Coastal Union Vs Azam FC

Aprili 28, 2013
Simba SC Vs Polisi Moro

Mei 1, 2013
Mtibwa Sugar Vs African Lyon
Yanga SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs TZ Prisons
Polisi Moro Vs Kagera Sugar
Ruvu Shooting Vs JKT Oljoro

Mei 8, 2013
Simba SC Vs Mgambo JKT

Mei 11, 2013
Azam FC  Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting

Mei 18, 2013
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union