
Chama cha mpira wa miguu barani Ulaya kimeanza mchakato wa kuifungulia kesi timu ya S.S.Lazio mara baada ya mashabiki wa kikosi hicho kinachotokea katika jiji la Roma kuonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa wachezaji wa Tottenham Spurz Jermain Defoe na Aaron Lennon.Klabu hiyo inaweza kukumbwa na adhabu kali kutokana na kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kuonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa wachezaji hao wa Tottenham Spurs Jermain Defoe na Aaron Lennon.Taarifa toka katika mtandao wa chama hicho unasema kuwa Chama cha mpira wa miguu barani humo(UEFA) kitakaa chini na kuipitia ripoti ya mwamuzi na kamisaa bila kusahau kamera za uwanjani katika mchezo huo ili kuweza kutoa maamuzi ya namna gani ya kuwaadhibu Lazio.
0 comments:
Post a Comment