Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, September 27, 2012

BADO NIMESIMAMA.Fabrice Muamba azindua kitabu kitakachoelezea maisha yake yote.

 Kitabu hicho cha Fabrice Muamba kitaelezea maisha yake yote likiwemo tukio lile la kuanguka uwanjani na kushindwa kupumua kwa takribani dakika 78.Muamba alitoa jina na jinsi kasha la juu la kitabu litakavyoonekana kwenye ukurasa wake wa twitter likimuonyesha mwenyewe akiivuta jezi ya timu yake ya Bolton ndani ikionekana nguo yenye ujumbe unaosema "Bado nimesimama' na kinatarajia kutoka mwezi
 


 Novemba.Kila mpenzi wa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays English Premier League( EPL) anamkumbuka Fabrice Muamba kwa matukio tofauti uwanjani.Lakini kubwa ambalo mpaka sasa mashabiki na wapenzi wa soka hawajalisahau ni lile kuanguka na kushindwa kupumua kwa dakika takribani 78.Tukio hilo lilitokea mwezi marchi pale katika dimba la White Hat Lane katika mchezo wa kombe la FA uliozikutanisha Bolton Wonderes na Tottenham Hotspurs.Baada ya tukio hilo Muamba alilazwa kwenye hospiltali London Chest Hospital kwa takribani mwezi mmoja kabla ya kutangaza kustaafu rasmi.

Muamba alizaliwa mwaka 1988 Kinshasa Congo kabla ya kwenda na familia yake Uingereza akiwa na umri wa miaka 11.Mwaka 2002 alijiunga na shule ya soka ya Arsenal lakini alifanikwa kucheza mechi moja tu kwenye kikosi cha kwanza katika kombe la ligi.Msimu wa 2006-2007 alipelekwa Birmigham kwa mkopo na hatimaye wakaamua kumbakisha na kumpa mkataba wa miaka mitatu.









0 comments:

Post a Comment