

Ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa Liverpool mara baada ya mechi tano na wa pili mfululizo katika juma hili ambapo majogoo hao wa Anfield wakiwafunga Norwich kwa magoli 5-2.Magoli hayo yakitiwa kimiani na Luis Suarez katika dakika 2,38,57 huku kiungo Nuri Sahin naye nyota yake ikizidi kung'aa baada ya kuifungia Liverpool goli lake la pili la msimu katika dakika ya 47 kabla ya nahodha Steven Gerrad kuhitimisha karamu ya magoli katika dakika ya 68.
Magoli kwa upande wa Norwich yalifungwa na Morrison dakika 61 na Grant Holt dakika ya 87 aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jackson.
0 comments:
Post a Comment