Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, September 29, 2012

NI JUVENTUS TENA

Andrea Pirlo - Juventus
Klabu ya Juventus imezidi kujikita kileleni katika Serie A mara baada ya kuifunga timu ya AS Roma kwa magoli 4-1.Magoli ya Juventus yakifungwa na Andrea Pirlo dakika ya 11,Vidal kwa njia ya penati dakika ya 16,Alessandro Matri katika dakika ya 19 na Giovinco dakika ya 90.Goli la Roma lilifungwa na Pablo Osvaldo kwa njia ya penati katika dakika ya 68.

SUAREZ AMLIPA VAN PERSIE

Hot shot: Luis Suarez scores his first goal
Mshambuliaji Luis Suarez jana alikuwa shujaa wa Liverpool mara baada ya kuifungia timu yake magoli matatu'hat trick' katika pambano lililofanyika pale Carrow Road dhidi ya Norwich City.Suarez aliyekuwa mwiba hapo jana akiongoza mashambulizi pamoja na makinda Suso na kinda mwingine Raheem Sterling walikuwa katika kiwango chao bora kabisa dhidi ya Norwich.
On target: Grant Holt of Norwich City
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa Liverpool mara baada ya mechi tano na wa pili mfululizo katika juma hili ambapo majogoo hao wa Anfield wakiwafunga Norwich kwa magoli 5-2.Magoli hayo yakitiwa kimiani na Luis Suarez katika dakika 2,38,57 huku kiungo Nuri Sahin naye nyota yake ikizidi kung'aa baada ya kuifungia Liverpool goli lake la pili la msimu katika dakika ya 47 kabla ya nahodha Steven Gerrad kuhitimisha karamu ya magoli katika dakika ya 68.
Magoli kwa upande wa Norwich yalifungwa na Morrison dakika 61 na Grant Holt dakika ya 87 aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jackson.

BARCA YAENDELEZA MAKALI HISPANIA

Messi gegen Sevilla
Klabu ya Barcelona iliendeleza makali yake katika Ligi Kuu ya soka nchini Hispania 'La Liga' mara baada ya kuifunga timu ya Sevilla kwa magoli 3-2.Magoli ya Barcelona yalifungwa na Cesc Fabregas katika dakika za 53 na 89 huku mshambuliaji David Villa naye akifunga dakika ya 93 likiwa goli lake la tatu la msimu.

Magoli kwa upande wa Sevilla yalifungwa na Piotr Trochowski dakika ya 26 na Alvaro Negredo dakika ya 48.

BAADA YA MIAKA 23 SPURS YASHINDA OLD TRAFFORD

There it is! Clint Dempsey scored Tottenham's third goal at Old Trafford
\Ilikuwa ni siku ya furaha kwa mashabiki wa klabu ya Tottenham Spurs siku ya jana baada ya kushuhudia timu hiyo ikifanya kitendo cha kuifunga klabu ya Manchester Umited baada ya miaka 23 ambapo mara ya mwisho timu hiyo kuifunga United ilikuwa mwaka 1989 hapo Old Trafford.
Just checking: Sir Alex Ferguson took his United players in at 2-0 down at half-time

Spurs walioingia uwanjani na falsafa tofauti pindi wanapokabiliana na Man united,walionekana kutulia na kucheza kwa kujiamini huku wakishambulia kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza 'counter attack'.Hakuna shaka kuwa Spurs walikuwa na rekodi mbaya sana hapo Old Trafford tangu goli la Gary Lineker mwaka 1989 ambapo timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Margaret Thatcher ndipo ilipoonja ladha ya ushindi na tangu mwaka huo 1989 ushindi wa Spirz Old Trafford ulikuwa ni ndoto.Wakiongozwa na viungo Mousa Dembele,Sandro,Bale,Lennon huku Jermain Defoe akicheza kama mshambuliaji pekee Spurz ilikuwa ni timu bora sana uwanjani hapo jana.

Call it a comeback: Nani pulled a goal back for United after half time
Magoli ya Spurs yalifungwa na Vertonghen 3, Bale 32, Dempsey 52.Huku Nani na Kagawa waliifungia Man United katika dakika za 51 na 53.

PREVIEW:MANCHESTER UNITED VS TOTTENHAM HOTSPURS


 Ready to rumble: Robin van Persie and Gareth Bale

 Habari za timu.
Antonia valencia anaweza kukosekana katika mchezo huu kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.Kocha wa Manchster United Sir Alex Ferguson inabidi aangalie kwa kina kama ataweza kuanza na Rooney baada ya kupona majeraha yaliyomweka nje kwa majuma kadhaa.

Kocha wa Spurs Andre Vias Boas atawarudisha kikosini goli kipa Brad Fiedel ,Gareth Bale na Jermain Defoe waliopumzshwa katikati ya wiki.Kyle Noughton anaweza pia naye kurudi baada ya kukosa mchezo dhidi ya QPR wki iliyopita.

DODOSO ZA MCHEZO.

Hakika Kocha Andre Vias Boas ana kibarua kigumu sana leo achila mbali kwamba mechi inachezwa Old Traford moja kati ya viwanja vigumu kwa timu yeyote kutembelea lakini ukweli ni kwamba Totenham hawajapata ushindi hapa tangu 1989 wakitembelea mara 26 wakinyukwa mara 22 katika mashindano yote waliyokutana na wameshapoteza mara 9 mfululizo hivi karibuni.Hayo ni kwa wale waumini wa takwimu lakini haimaanishi kwamba Spurs hawana nafasi ya kupata ushindi  katika mchezo wa leo.

Kimatokeo uwanjani timu zote zipo vizuri kuelekea mchezo huu achilia mbali ushindi wa kila timu kwenye michezo yao ya kombe la ligi katikati ya wiki lakini Manchester wameshinda michezo 4 mfululizo ya ligi huku Spurs akishinda 2.Ktika michezo yao ya wiki iliyopita ilibidi kila mtu apigane kweli kweli kupata pointi tatu wakitoka katika hali ya kupoteza mchezo na mwisho ushindi katika mechi dhidi ya Liverpool na QPR kwa pamoja.

Hakika mtu muhimu kwa upande wa Spurs leo atakuwa Mousa Dembele kwani achilia mbali uwezo wake anaondelea kuonyesha wiki hadi wiki lakini Mbeliiji huyu itakuwa mara yake ya pili kucheza Old Traford msimu huu mwezi August akija kucheza akiwa na kikiosi cha Fulham na aliwafanya walinzi wa United alichokitaka.

UKWELI KUELEKEA MCHEZO HUU.
Spurs mara ya mwisho kuifunga United ilikuwa mwaka 2001 kwa 3-1 pale White hat lane.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha sasa cha Manchester United kama Dan Welbeck, Deavid de Degea na Phil Jones walikuwa hawajazaliwa wakati Spurs wanaifunga Manchester United kwa mara ya mwisho Old Traford mwaka 1989.

Ryan Giggs ameifunga Spurs magoli 10 ni mengi kuliko aliyoifunga timu yoyote

Manchester United wamepata penati tatu mfululizo katika michezo mitatu ya mwisho na mara ya mwisho Arsenal ndio wamepata penati nne mfululizo mwaka 2007.










KUMBE HATA WAO WANAPANDA DALADALA:Wachezaji wa Manchester City wakisubiri treni kuwahi London kwenye mchezo dhidi ya Fulham


Long haul: Led by Pablo Zabaleta, the players make their way to the train with their luggage


Going loco: The City players wait to board their train to London at Stockport station, with something on Carlos Tevez's phone offering a welcome distractionTime to kill: David Silva is deep in conversation as City head down to London for their match with FulhamTrain spotting: City's players wait for the service to London, where they will hope to improve their indifferent form by beating FulhamBit nippy! Sergio Aguero zips up against the Stockport cold, while James Milner is kept entertained by TevezNo way! Tevez can't believe what's on his screen, while Scott Sinclair is similarly engaged

PREVIEW: ARSENAL VS CHELSEA




 La London derby: Spaniards Santi Cazorla and Fernando Torres go head-to-head

 Ni moja kati ya wiki muhimu sana kwa Arsenal baada ya wiki iliyopita kuwalazimisha mabingwa watetezi Manchester City sare pale Etihad wiki hii watakuwa Emirates kuwakaribisha  watani wao wa jijini London Chelsea na pengine ni wakati mzuri  kumuonyesha kila mtu kwamba wako tayari kwa mbio  za ubingwa msimu huu hawatanii.Mechi yenyewe inaahidi kuwa mechi nzuri na ya kusisimua pengine kuliko msimu uliopita achilia mbali utani wao jijini London lakini Chelsea msimu wako tofauti kutokana na aina ya wachezaji iliyowasajili

Chelsea wanaweza wakawa wameshinda ile vita ya nani ni mfalme na fahari ya jiji la London kwa kuchukua UEFA Champions league msimu uliopita lakini kitu pekee kinachomsumbua na kumtoa mate mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic ni mpira Wenger. Mpira Wenger umemlazimisha Abramovic kufungua pochi na kuwaleta Eden Hazard,Marko Marin,Oscar the new Kaka’ na japo Marin bado hajacheza lakini tayari hao waili wameshaonyesha thamani zao kwa muda mchache.

Didier Drogba vs Arsenal.
 Missing man: Didier Drogba is at Shanghai Shenhua now
Arsenal na Arsene Wenger hatimaye watakuwa na tabasamu kuelekea huu mchezo kwani hatimaye wanaenda kukutana na Chelsea bila Didier Drogba.Tembo huyu ameshawakosesha sana usingizi mashabiki wa Arsenal kwani anaweza kwa msimu huo akawa amepoteza ubora wake lakini mechi dhdi ya Arsenal ikamrudisha.Takwimu zinaonyesha katika michezo 14 aliyocheza dhidi ya Arsenal hajafunga mchezo 1 akifunga michezo 13 ikiwa ni  wastani wa goli 1 kila mchezo hakika Chelsea watamkosa mtum huyu.Drogba ameenda zake Shaghai Shenshua bure na Wenger  anasema nadhani Chelsea wanammisi sana ila sio Arsenal emeshatuumiza sana akikieleza kituo cha Sky sports. Takwimu nyingine zinaonesha Drogba akiwa Chelsea Dhidi ya Arsenal W7,D3,L1 na bila ya Drogba W0,D9,L13 je leo itakuwaaje?

MIPAMBANO MUHIMU LEO.

Eden Hazard vs Karl Jenkison.
 Breakthrough: Jenkinson has established himself in the Arsenal first team
Hakuna shaka kwamba beki huyu wa kulia wa Arsenal Karl Jenkison anaendelea kuimarika siku hadi siku na kuwafanya mashabiki wa Arsenal wasahau kwamaba kuna mtu anaitwa Bacary Sagna na moja kati ya sehemu ambazo Wenger atakuwa na wakati mgumu msimu huu.Mechi 5 zilopita inawezekana amekutana na watu wasumbufu ila sio Eden Hazard  Eden =” the bibilical place which has got natural talents and Wonders”) Hazard = Dangerous = Hatari  na jina la kitabu linasadifu yaliyomo.

Wenger vs Walcott.
 Staying put: Walcott wants to pen a new deal with the Gunners
Achilia mbali kwamba kuna matatizo ya mktaba ambapo Walcott mwenyewe amesemea atasaini hivi karibuni kwani anataka afanye yale ambayo yamefanywa na mtu ambaye anavaa jezi yake na huyu sio mwingine ni Thiery Henry.Wacott anaonekana kazi anaiweza achilia mbali kasi yake  na umaliziaje wake ambao unaimarika siku hadi siku lakini hata takwimu zake dhidi ya  Chelsea mimi nampa nafasi ya kuanza mbele ya Gervnho.Walcott ameendelea kusisistiza kwamba anataka kucheza kama mshambuliaji wa kati na Wenger mwenyewe anasema binafsi anamuona kama mshambuliaji wa kati lakini inabidi awe mstahimilivu kidogo.

David Luiz vs Giroud.
 Worth fighting over: John Terry holds off Jonathan Walters as David Luiz (right) backs off
Arsenal inawezekana wamezipokea kwa shangwe habari za John Terry kusimamishwa mechi 4 na adhabu nyingine ya £220,000 baada  FA kumpata na makosa ya kumbagua Antoni Ferdinand. Olivier Giroud baada ya kusshusha presha baada ya kufunga goli la kwanza akiwa na jezi Arsenal kwenye michuano  ya kombe la ligi na inawezekana asifunge goli leo lakini uwepo wake mbele utawapa wakati mgumu Luiz na Cahili ktuokana na urefu na nguvu zake.

Vermaelen vs Koscielny vs Martesacker.
 Laurent Koscielny
Hakuna wakati mashabiki wa Arsenal na Arsene Wenger wana wakati mgumu  kama sasa ukiwaambia kati ya mabeki hawa nani aanze nani akae nje kwasababu wote wameonyesha sio tu kustahili kuanza kikosi cha kwanza lakini  pia  ni moja kati ya walinzi mahili kwa sasa ligi kuu ya Premier pale Uingereza.Msimu ulipoanza wengi walikuwa na uamuzi rahisi kumpa Vermaelen na Koscielny nafasi ya kuanza kutokana ubora waomsimu uliopita lakini kuumia kwa Koscielny kumempa nafasi Martesacker kuonyesha kwamba anastahili sio tu kuvaa jezi ya Arsenal lakini pia kuanza kikosi cha kwanza.

Vito Manone Vs Fernando Torres.
 Hot shot: Torres scores against Newcastle
Vito Manone anampa presha ya kutosha kipa namba moja wa Arsenal Wojciech Szcsezny kutokana uwezo ambao anaendelea kuonyesha.Anatakiwa kuendelea kumfanya mzee wenger aendelee kumuamini  hasa uikizingatia anakutana na safu ya ushambuliaji ya Fernando Torres  ambaye ameshaanza ule utaratibu wake wa kufumania nyavu. Vito Manone ni goli kipa mzuri na mashabiki wengi wa Arsenal wangependelea achukue nafasi hiyo moja kwa moja lakini binafsi naona aendelee kuwa msaidizi  mzuri wa Szcsezny kwani italeta ushindani ambao utakuwa na faida kwa Arsenal.

Sehemu ya kiungo.
 Playmaker: Eden Hazard
Sehemu ya kiungo ya Chelsea na Arsenal ndio kwa kiasi kikubwa itaamua mpambano huu kwani atakayeibuka kinara wa hili eneo kwa kiasi kikubwa ameshinda mechi hii.Kwa upande wa Chelsea John Obi Mikel atapewa jukumu alake la kawaida kutoa ulinzi kwa David Luiz na Gael Cahil na Frank Lampard,Oscar au Juan Matta atapewa nafasi ya kusambaza mipira na kutoa ubunifu katika eneo la hatari.Kwa upande wa Arsenal Mikel Arteta natakiwa kuendelea na anachokifnya kwa sasa kwani wengi hawamuongelei ila kwangu ni mtu mihimu sana kwani ndio analeta utulivu  muhimu katikati ya uwanja wakati Abou Diaby anatakiwa kuongeza pale alipoishia wiki iliyopita huku kama Arsenal wanachukua pointi tatu Emirates  leo basi Santiago Rodriguez Carzola analo jawabu.








Thursday, September 27, 2012

WALIKUWA,WAMEKUWA NA WATAENDELA KUWA BORA MUDA WOTE

 

Shirikisho la soka nchini Italia maarufu kama Federazione Italiana Giouco Calcio(FIGC) linatarajia kuwatangaza wachezaji Paolo Maldini,Marco Van Basten na mkongwe Giovanni Trapattoni kama wachezaji bora wa muda wote katika zile tuzo maarufu kama 'Italian Football Hall of Fame' mwaka huu.

Tuzo hizo zitakazofanyika katika jiji la Florence mwaka huu mnamo Disemba 31 zilikuwa na kamati maalumu ambayo ilikaa na kuchagua majina bora XI ya muda wote yaliyokuwa na mchanganyiko wa wachezaji,marefa,makocha na watu wengine mbalimbali waliochangia kukuza soka la Italia.Kamati hiyo ilikuja na majina kama:
 Maldini (Italian ), Van Basten (Uholanzi), Trapattoni (Kocha), Giampiero Boniperti (Mkurugenzi Italia), Luigi Agnolin na Paolo Casarin (Refa wa Italia), Dino Zoff (Mchezaji/kocha), Angelo Schiavio, Concetto Lo Bello, Valentino Mazzola na Nereo Rocca (Katika kumbukumbu).

Mchezaji wa zamani wa AC Milan Paolo Maldini ambaye ameshinda jumla ya mataji 26 katika muda wote wa uchezaji wake akiwa na klabu hiyo ya Milan yakiwemo makombe saba(7) ya Ligi Kuu ya soka nchini Italia,makombe matano(5) ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya,makombe matano ya SuperCup na vilabu bingwa duniani(Intercontinental/FIFA Club World Cup’s)ambayo ni matatu(3).

Kwa upande wa kocha Giovanni Trapatonni naye hayupo nyuma katika rekodi binafsi na mafanikio akiwa ndani na nje ya soka la Italia.Trapattoni ameshinda jumla ya makombe 29 akiwa kama kocha na mchezaji yakiwepo makombe 12 ambayo ameyatwaa katika Ligi mbalimbali katika nchi nne(4)tofauti.Gio ndiye kocha pekee kufanikiwa kushinda makombe yote ya Ulaya ukiacha kombe la Intertoto.Lakini amekwishatwaa makombe matatu(3) tofauti ya Kombe la Ulaya akiwa natimu tofauti.

Kwa upande wa aliyekuwa mchezaji bora wa Ulaya mara tatu(3) na aliyeisaidia timu ya taifa ya Uholanzi kuutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1988 Marco Van Basten naye yumo katika kinyang'anyiro hiko.Van Basten aliyeshinda mataji manne(4) ya Serie A,makombe matatu(3) ya Ulaya akiwa na klabu ya AC Milan amepewa heshima hiyo ya kuchukua tuzo hiyo mwaka huu Disemba ya 31.

Wachezaji waliochaguliwam mwaka huu wataungana na wale wa mwaka jana(2011) waliopewa tuzo kam hiyo ambao ni:
Michel Platini, Roberto Baggio, Marcello Lippi, Arrigo Sacchi, Adriano Galliani, Pierluigi Collina, Gigi Riva, Giuseppe Meazza, Giovanni Ferrari, Silvio Piola, Gaetano Scirea, Artemio Franchi, Ottorino Barassi, Vittorio Pozzo, Enzo Bearzot,Ferruccio Valcareggi, Fulvio Bernardini and Giovanni Mauro.

ASAMOAH AONGOZA KUPIGA PASI ZA MWISHO SERIE A

Kwadwo Asamoah - Juventus
Kwado Asamoah

Mchezaji raia wa Ghana ambaye ameamia klabu ya Juventus msimu huu akitokea klabu ya Udinese Kwado Asamoah ndiye kinara katika kupiga pasi za magoli(Assist) katika Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufufu kama Serie A.Katika orodha hiyo ya wapiga pasi za mwisho wamo pia,

Fransesco Totti   (AS Roma)    Pasi (2)

Mirko Vucinic (AS Roma)       Pasi (2)

Alesio Sestu (Siena)                 Pasi (2)



BADO NIMESIMAMA.Fabrice Muamba azindua kitabu kitakachoelezea maisha yake yote.

 Kitabu hicho cha Fabrice Muamba kitaelezea maisha yake yote likiwemo tukio lile la kuanguka uwanjani na kushindwa kupumua kwa takribani dakika 78.Muamba alitoa jina na jinsi kasha la juu la kitabu litakavyoonekana kwenye ukurasa wake wa twitter likimuonyesha mwenyewe akiivuta jezi ya timu yake ya Bolton ndani ikionekana nguo yenye ujumbe unaosema "Bado nimesimama' na kinatarajia kutoka mwezi
 


 Novemba.Kila mpenzi wa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays English Premier League( EPL) anamkumbuka Fabrice Muamba kwa matukio tofauti uwanjani.Lakini kubwa ambalo mpaka sasa mashabiki na wapenzi wa soka hawajalisahau ni lile kuanguka na kushindwa kupumua kwa dakika takribani 78.Tukio hilo lilitokea mwezi marchi pale katika dimba la White Hat Lane katika mchezo wa kombe la FA uliozikutanisha Bolton Wonderes na Tottenham Hotspurs.Baada ya tukio hilo Muamba alilazwa kwenye hospiltali London Chest Hospital kwa takribani mwezi mmoja kabla ya kutangaza kustaafu rasmi.

Muamba alizaliwa mwaka 1988 Kinshasa Congo kabla ya kwenda na familia yake Uingereza akiwa na umri wa miaka 11.Mwaka 2002 alijiunga na shule ya soka ya Arsenal lakini alifanikwa kucheza mechi moja tu kwenye kikosi cha kwanza katika kombe la ligi.Msimu wa 2006-2007 alipelekwa Birmigham kwa mkopo na hatimaye wakaamua kumbakisha na kumpa mkataba wa miaka mitatu.