Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, August 23, 2012

EL CLASICO NI MECHI NDANI YA MECHI


 


Inaitwa El clasico kikwao kizungu ni the Clasic kikwetu hapa itakuwa na majina mengi kwa kihaya,kichaga,kisambaa na makabila mengi ila kiufupi ni zaidi ya mechi ya mpira wa miguu.El clasico ni mehi inayozikutanisha Real Madrid na Barcelona kwenye michuano ya ndani tofauti na UEF.Achana na mashabiki ambao wanaingia Nou camp ama stadio Santiago Bernabeu huu mpambano unakadiriwa kutazamwa na mshabiki zaidi ya billion moja ulimwenguni kote.Ni mechi ambayo achilia mbali kwamba inagusa nyanja zote za kimaisha za watu lakini pia sio Messi tu ama Christiano Ronaldo ambao ikiisha huwaacha hoi bali hata yule anayeshika ufagio kuhakikisha kila sehemu inakuwa safi.Hakika ni zaidi ya mechi ya mpira wa miguu.

SUPERCOPA NI NINI?
Supercpopa ni mechi inayowakutanisaha bingwa wa ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga na bingwa wa kombe la mfalme kila mwezi wa nane kila mwaka.Msimu wa 2011-2012 mechi kama hii ilichezwa wakati huo Fc Barcelona alikuwa bingwa wa La Liga na Real Madrid alikuwa ndio bingwa wa kombe la mfalme na matokeo Barcelona ilichukua kombe kwa jumla ya magoli 5-4, wakitoka 2-2  Bernabeu  na Nou Camp  wakatoka  3-2 Berbabeu.Safari hii Rea Madrid akishinda La Liga na Barcelona akichukua kombe la mfalme  na ngoma ikianzia Nou Camp na baadae Bernabeu je ni zamu ya  Mourinho?
Mpambano huu kila siku unaongezeka msisimko na mpaka imefika hatua watu wakaupa jina la mechi ndani ya mechi ndio unashangaa? Ndani ya mechi moja kuna mechi nyingine zina endeleam kwa mfano

MOURINHO vs VILANOVA.
Je hii sio mechi? Mwezi wa nane mwaka jana mechi ilikuwa na vurugu nyingi sana japo iliisha kwa Mourinho kupoteza pambano lakini pia akimtia Vilanova vidole vya macho wakati huo akiwa kama kocha msaidizi wa aliyekuwa kocha wa Barcelona wakati huo Pep Guardiola.

MOURINHO.
 


Kutoka the’ Special one’ mpaka sasa akjiita the’ Only one’ huyu jamaa haishi vituko.Anajiita hivi kwa maana kwamba ameshaziteka ligi zote kubwa Ulaya unakataa nini? Ebu cheki  hizi takwimu akichukua makombe 17 na vilabu vitatu tofauti sio the Only One? Alinza na Fc Porto  alichukua ligi mara 2,Portugal cup 1 na champions league 1 na Supercopa1 hapo ni Ureno. Uingereza kazi na Chelsea ligi 2 FA cup 1 kombe la ligi(Carlinmg Cup) 2 na Ngao ya hisani( Community Shield) 1. ITALY. Hapa kazi inafanyika na Inter Milan, alinza na Sirie A 2 (scudetti) Copa Italia 1,Champions league1 na Supercpoa 1 hakika ni yeye pekee.

Mourunho ni mtu anayependa kucheza mind game na tayari ameshasema Superopa kwake sio muhimu na kama angeambiwa achague basi angechagua kilichotokea msimu uliopita apoteze Supercpoa lakini ashinde ligi je ni kweli? Ebu cheki hizi takwimu.Supertaka C.de Oliveira (Porto 2003) Community Shield  (Chelsea 2005)Supercopa Italina (Inter Milan 2008. Ukizingatia kwamba Mourinho ameshashinda La liga pamoja na kombe la mfale ni dhahiri washahiri anaihitaji Supercpoa kwenye CV yake na baada ya” the special one” na the” Only One” nanai anayejua baada ya kulipata atajiita nani?

VILANOVA.
 

 Ameshudia Barcelona ikichukua vikombe vingi chini ya Guardiola na yeye akiwa ni msaidizi tu sasa ni nafasi yake kupata kombe lake la kwanza akiwa kama kocha mkuu.Anaonekana ni mtu makini na ndio maana Barcelona wakamchagua kuwa kama kocha mkuu japo anaonekana mtu mwenye presha sana hasa labda ni kutoka na kivuli cha mafaniko ya Guardiola.Vilonova anataka kuwaonyesha watu Barcelona baada ya Guardiola maisha baada ya Guardiola kwmba yanawezekana.

MESSI vs RONALDO
 


Wachezaji bora kabisa duniani kwa sasa na tayari kuna maswali kwamba tayari wawepo kwenye orodha ya magwiji kama kina Pele ,Maradona na wengine wengi ndio unashangaa nini? Na wakati Dunia na pande za kuu nne  wamezipunguza na kuzifanya mbili? Huku kuna wafuasi wa MESSI na huku kuna wafuasi wa RONALDO. Na miaka 4 sasa iwe ni mchezaji wa  FIFA  ama UEFA  ni hao wawili ndo hupigiwa kula za mwisho japo Messi ameitetea nafasi ya kwanza mara kadhaa.

KIUFUNDI.
 

 
Barcelona au Baugrana ni walewale japo kocha sio Pep Guardiola ila mbinu zao na imani ya mifumo yao ni ile ille tunasema chupa tu ndio mpya mvinyo ni ule ule.Mechi hii mara nyingi hutumika kutambulisha wachezaji wapya kwa hiyo kitu pekee tunachotegemea ni kucheza kwa Alex Song.Barcelona ni ile ile kama tulivyoizoea mfumo wao ukionekana 4-3-3 kwenye makaratasi lakini kitendaji unabadilika na kuwa 3-4-3 kama tulivyoona mechi na Manchester na pia wikiendi walpocheza na Real Sociedad. Messi anaonekana yupo tayari kiakili hasa baada ya kufunga mawili  katika ushindi wa 5-1 kwenye La liga na pia tunategea Davi Villa atampunguzia Messi  zile 44%   za ufungaji  wa magoli msimu uliopita baada ya kurudi kutoka miezi 8 ya majeraha.

Huku Loss Blacos ama Real Madrid nao wanaonekana ni wale wale hasa kutokana na ukweli kwamba hawajafanya usajili japo tunategemea Luka Modric kujiunga nao hivi karibuni. Achilia mbali majeruhi ya mtu kama pepe pia wanaweza wakawapoteza Ricardo Carvaryo na Nuri Sahini ambaye anaelekea Arsenal kwa hiyo tunategemea Raul Arbiol pamoja na Ramos. Mfumo wao wa 4-2-3-1 unaonekana kuendelea kutumika Alonso na Khedira kwenye 2, Ronaldo,Ozil na Dimaria kwenye 3, na Benzema ama Higuain kwenye 1.Sare ya 1-1 na Valencia wanapaswa kushangilia kwani hawakuistahili wakicheza  hovyo kabisa sijui kwamba homa ya El Clasico ilikuwa imeshaingia ila nawategemea kubadilka sana maana hii ni biashara nyingine kabisa.

JE UNAJUA? 
Pique vs Ronaldo

 Je unajua kwamba Real Madrid na Barcelona wameshakutana tayari mara 220, Real Madrid akishinda mara 87 na Barcelona akishinda mara 86 wakienda sare michezo 47.

Je unajua kwamba Barcelona wamepoteza mchezo mmoja tu katika jumla ya michezo 8 waliyocheza hivi karibuni na Real Madrid? Barcelona wameshinda mara 4  na sare 3.

Je unajua Barcelona ameshinda fainali zote tatu mfululizo za Supecopa zilizopita? 2009 alishinda dhidi ya Athletic Bilbao, 2010 alishinda  dhidi ya Sevilla na 2011 akiwafunga Real Madrid.

Je Unajua kwamba Lionel Messi ameshafunga magoili 13 katika El Clasico 19 zote alizocheza? Anapitwa goli 1 na gwiji la Real Madrid  Cesar Rodriguez mwenye magoli 14.

Je unajua Real Madird chini ya Mourinho katika safari nne walizoenda Nou Camp wamepoteza mchezo mmoja tu? Wameshinda 1 na sare 2.

Je unaijua Rekodi ya Mourinho kwenye El Clasico? Ameshinda 2 sare 4 na amefungwa 5.

Je unajua kwamba kadi nyekundu 8 kati ya 10 zilizotolewa kwenye El Clasico zimeenda kwa wachezaji wa Real Madrid?

Je unajua kwamba Christiano Ronaldo amefunga magoli 6 tu katika mechi zote ambazo amekutana na Barcelona? Hii injumuisha mechi alizocheza pia wakati akiwa  na Manchester Utd



0 comments:

Post a Comment