akumbuka wakati Fulani nipo chuoni
pale chimwaga jengo Fulani maarufu wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma
wanalifahamu sana baadhi ya vipindi au[ lectures] na mihadhara mbalimbali
inafanyika pale kuna kozi flani hivi kila ikiisha wanafunzi wanahisi kuchanganyikiwa.
Nikamuuliza mwalimu wangu wa somo hilo
akaniambia usishangae sana ukiona kuna kitu nimekufundisha halafu ukahisi kama unakaribia
kuchanganyikiwa hivi ujue unakaribia kuelewa kwasababu wakati wa
kuchanganyikiwa ndo wakati wa ubongo kuchambua kipi cha kuelewa na kufuata na
kipi sio kitu cha msingi na kuachana nacho.
Nao wahenga wana msemo wao wanasema
ukijua tatizo ujue unakaribia kulipatia
jawabu ndo kitu kinakaribia kutokea pale
kwenye viwanja vya London Colney na Emirates kwa pamoja.
Ukitua uwanja wa Emirates leo kitu
unachokutana nacho mara moja ni sanamu za watu watatu huyu ni Arsene wenger
kocha anayetajwa kuwa ndo mwalimu mwenye mafanikio kuliko wote pale Arsenal na
mchango wake kwenye soka la Uingereza haupingiki,akifuatwa na mfaransa mwenzake
mfumania nyavu bora wa Arsenal na ligi kuu pale Uingereza Thiery henry pembeni
kidogo ni Toni Adams moja kati ya mabeki
wakati bora kabisa pale Arsenal na England.
Hizi ni nembo za ushindi na ushujaa
pale Emirates na kwa pamoja huu ni utambulisho kwa mashabiki, makinda
wanaochipukia pamoja na wachezaji wapya wanaosajiliwa kujionea moja kati
ya vitu vizuri vilivyowahi kutokea katika historia ya timu yao.Ukienda popote
vilabu vyenye mafanikio makubwa katika soka watu hawa wana nafasi kubwa sana
lakini si Arsenal ukija hapo mambo ni tofauti kidogo hapa utaishia
kuambulia mikanda ya video na simulizi tu hakika ukiwa kama mpenzi wa hii timu
hakika nilazima utahisi kuchanganyikiwa.
Hapa majuzi dirisha dogo la mwezi
January tulimshuhudia Thiery henry akirudi Arsenal na ukiacha Van persie huyu
jamaa ni miongoni mwa watu waliochangia kwa kiasi kikubwa Arsenal kugeuza
msimamo waligi ya premier pale Uingereza kuitoa Arsenal katika kile
kinachoaminnika ni kuanza msimu vibaya ambako hakujawahi kushuhudiwa katika
historia ya timu hiyo.Huyu alikuwa mtu muhimu sana pale eamirates ukitoa
mzee Wenger, kuanzia London Colney mpaka kwenye vyumba vya kubadilihia
nguo,hata wale wachezaji makinda ambao walipata kumuona kupitia luninga zao ama
kwenya mikanda ya video hakika iliwaongezea kitu cha ziada.
Hakika anayewza kurishuhudia kwa
uzuri kabisa ni kinda mwenye kipaji cha
hali ya Chamberlain anasema” nilipomwona kwa mara ya kwanza nilimshangaa sana
nilimuona kama si mchezji kama mimi lakini baada ya kufanya naye mazoezi ndo
nikahisi naye mtu”wakati wa mechi na Manchester pale Emirates akasema “wakati
tunakimbia naye aliniambia uwezo wangu na amesesma vitu ambavyo naweza kufanya
na akanisisitiza niendelee kufanya hivyo.Hivi ndo vitu ambavyo vinaweza
kumtofautisha Benick Afobe na Dan Welback ambaye kila siku anafanya mazoezi na
watu ambao wamefanya vitu vikubwa na klabu kama kina Ryan Giggs na Paul Scholes
sasa Henry yupo zake marekani lazima
uhisi kuna kuchanganyikiwa kama kweli una mapenzi na timu yako.
Nakumbuka wakati ule kuelekea
msimu mpya miaka nane sasa imeepita Arsenal wakianza msimu kama mabingwa
watetezi ni kipindi cha kuwaongezea mikataba Thiery henry,Patric Vieira na Denis
Bergkamp huku mikataba yao ikiwa imebaki miaka mitatu na mchezaji pekee anayeuzwa
ni Nelson Vivas kama ni leo timu ikiwa Uchina ikijindaa na msimu mpya ungesikia
taarifaa za kuuzwa kwa Sebastiani
Squilacci, Maroune Chmakh na imeshaandaa mikataba minono kwa kina
Fabregas,Nasri,Walcott pamoja na Vanpersie lakini siku hizi mambo yamebadilika
sana wanaotakiwa kubaki ndo wanaondoka wanaotakiwa kuondoka ndo wanabaki katika
mazingira haya kama una moyo wenye nyama kama wangu lazima uhisi kuna
kuchanganyikiwa.
Arsene wenger na Arsenal wanammisi sana
mtu anayeitwa Devid Dein huyu alikuiwa ni zaidi ya makamu mwaenyekiti alikuwa yuko kwaajili ya kumfanya kila mtu sio tu
anafanya kazi bali pia kuifurahia na kuifanya Arsenal pahala pazuri kila mtu
angetamani kuishi.Sasa mtu huyu ameondoka na kila kitu pale kuanzia makombe mpaka mastaa wa timu Van persie
ndo anamalizikia katika kile kizazi ambacho kilipokea tuzo ya kuwa timu bora
kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka ishirini ya uhai wa Bacrays English
Premier League.
Kitu pekee alichobakiziwa ni mpira
Wenger na ndo hi ndo jeuri pekee ya mashabiki kwenye vibanda vya
kuangalizia mpira pale Shimo la udongo jamaa achilia mbali kwamba ndo
aliyempa shavu wenger akimtoa Japan huko vichakani Nagoya Grumpus 8 lakini pia
ndiye aliyekuwa msaada mkubwa katika kuwaleta nyota kibao Emirates kina Denis,Thiery
henry alikuwa ni kama Pini Zahavi wa Arsensal manake alikuwa anazijua fitina
kwelikweli.

Ukimuona mzee wenger katikati
ya pambano pale Wembley anasimama anakaa kama kuna mtu anamchezesha hivi anakunywa
maji anatema anatupa chupa yenyewe kabisa kachanganyikiwa na unaweza
kusema ni mtu wa jabu sana au ndo yale ya kuficha mchele mpaka siku ya krismas
au IDD huku watu wanakufa njaa manake jinsi ya kumaliza miviga.
Anajua manake ameshaozesha watoto na ana
wajukuuu,achana na sera na mvurugano uliopo kati ya watu wawili wanaohodhi hisa
nyingi Stan Kroenke pamoja na Ulshar Usmanov unamuacha vipi Dennis Bergkamp
ajiunge na Ajax au Patrick Viera ajiunge kama mkrugenzi wa maendeleo ya michezo
huku ukiwahitaji kwa kiasi kikubwa ,fikiria kueleke mchezo Fulani wa ligi na
labda Manchester city pale uwanja wa Ethadi huku Fabregas akiwa na mawazo
kuelekea mchezo huo akicheki pembeni kuna Patrick Viera akitabasamu
nakumuelezea jinsi walivyompiga City nje ndani katika ule msimu anamaliza vita
kama ilivyoanza ni msimu ambao Arsenal wanamaliza wakiwa hwajapoteza mchezo
wowote sio Highbury wala Oldtraford.
Kuna wakati Fabregas mahesabu
yalikuwa hayaendi kabisa kama kachanganyikiwa hivi anatamani kumwambia kitu
mzee Wennger anashindwa akicheki pembeni anamwona Craig Eastmond na Watt
Sanchez juu kabisa hapo anakutana na lile kundi la machinga kutoka marekani wao
lillowaleta mjini ndo haswa wanalifanya kwa asilimia mia moja unachowaza ndugu
yangu shimo la Udongo pale sio wao wanachowaza lazima uhisi kama
unachanganyikiwa hivi.
Fabregas kwake ni kama
kukabidhiwa jezi huku akiwa mchezo hujaulewa alipewa jukumu la kuwa baba wakati
na yeye alikuwa mtoto aliyehitaji kulelewa alitamani sana lile somo la ziada
ambalo Messi,Iniesta,Xavi wanalipata toka kwa akina Guardiola mwisho unajua
alisema nini “wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu akitoka baba yangu
aliyelala na mama yangu nikazaliwa mimi wewe ndo unafuata” lakini sina budi
kusema usiku mwema kama ambavyo Van persie anamwambia leo lazima uhisi
kunyanganyikiwa kama kweli una mapenzi ya ukweli na timu yako.
Arsenal ni moja kati ya vijiji
ambavyo havina wazee na ndio maana mpaka sasa ni msimu wa saba sasa Wanacheza
soka ambalo imekuwa ndo kielelezo cha soka bora ulimwenguni kwa sasa lakini
bado hawajaonja vikombe na wameishia kuskia nderemo,vifijo na na
vigelegele kwenye kijiji cha wenzao hapohapo kaskazini mwa LONDON yani Chelsea.
Wako wapi kina Toni Adams,yuko wapi
Yule mwanaume wa shoka aliyekuwa tayari kuitumikia Arsenal bila hata
senti pale katikati ya dimba kumpa somo la ziada ndugu yangu Abou Diaby
jinsi ya kupata pointi tatu muhimu hata pale inapoonekana zingepotea,yuko wapi
Sol Campbell ammpe somo la ziada Laurent Cocilienly anapolala siku ya mviga
pale Wimbley,wapi Dennis Bergkapm ampe Vanpersie somo la ziada kwamba sio kila
mahali atakuta nyasi za kijani sio kila mahali watamuimba “he scores when he
wants” kama ilivyo sasa kwenye mitaa na
barabara za Brayantwoods,Gillesple hakika ukiyawaza haya lazima uhisi
unachanganyikiwa.
Ujenzi wa moja kati ya viwanja
vizuri Ulaya uliogharimu takribani pauni za kiingereza million 500 ni
kati ya vitu Wenger anapigiwa upatu kuwa nyuma ya mafanikio yake.Malengo ya
kujenga uwanja ni yale yale kuendelea kuifanya Arsenal kuwa moja kati ya
timu kubwa Ulaya.
Na kitu pekee ambacho kimeiangusha mpaka sasa
ni jinsi ya kulipa deni la uwanja na kuendelea kulinda heshima yake kama timu
kubwa pale Uingereza na Ulaya kwa ujumla.Njia walizochagua ni pamoja na
kutegemea mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupandisha tiketi za kuingilia
uwanjani na kupunguza mishahara ya wachezaji ambacho kinamuondoa Van Persie japo anajaribu
kukanusha vikali.
Msimu huu tiketi zinonekana kupunguzwa kwa
kiasi kikubwa hasa kwa mechi za nyumbani pamoja na kuuzwa kwa wachezaj nyota na
kununua wale wa bei rahisi washindane na timu ambazo zina mashuga dady kama
vile Chelsea pamoja na Manchester city hakika ukiyawaza haya lazima uhisi
kuchanganyikiwa kama kweli ni shabiki wa ukweli.

Japo ndani ya misimu saba sasa
hawajachukua kikombe chochote lakini bado imeendelea kulinda hadhi yake ulaya
ikifuzu mala 16 ni nyingi zaidi kuliko pengine kuliko timu yoyote ya premier na
chini ya Wenger haionekani kutofanya hivyo hivi karibuni na zaidi kukaribia
kabisa zile siku ambazo Vanpersie na mashabiki wanazitoa.
0 comments:
Post a Comment