
Young Africans Sports Club Mabingwa wa Kombe la Vilabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kesho inatarajiwa kushuka dimbani
kucheza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya mechi
itakayoanza majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
saalaam.
Mara baada ya kuweka
kambi ya takribani wiki mbili katika mji wa Antalya nchini Uturuki
kikosi cha Young Africans kimerejea kikiwa na morali ya hali ya juu,
wachezaji na benchi la ufundi wakihitaji kushinda kila mchezo
unaowakabli ili kujiweka katika hali nzuri ya kutwaa Ubingwa wa Vodacom.
Katik
micheoz miwili ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa duru la pili la
ligi kuu Young Africans ilishinda michezo yote, mchezo wa kwanza kwa
mabao 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini
kabla ya kushinda tena 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo
ya Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika jijini Mwaza.
Young
Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa kuwa na
alama 29 alama tano zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili ikiwa na
alama 24, huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 25 na kufungwa mabao 10 tu
katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom
Katika
mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa katika dimba la uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya timu zilitoka sare ya bila kufungana mchezo ambao
pia ulikuwa ni wa waufunguzi katika araundi ya kwanza.
Kocha
Mkuu Ernest Brandts amesema kikosi chake kimekamilika, kiakili, kiafya
na kimorali hivyo anaamini vijana wake wataibuka na ushindi katika
mchezo wa kesho dhidi ya Prisons kutoka Mbeya.
Kikosi
cha wachezaji 27 leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi
katika uwnja wa mabatini kijitonyama huku wachezaji wote wakiwa katika
hali nzuri ya kimchezo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja.
Timu imeingia kambini leo asubuhi katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani.
0 comments:
Post a Comment