Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, August 13, 2012

NI DAKIKA 3060 ZA MSUGUANO JE BAYERN AU DORTIMUND TENA?


Ni swali ambalo situ kila mpenzi wa hizi timu mbili kubwa pale BUNDESLIGA linawaumiza kichwa  bali pia wachambuzi wa soka kutoka kila pande ya Dunia.Borussia Dortimund chini ya rais Dr Reinhard Rauball  mkurugenzi mkuu Hans-Joachim Watzke, mkurugenzi wa michezo na mchezaji mwenye lekodi ya michezo mingi Dortimund Michael Zorc  kwa pamoja na Kocha Juggen Klopp a.k.a  JK hakika wamefanya kazi kubwa sio tu kuirudisha Dortimund katika makali yake bali pia kupata kile kinachoitwa kwa sasa mpira Dortimund.
Dortimund wamepita vipindi tofauti vya raha na karaha na tatizo kubwa likiwa katika usimamizi wa fedha na kupelekea mpaka kufirisika na tishio kubwa likiwa lile la 2005.Westfallen Stadion moja kati ya viwanja vikubwa Ujerumani na Ulaya ukikabidhiwa kwa kampuni ya Insuarance ya Signal Iduna na uwanja kuitwa Signal Igunal Park mpaka 2016 ili kupunguza madeni ya Dortimund.

Unaikumbuka Dortimund ya mwaka 1997 chini ya Ottmar Hitzfeld ikiwa na nyota kama Karl Heinz Riedle kocha wa sasa wa Norwich Paul Lambert,kikosini pia kukiwa na kinda aliyekuwa anakuja kwa kasi kweli Lars Ricken na sasa akisimamia timu ya vijana.Waliisasambua Juventus 3-1 mbele ya Zinedine Zidane kuchukua Uefa Champions league na wakati ule Intecontinetal cup wakiilaza Cruzeiro 2-0 hakika hii ilikuwa Dortimund ambayo kurudia walichokifanya umekuwa ni mtihani kweli kweli.

JUGGEN KLOPP JK
 Wamepita walimu wengi lakini yeye ndo nembo ya ushindi sasa pale Westphalia.Achana na bajeti finyu ambayo hana budi kwenda nayo huyu jamaa ameleta vitu viwili vikubwa kwanza ni mpira Dortimund na nidhamu kubwa kikosini.Ametengeneza kitu ambacho  walimu wengi kinawashinda kutengeneza kwamba hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu.

 Msimu wa kwanza tu aliitoa Dortimund kutoka nafasi ya 13 nafasi mbovu katika kipindi cha miaka 20  mpaka nafasi ya sita akiwa na rekodi nzuri ya Ulinzi wa Hummels na Subotic  2008-2009  na nafasi ya tano msimu wa 2009-2010. Msimu wa tatu na nne amewafanya Dortimund mabingwa akitumia sana timu yao vijana na mtandao madhubuti wa kupata vijana wenye vipaji lakini kwa pesa kiduchu akachukua kombe msimu uliofuta wa 2010-2011 akiwaacha wengi midomo wazi wakiwa hawaamini.


Msimu uliofuta wengi wakiamini ule ulikuwa ni moto wea kifuu JK aliwashangaza tena akichukua makombe mawili kwa mara ya kwanza tena kwa kuweka rekodi ya kufikisha pointi 81 ni nyingi kuliko zote katika historia ya Bundesliga.Wakianza msimu bila ya mfungaji bora wa msimu uliopita Lucas Barios staili yake ya kuwajaza vijana kujiamini inamleta Lobert Lewandoski na kuwafanya mashabiki kumsahau kabisa Lucas Barios.

Kipindi cha majira ya joto wanamuuza nyota Nuri Sahini kwenda Madrid lakini anamuinua Shinji kagawa kuziba pengo mashabiki wanamsahau Sahin.Msimu huu wanamuuza Shinji kagawa kwenda Manchester United wanamrudisha nyota wao waliyemlea na kumkuza wenyewe kutoka Gladbach Marco Reus kuziba pengo la kagawa na nina uhakika watu watamsahau Shinji Kagawa.

Swali kubwa ni je Dortimund ataendelea kuitambia Bayern Munchen na Bundesliga kwa ujumla? Hebu tuone misimu  huu utakovyokuwa.

MSIMU HUU UNAONEKANA MGUMU
.Msimu huu unaonekana kuahidi kuwa mgumu na wenye ushindani pengine kuliko mismu miwli iliyopita kutokana na sababu zifuatazo.Msimu uliopita unaonekana ni msimu mbaya na wa kusikitisha kwa The Bavarians kwani sio tu kwamba walipoteza tena taji la Bundesliga bali walikuwa nyanya Aliaz Arena na hata Stadio Signal Iduna Park mbele ya Dortimund.Wakapoteza tena kwenye  kombe la Ujerumani kwa kipigo cha 5-2 kabla ya Drogba kukamilisha kile kilichokuwa kinaonekana kama homa ya kucheza fainali ya klabu bingwa uwanja wa nyumbani kwa hiyo msimu huu unaonekana kama msimu wa visasi kweli kweli.

 USAJILI
Baada ya kumkosa Marco Reus Bayern wamemsajili Xherdan Shaqili pembeni kule kwa Roben ambaye sio  tu kwamaba  ana historia mbaya ya majeraha lakini pia akionekana kuigharimu Bayern kwenye matukio muhimu lakini kubwa abisa ambalo hata vyombo vingi vya habari vya Ujerumani vilikuwa vikimpigia kelele ni la kuwa mmbinafsi uwanjani.Lakini pia Wamewasajili Claudio Pizzaro na Mario Mandzukic kwenye ushambuliaji.Wengi watajiuliza kwa nini Claudio Pizzaro na Mario Mandzukic na tayari Bayern wana mtu hatari mbele Mario Gomez? Lakini amini usiamini pamoja na kupitwa na Messi na Ronaldo pekee kwenye kufumania nyavu Ulaya msimu uliopita Gomez amekuwa akipondwa sana na wakongwe wa Bayern Munchen na hata rais  wa Bayern Ruminage  akidaiwa  kupoteza nafasi nyingi  sana na kufunga chache.

Dortimund kwa upande wake Baada ya kuondokewa na Kagawa walimsajili Marco Reus. Ni mtu hatari sana aking’ara na Gladbach msimu uliopita na wakuwafanya msimu huu washiriki klabu bingwa barani ulaya.Anatazamiwa kutengeneza uwiano na uelewano mzuri na kinda mwenye kipaji cha hali ya juu ujerumani kwa sasa na rafiki yake toka timu ya vijana  ya Dortimund Mario Gotze. Ujio wa Gotze ni kama usajili mpya kwani kwa kipindi kirefu amekuwa akiandamwa na majeraha na hakika wananifanya niisubri Bundesliga kwa hamu sana.Lakini pia wamewasajli Leonardo Bittencourt,Julian Schieber na Olivier Kirch.Ujio wa Kirch Unatazamiwa  kutoa msaada pembeni kule beki ya kulia kwa Lukasz Pisczcek ambaye majeraha kidogo yamekuwa ya kimsumbua.

UZOEFU WA MICHUANO MIKUBWA
Tatizo kubwa ambalo laweza kuisumbua Dortimund msimu huu ni michuano ya Virabu bingwa barani Ulaya.Japo walicheza vizuri katika makundi msimu uliopita lakini kimbinu na kiakili Dortimund walionekana hawajakomaa na hata kocha Juggen Kopp akisema michuano hii imekuwa mikubwa sana kwa baadhi ya nyota wake.Japo walianza vibaya ligi lakini kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi lake lililokuwa na Arsenal,Marsille na olimpiacos iliwafanya wachukue Bundesliga bila kupoteza hata mchezo mmoja katika yote iliyokua imebaki baada ya kuutoa mzigo wa klabu bingwa.

1 comment:

  1. Dortmund must find a way to recover the gap left by Shinji kagawa, Reus hmslf cnt, nor Mario Gotze who seems 2 be addicted wit injuries, jus like tom cleverley and jack wilshare. .shinji was such important player in their squard, made them succed wot they've succeeded. .

    ReplyDelete