
Alikuwa ni Robin Van Persie ambaye hapo jana usiku aliihakikishia ushindi klabu ya Man United mara baada ya kufunga mara mbili dhidi ya klabu ya CFR Cluj ya nchini Romania katika ule usiku wa Ulaya.Van Persie alikuwa akitokea pembeni zaidi ili kumpisha mshambuliaji mwenzake Chicharito kusimama katikati aliweza kutumia vyema nafasi alizopata mara baada ya kupata pasi toka kwa mshambuliaji mwenzake Wayne Rooney.

Akizungumzia magoli hayo mshambuliaji huyo alisema kuwa kwa sasa ana magoli saba aliyoyafunga katika klabu hiyo na anahitaji kufunga magoli mengi zaidi.Katika mechi hiyo ilimalizika kawa Man United kushinda magoli 2-1 ilimshuhudia beki wa Man United wa kati Johnny Evans akipata majeraha na hivyo kuongeza wasiwasi katika kambi ya Man United ambayo kwa sasamimeonekana kuwa na majeruhi wengi.
Majeruhi hao ni pamoja na nahodha Nemanja Vidic,Chriss Smalling,Phil Jones na sasa Johnny Evans.Bado ripoti ya madaktari haijatoka kuhusu Johnny Evans na kocha Ferguson anahamini kuwa mchezaji huyo atakuwepo katika mechi dhidi ya Newcastle United jumapili hii.

Katika hatua nyingine klabu ya Chelsea iliweza kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Nordsjaelland ya nchini Denmark.Mabao ya Chelsea yalifungwa na Juan Mata katika dakika za 33,82,David Luiz dk ya 79 na Ramirez katika dakika ya 89.

Pale Estadio Da Luz klabu ya Barcelona ilipata ushindi mzuri wa ugenini dhidi ya klabu ya Benfica huku shukrani zikiwaendea wachezaji Sanchez na Fabregas walioipatia ushindi timu hiyo.Katika mechi hiyo kulikuwapo na tukio baya la beki wa Barca Carles Puyol kuvunjika mkono na hivyo kuzidi kuipa wasiwasi ngome ya Barca ambayo imekumbwa na majeruhi wengi kama Gerad Pique na beki mwingine Adriano.
0 comments:
Post a Comment