
Ni moja kati ya wiki muhimu sana kwa Arsenal baada ya wiki
iliyopita kuwalazimisha mabingwa watetezi Manchester City sare pale Etihad wiki
hii watakuwa Emirates kuwakaribisha
watani wao wa jijini London Chelsea na pengine ni wakati mzuri kumuonyesha kila mtu kwamba wako tayari kwa
mbio za ubingwa msimu huu
hawatanii.Mechi yenyewe inaahidi kuwa mechi nzuri na ya kusisimua pengine
kuliko msimu uliopita achilia mbali utani wao jijini London lakini Chelsea
msimu wako tofauti kutokana na aina ya wachezaji iliyowasajili
Chelsea wanaweza wakawa wameshinda ile vita ya nani ni
mfalme na fahari ya jiji la London kwa kuchukua UEFA Champions league msimu
uliopita lakini kitu pekee kinachomsumbua na kumtoa mate mmiliki wa Chelsea
Roman Abramovic ni mpira Wenger. Mpira Wenger umemlazimisha Abramovic kufungua
pochi na kuwaleta Eden Hazard,Marko Marin,Oscar the new Kaka’ na japo Marin
bado hajacheza lakini tayari hao waili wameshaonyesha thamani zao kwa muda
mchache.
Didier Drogba vs Arsenal.

Arsenal na Arsene Wenger hatimaye
watakuwa na tabasamu kuelekea huu mchezo kwani hatimaye wanaenda kukutana na
Chelsea bila Didier Drogba.Tembo huyu ameshawakosesha sana usingizi mashabiki
wa Arsenal kwani anaweza kwa msimu huo akawa amepoteza ubora wake lakini mechi
dhdi ya Arsenal ikamrudisha.Takwimu zinaonyesha katika michezo 14 aliyocheza
dhidi ya Arsenal hajafunga mchezo 1 akifunga michezo 13 ikiwa ni wastani wa goli 1 kila mchezo hakika Chelsea
watamkosa mtum huyu.Drogba ameenda zake Shaghai Shenshua bure na Wenger anasema nadhani Chelsea wanammisi sana ila
sio Arsenal emeshatuumiza sana akikieleza kituo cha Sky sports. Takwimu
nyingine zinaonesha Drogba akiwa Chelsea Dhidi ya Arsenal W7,D3,L1 na bila ya
Drogba W0,D9,L13 je leo itakuwaaje?
MIPAMBANO MUHIMU LEO.
Eden Hazard vs Karl Jenkison.

Hakuna shaka kwamba beki huyu wa kulia wa Arsenal Karl
Jenkison anaendelea kuimarika siku hadi siku na kuwafanya mashabiki wa Arsenal
wasahau kwamaba kuna mtu anaitwa Bacary Sagna na moja kati ya sehemu ambazo
Wenger atakuwa na wakati mgumu msimu huu.Mechi 5 zilopita inawezekana amekutana
na watu wasumbufu ila sio Eden Hazard
Eden =” the bibilical place which has got natural talents and Wonders”)
Hazard = Dangerous = Hatari na jina la
kitabu linasadifu yaliyomo.
Wenger vs Walcott.

Achilia mbali kwamba kuna matatizo ya mktaba ambapo Walcott
mwenyewe amesemea atasaini hivi karibuni kwani anataka afanye yale ambayo
yamefanywa na mtu ambaye anavaa jezi yake na huyu sio mwingine ni Thiery
Henry.Wacott anaonekana kazi anaiweza achilia mbali kasi yake na umaliziaje wake ambao unaimarika siku hadi
siku lakini hata takwimu zake dhidi ya
Chelsea mimi nampa nafasi ya kuanza mbele ya Gervnho.Walcott ameendelea
kusisistiza kwamba anataka kucheza kama mshambuliaji wa kati na Wenger mwenyewe
anasema binafsi anamuona kama mshambuliaji wa kati lakini inabidi awe
mstahimilivu kidogo.
David Luiz vs Giroud.

Arsenal inawezekana wamezipokea kwa shangwe habari za John
Terry kusimamishwa mechi 4 na adhabu nyingine ya £220,000 baada FA kumpata na makosa ya kumbagua Antoni
Ferdinand. Olivier Giroud baada ya kusshusha presha baada ya kufunga goli la
kwanza akiwa na jezi Arsenal kwenye michuano
ya kombe la ligi na inawezekana asifunge goli leo lakini uwepo wake
mbele utawapa wakati mgumu Luiz na Cahili ktuokana na urefu na nguvu zake.
Vermaelen vs Koscielny vs Martesacker.

Hakuna wakati mashabiki wa Arsenal na Arsene Wenger wana
wakati mgumu kama sasa ukiwaambia kati
ya mabeki hawa nani aanze nani akae nje kwasababu wote wameonyesha sio tu
kustahili kuanza kikosi cha kwanza lakini
pia ni moja kati ya walinzi
mahili kwa sasa ligi kuu ya Premier pale Uingereza.Msimu ulipoanza wengi
walikuwa na uamuzi rahisi kumpa Vermaelen na Koscielny nafasi ya kuanza
kutokana ubora waomsimu uliopita lakini kuumia kwa Koscielny kumempa nafasi
Martesacker kuonyesha kwamba anastahili sio tu kuvaa jezi ya Arsenal lakini pia
kuanza kikosi cha kwanza.
Vito Manone Vs Fernando Torres.

Vito Manone anampa presha ya kutosha kipa namba moja wa
Arsenal Wojciech Szcsezny kutokana uwezo ambao anaendelea kuonyesha.Anatakiwa
kuendelea kumfanya mzee wenger aendelee kumuamini hasa uikizingatia anakutana na safu ya
ushambuliaji ya Fernando Torres ambaye
ameshaanza ule utaratibu wake wa kufumania nyavu. Vito Manone ni goli kipa
mzuri na mashabiki wengi wa Arsenal wangependelea achukue nafasi hiyo moja kwa
moja lakini binafsi naona aendelee kuwa msaidizi mzuri wa Szcsezny kwani italeta ushindani
ambao utakuwa na faida kwa Arsenal.
Sehemu ya kiungo.

Sehemu ya kiungo ya Chelsea na Arsenal ndio kwa kiasi kikubwa
itaamua mpambano huu kwani atakayeibuka kinara wa hili eneo kwa kiasi kikubwa
ameshinda mechi hii.Kwa upande wa Chelsea John Obi Mikel atapewa jukumu alake
la kawaida kutoa ulinzi kwa David Luiz na Gael Cahil na Frank Lampard,Oscar au
Juan Matta atapewa nafasi ya kusambaza mipira na kutoa ubunifu katika eneo la
hatari.Kwa upande wa Arsenal Mikel Arteta natakiwa kuendelea na anachokifnya
kwa sasa kwani wengi hawamuongelei ila kwangu ni mtu mihimu sana kwani ndio
analeta utulivu muhimu katikati ya uwanja
wakati Abou Diaby anatakiwa kuongeza pale alipoishia wiki iliyopita huku kama
Arsenal wanachukua pointi tatu Emirates
leo basi Santiago Rodriguez Carzola analo jawabu.
0 comments:
Post a Comment