
Habari za timu.
Antonia valencia anaweza kukosekana katika mchezo huu kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.Kocha wa Manchster United Sir Alex Ferguson inabidi aangalie kwa kina kama ataweza kuanza na Rooney baada ya kupona majeraha yaliyomweka nje kwa majuma kadhaa.
Kocha wa Spurs Andre Vias Boas atawarudisha kikosini goli kipa Brad Fiedel ,Gareth Bale na Jermain Defoe waliopumzshwa katikati ya wiki.Kyle Noughton anaweza pia naye kurudi baada ya kukosa mchezo dhidi ya QPR wki iliyopita.
DODOSO ZA MCHEZO.
Hakika Kocha Andre Vias Boas ana kibarua kigumu sana leo achila mbali kwamba mechi inachezwa Old Traford moja kati ya viwanja vigumu kwa timu yeyote kutembelea lakini ukweli ni kwamba Totenham hawajapata ushindi hapa tangu 1989 wakitembelea mara 26 wakinyukwa mara 22 katika mashindano yote waliyokutana na wameshapoteza mara 9 mfululizo hivi karibuni.Hayo ni kwa wale waumini wa takwimu lakini haimaanishi kwamba Spurs hawana nafasi ya kupata ushindi katika mchezo wa leo.
Kimatokeo uwanjani timu zote zipo vizuri kuelekea mchezo huu achilia mbali ushindi wa kila timu kwenye michezo yao ya kombe la ligi katikati ya wiki lakini Manchester wameshinda michezo 4 mfululizo ya ligi huku Spurs akishinda 2.Ktika michezo yao ya wiki iliyopita ilibidi kila mtu apigane kweli kweli kupata pointi tatu wakitoka katika hali ya kupoteza mchezo na mwisho ushindi katika mechi dhidi ya Liverpool na QPR kwa pamoja.
Hakika mtu muhimu kwa upande wa Spurs leo atakuwa Mousa Dembele kwani achilia mbali uwezo wake anaondelea kuonyesha wiki hadi wiki lakini Mbeliiji huyu itakuwa mara yake ya pili kucheza Old Traford msimu huu mwezi August akija kucheza akiwa na kikiosi cha Fulham na aliwafanya walinzi wa United alichokitaka.
UKWELI KUELEKEA MCHEZO HUU.
Spurs mara ya mwisho kuifunga United ilikuwa mwaka 2001 kwa 3-1 pale White hat lane.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha sasa cha Manchester United kama Dan Welbeck, Deavid de Degea na Phil Jones walikuwa hawajazaliwa wakati Spurs wanaifunga Manchester United kwa mara ya mwisho Old Traford mwaka 1989.
Ryan Giggs ameifunga Spurs magoli 10 ni mengi kuliko aliyoifunga timu yoyote
Manchester United wamepata penati tatu mfululizo katika michezo mitatu ya mwisho na mara ya mwisho Arsenal ndio wamepata penati nne mfululizo mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment