

Spurs walioingia uwanjani na falsafa tofauti pindi wanapokabiliana na Man united,walionekana kutulia na kucheza kwa kujiamini huku wakishambulia kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza 'counter attack'.Hakuna shaka kuwa Spurs walikuwa na rekodi mbaya sana hapo Old Trafford tangu goli la Gary Lineker mwaka 1989 ambapo timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Margaret Thatcher ndipo ilipoonja ladha ya ushindi na tangu mwaka huo 1989 ushindi wa Spirz Old Trafford ulikuwa ni ndoto.Wakiongozwa na viungo Mousa Dembele,Sandro,Bale,Lennon huku Jermain Defoe akicheza kama mshambuliaji pekee Spurz ilikuwa ni timu bora sana uwanjani hapo jana.

Magoli ya Spurs yalifungwa na Vertonghen 3, Bale 32, Dempsey 52.Huku Nani na Kagawa waliifungia Man United katika dakika za 51 na 53.
0 comments:
Post a Comment