Naitwa Edgar Kibwana.
Ni mfuatiliaji na mchambuzi wa michezo mbalimbali duniani
ukiwepo mchezo wa mprira wa miguu maarufu kama (soka).Nilianza kufuatilia soka
takribani miaka 10 iliyopita katika ligi ya ndani ya nchi yetu ya Tanzania
lakini pia nilipata fursa ya kufuatilia soka la nje ya nchi kwa kuzitazama ligi
za nchi mbalimbali kama Ujerumani, Italia, Uingereza na michuano ya klabu
bingwa Afrika, klabu bingwa ulaya, mataifa Afrika, kombe la mataifa ulaya, Amerika
ya Kusini,Olimpiki na bila kusahau kombe la dunia.
Katika kutimiza azma yangu ya kuwa mchambuzi wa kimataifa
katika soka, nimeanzisha blog itakayokuwa na uchambuzi wa soka pamoja na
michezo mingine kama mpira wa kikapu nk.lengo likiwa ni kuzidi kuwahabarisha
wadau wa michezo na kujaribu kushea mambo mbalimbali katika kuongeza weledi wa
mambo, kutoa burudani au kupata burudani kupitia michezo.Nipo pamoja na
wachambuzi wenzangu Wilson au Willy, Rahim, Salum, Jumanne na tunakaribisha
wengine watakouguswa na uchambuzi wetu. Karibuni sana katika kutoa uchambuzi
bila kusahau maoni.
Tuungane pamoja katika edgarkibwana.blospot.com
KARIBUNI SANA.
Mob: 0714 041236
Face book: Edgar kibwana
0 comments:
Post a Comment