Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, September 27, 2012

WALIKUWA,WAMEKUWA NA WATAENDELA KUWA BORA MUDA WOTE

 

Shirikisho la soka nchini Italia maarufu kama Federazione Italiana Giouco Calcio(FIGC) linatarajia kuwatangaza wachezaji Paolo Maldini,Marco Van Basten na mkongwe Giovanni Trapattoni kama wachezaji bora wa muda wote katika zile tuzo maarufu kama 'Italian Football Hall of Fame' mwaka huu.

Tuzo hizo zitakazofanyika katika jiji la Florence mwaka huu mnamo Disemba 31 zilikuwa na kamati maalumu ambayo ilikaa na kuchagua majina bora XI ya muda wote yaliyokuwa na mchanganyiko wa wachezaji,marefa,makocha na watu wengine mbalimbali waliochangia kukuza soka la Italia.Kamati hiyo ilikuja na majina kama:
 Maldini (Italian ), Van Basten (Uholanzi), Trapattoni (Kocha), Giampiero Boniperti (Mkurugenzi Italia), Luigi Agnolin na Paolo Casarin (Refa wa Italia), Dino Zoff (Mchezaji/kocha), Angelo Schiavio, Concetto Lo Bello, Valentino Mazzola na Nereo Rocca (Katika kumbukumbu).

Mchezaji wa zamani wa AC Milan Paolo Maldini ambaye ameshinda jumla ya mataji 26 katika muda wote wa uchezaji wake akiwa na klabu hiyo ya Milan yakiwemo makombe saba(7) ya Ligi Kuu ya soka nchini Italia,makombe matano(5) ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya,makombe matano ya SuperCup na vilabu bingwa duniani(Intercontinental/FIFA Club World Cup’s)ambayo ni matatu(3).

Kwa upande wa kocha Giovanni Trapatonni naye hayupo nyuma katika rekodi binafsi na mafanikio akiwa ndani na nje ya soka la Italia.Trapattoni ameshinda jumla ya makombe 29 akiwa kama kocha na mchezaji yakiwepo makombe 12 ambayo ameyatwaa katika Ligi mbalimbali katika nchi nne(4)tofauti.Gio ndiye kocha pekee kufanikiwa kushinda makombe yote ya Ulaya ukiacha kombe la Intertoto.Lakini amekwishatwaa makombe matatu(3) tofauti ya Kombe la Ulaya akiwa natimu tofauti.

Kwa upande wa aliyekuwa mchezaji bora wa Ulaya mara tatu(3) na aliyeisaidia timu ya taifa ya Uholanzi kuutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1988 Marco Van Basten naye yumo katika kinyang'anyiro hiko.Van Basten aliyeshinda mataji manne(4) ya Serie A,makombe matatu(3) ya Ulaya akiwa na klabu ya AC Milan amepewa heshima hiyo ya kuchukua tuzo hiyo mwaka huu Disemba ya 31.

Wachezaji waliochaguliwam mwaka huu wataungana na wale wa mwaka jana(2011) waliopewa tuzo kam hiyo ambao ni:
Michel Platini, Roberto Baggio, Marcello Lippi, Arrigo Sacchi, Adriano Galliani, Pierluigi Collina, Gigi Riva, Giuseppe Meazza, Giovanni Ferrari, Silvio Piola, Gaetano Scirea, Artemio Franchi, Ottorino Barassi, Vittorio Pozzo, Enzo Bearzot,Ferruccio Valcareggi, Fulvio Bernardini and Giovanni Mauro.

0 comments:

Post a Comment