Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, October 6, 2012

PREVIEW: WEST HAM VS ARSENAL




 Saving the best until last? West Ham host Arsenal in a London derby to conclude Saturday's fixtures

 Arsenal baada ya kupoteza mchezo wao kwa wa wapinzani wao wa jiji la London msimu huu dhidi ya Chelsea katika uwanja Emirates wanataka kujirejesha katika nafasi ya kuhesabiwa kama mabingwa ifikapo mwezi wa tano mwaka huu. Mchezo dhidi ya West Ham ni mchezo wa pili katika michezo mitano ambayo Arsenal itacheza msimu huu dhidi ya wapinzani wake wa jiji la London.Mchezo huu unaahidi kuwa mgumu kweli kweli achilia mbali ukweli kwamba West Ham  nao wanatoka  London pia  wanashika nafasi 7 na pointi zake 11 na Arsenal nafasi ya 8 na pointi zake 9 lakini mchezo wa Arsenal dhidi ya kocha wa West Ham Big Sam haukuwahi kuwa rahisi wakishinda mechi 2 tu katika mechi 9.

 Back with a bang: Andy Carroll performed well after coming off the bench in West Ham's 2-1 win at QPR on Monday
West Ham  wamenza vizuri ligi  msimu huu sio vizuri  kuliko Arsenal pekee bali kuliko timu zote ambazo zimepata nafasi ya kushiriki ligi kuu ya premier nchini Uingereza msimu huu.Aina ya mchezo wa West Ham na Sam Allardyce’s ni michezo ile ile ya wakina Stoke City na mbinu ambayo inahitahi watu wenye nguvu juu na chini na mbinu ambayo haimpi shida  Arsenal peke yake bali timu nyingi ligi kuu ya premier pale Uingereza. Na ni mbinu hii ndio imewahakikishia Stoke City maisha marefu ligi kuu ya Premier pale Uingereza tangu wamepanada  na hakika wataendelea kuishi milele na naona  West Ham wanataka kupita njia hii.
 Back in the game: Lukas Podolski levels for Arsenal
Lakini mchezo huu ni mchezo ambao Arsenal kwa kiasi  kikibwa inatarajiwa kuibuka na ushindi hasa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Chelsea lakini pia mchezo dhdi ya Olimpiacos ambao arsenal iliibuka na ushindi wa 3-1 umeweza kuwarudisha Arsenal katika hali ya kawaida kisaikolojia na kuondoa hofu hasa kwa mabeki Thomas Vermaleen na Laurent Koscielny.

Kevin Nolan amekuwa anaiongoza West Ham kwa mfano mpaka sasa kwana anauwezo mkubwa wa kuituliza timu pale inapohitaji na  Ricardo Vaz te hakika amekuwa akifanya kazi ya kuvutia na kutoa ubunifu West Ham inaohitaji hasa akicheza nyuma ya Carton Cole au Andy Carroll.
 Influential: Gervinho hit two and was at the heart of much of Arsenal's attacking guile

Mzee wenger anasema ni kawaida kwa Arsenal kuwabadilisha wachezaji wa pembeni kuwa wachezaji wa kati kama alivyofanya kwa Thiery Henry na Robin Van Persie na sasa kawa Gervinho na Walcott ila atanishangaza sana kama atamtumia Gervinho katikati leo hasa kutokana na aina ya mchezo wa West Ham wanaoucheza ambao unahitaji nguvu zaidi.
 First up: Mohamed Diame fouled Shaun Wright-Phillips and picked up a booking

Sehemu ya kiungo ni sehemu muhimu sana kwa upande wa Arsenal hasa kutokana na aina ya mchezo waocheza wa pasi fupi na za haraka ukijulikana hasa kama mpira Wenger na wanabahati sana mpaka sasa kwamba baada ya kuwepo kwa wasi wasi kukosekana kwa Mikel Artea dhidi ya Olimpiacos katikati ya wiki lakini yuko fiti.

 Good feeling: Podolski is mobbed after his goal

 UKWELI KUULEKEA MCHEZO HUU

Achilia mbali ukweli kwamba Arsenal ndio wafalme wa London lakini mpaka sasa West Ham wameshinda mechi zote dhidi ya wapinzani wake jijini London wakishinda mechi dhidi ya Fulham na QPR.

Japo West Ham hawajapoteza mchezo wowote katika mji  wa London lakini pia usisahau kwamba hawajawahi kuifunga Arsenal tangu 2007.

Baada ya kuona hizi takwimu nilizitegemea sana kutokana na mchezo wanaocheza kwani West Ham ndio timu iliyopata kadi nyingi 15 kuliko timu yoyote katika  premier Ligi ya Uingereza.

Arsenal wanajivunia ukuta mzuri katika ligi mkuu mpaka sasa wakiwa wamefungwa goli moja tu mpaka sasa.

Kama Arsenal wataibuka na ushindi katika mchezo wa leo utakuwa ni ushindi wa 350 tangu Arsenal Wenger ateuliwe kuwa kocha wa Arsenal.
Vikosi vyaweza kuwa hivi.
WEST HAM
Jaaskelainen
Demel, Tomkins, Collins, Taylor
Noble, Diame
Vaz Te, Nolan, Jarvis na
Carroll
ARSENAL
Mannone
Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs

Arteta, Ramsey, Cazorla, Podolski
Gervinho na Giroud













Thursday, October 4, 2012

RYAN SHAWCROSS AITWA KIKOSI CHA ENGLAND

Case for the defence: Stoke's Ryan Shawcross (left) is back in the England squad
Wachezaji Ryan Shawcross,Fraser Forster na Kieran Gibbs wameitwa na kocha Roy Hodgson katika maandalizi ya mechi za makundi kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino na Poland.Akitangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari,kocha Roy amesema kuwa anatumai beki wa kati wa wa klabu ya Soke City Ryan Shawcross ataongeza nguvu hasa katika kipindi hiki ambacho aliyekuwa nahodha wa timu hiyo John Terry akitangaza kustahafu.
New boy: Celtic goalkeeper Fraser Forster (right) gets his maiden call-up
Katika kikosi hicho pia ametajwa kipa wa klabu ya Celtic ya nchini Scotland Fraser Forster.Forster ameitwa kwa mara ya kwanza na hivyo ataungana na makipa wengine kama John Ruddy(Norwich City) na Joe Hart wa Man City.Yumo pia kinda Kieran Gibbs ambaye naye alikwishaichezea Uingereza hapo kabla lakini kutokana na majeruhi amekuwa akikosa kuitwa mara kwa mara atakuwemo katika kikosi hicho akiungana na mabeki kama Leington Baines,Ashley Cole na wengineo.
Kikosi kamili ni pamoja na:

Magolikipa: Fraser Forster, Joe Hart, John Ruddy.

Mabeki: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Kieran Gibbs, Phil Jagielka, Glen Johnson, Joleon Lescott, Ryan Shawcross, Kyle Walker.

Viungo: Michael Carrick, Tom Cleverley, Steven Gerrard, Adam Johnson, Aaron Lennon, Frank Lampard, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott.

Washambuliaji: Andy Carroll, Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Welbeck

PATO ARUDI KUIONGEZEA NGUVU AC MILAN

Alexandre Pato - Milan
Mshambuliaji wa timu ya soka ya AC Milan Alex Pato amerudi katika kikosi hicho kwa kufanya mazoezi na wenzake mara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.Pato aliyejiunga na wenzake leo asubuhi alifanya mazoezi yote pamoja na wenzake na hivyo kumpa ahueni kocha Massimiliano Allegri hasa katika kuelekea katika pambano lao la watani wa jadi 'Derby Della Capitale' dhidi ya Inter Milan.

Ujio wa Pato utawapa nguvu Milan hasa katika sehemu ya ushambuliaji kwani ataungana na nyota wengine katika nafasi hiyo kama Bojan Krkic,Giampaolo Pazzini,Kevin Prince Boateng na wengineo

Tuesday, October 2, 2012

VAN PERSIE AIPA USHINDI MAN UNITED

 Dream team: Wayne Rooney (right) and Robin van Persie (centre) celebrate Manchester United's win at Cluj
Alikuwa ni Robin Van Persie ambaye hapo jana usiku aliihakikishia ushindi klabu ya Man United mara baada ya kufunga mara mbili dhidi ya klabu ya CFR Cluj ya nchini Romania katika ule usiku wa Ulaya.Van Persie alikuwa akitokea pembeni zaidi ili kumpisha mshambuliaji mwenzake Chicharito kusimama katikati aliweza kutumia vyema nafasi alizopata mara baada ya kupata pasi toka kwa mshambuliaji mwenzake Wayne Rooney.
 Nice finish: United's £24m marksman flicks in his second goal of the night following Rooney's superb pass
Akizungumzia magoli hayo mshambuliaji huyo alisema kuwa kwa sasa ana magoli saba aliyoyafunga katika klabu hiyo na anahitaji kufunga magoli mengi zaidi.Katika mechi hiyo ilimalizika kawa Man United kushinda magoli 2-1 ilimshuhudia beki wa Man United wa kati Johnny Evans akipata majeraha na hivyo kuongeza wasiwasi katika kambi ya Man United ambayo kwa sasamimeonekana kuwa na majeruhi wengi.

Majeruhi hao ni pamoja na nahodha Nemanja Vidic,Chriss Smalling,Phil Jones na sasa Johnny Evans.Bado ripoti ya madaktari haijatoka  kuhusu Johnny Evans na kocha Ferguson anahamini kuwa mchezaji huyo atakuwepo katika mechi dhidi ya Newcastle United jumapili hii.

Cech mate: The Chelsea fans enjoyed their first win in the competition since winning it last May
Katika hatua nyingine klabu ya Chelsea iliweza kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Nordsjaelland ya nchini Denmark.Mabao ya Chelsea yalifungwa na Juan Mata katika dakika za 33,82,David Luiz dk ya 79 na Ramirez katika dakika ya 89.
carles puyol fall
Pale Estadio Da Luz klabu ya Barcelona ilipata ushindi mzuri wa ugenini dhidi ya klabu ya Benfica huku shukrani zikiwaendea wachezaji Sanchez na Fabregas walioipatia ushindi timu hiyo.Katika mechi hiyo kulikuwapo na tukio baya la beki wa Barca Carles Puyol kuvunjika mkono na hivyo kuzidi kuipa wasiwasi ngome ya Barca ambayo imekumbwa na majeruhi wengi kama Gerad Pique na beki mwingine Adriano.

KLABU BINGWA ULAYA.CELTIC YAIFUNGA MOSCOW

 Celtic's Samaras breaks ten-man Spartak
Alikuwa ni Mgiriki Giorgos Samaras ambaye ameipa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya klabu ya Spartak Moskva.Magoli ya Celtic yalifungwa na Hooper dakika ya 12,Kombarov katika dakika ya 71 ambaye alijifunga na Samaras dakika ya 90.Huku magoli ya Spartak yalifungwa na Emenike katika dakika za 41na 48.

RATIBA YA KULITEMBEZA KOMBE LA UEFA YAENDELEA

Bologna opens arms to trophy tour
Fabrizio Ravanelli na Gianluca Pagliuca
 Likifanya ziara katika miji mbalimbali Ulaya,Kombe la Klabu Bingwa Ulaya(UEFA Champions League Trophy) limeendelea tena na sasa ikiwa ni zamu ya nchi ya Italia ambapo jiji la Bologna limepata nafasi hiyo ya kutembelewa na kombe hilo.Katika ziara hiyo kivutio kikubwa kilikuwa ni nyota kadha wa kadha waliohusika kulipokea kombe hilo katika jiji la Bologna.

Nyota hao walikuwa ni pamoja na Fabrizio Ravanelli na Gianluca Pagliuca.Ravanelli ambaye alishinda taji hilo akiwa na klabu ya Juventus ya nchini Italia mwaka 1996 alionekana akiwa na furaha sana mara baada ya kulishika kombe hilo la Ulaya.Kwa upande wa Pagliuca ambaye ni balozi wa jiji la Bologna kupitia kampuni ya Unicredit naye alikuwa ni mwenye furaha nyingi mno.

Tukumbuke Pagliuca alifika fainali akiwa na klabu ya Sampdoria mwaka 1992 ambapo fainali walifungwa na klabu ya Barcelona

KWA KHERI MICHAEL BALLACK

 Up for the cup: Ballack enjoyed success with Bayern Munich in his homeland
Katika maisha yangu ya ufuatiliaji soka nimebahatika kuwashuhudia wachezaji wengi bora ambao kwa hakika siyo mimi tu walinifanya niwe nawahi kuangalia mechi katika runinga,bali naamini kwa wapenzi wengi wa kabumbu hali ipo hivyo kuwa walikuwa/wapo tayari hata kuacha shughuli zao za msingi ili kupata kushuhudia baadhi ya mechi ambazo ziliwahusisha nyota kadha wa kadha.
Up for the cup: Ballack enjoyed success with Bayern Munich in his homeland
Nimebahatika kuwaona wachezaji wengi uwanjani hapa duniani katika idara tofauti tofauti kama idara ya Ulinzi(magolikipa,mabeki),idara ya viungo na idara ya ushambuliaji.Katika idara hizo idara ya kiungo ndiyo imekuwa na mvuto sana kwa maana ya kwamba huwa inateka hisia za watu wengi sana.Dunia imepata kuwashuhudia viungo kama kina Sebastian Veron,Diego Semeon,Zinedine Zidane,Xavi,Iniesta,Roy Keane,Patrick Vieira,Stefan Effenberg na wengineo wengi.
... but he led his country with distinction at their own World Cup in 2006
Moja kati ya viungo katika idara hiyo ambayo hatosahaulika na wapenzi wengi wa kabumbu ni kiungo Michael Ballack ambaye amepata kuvichezea vilabu vingi tofauti kama Bayer 04 Levekusen,Bayern Munich,Chelsea na Chemnitz ikiwa ni timu yake ya utoto ametangaza kustaafu soka katika umri wake wa miaka 36.

Ballack ambaye alikuwa anasifika kwa uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali ametangaza uamuzi huo ikiwa ni miaka takribani 17 tangu aanze sok lake katika klabu ya Chemnitz iliyokuwa inatoka katika mji aliokulia wa Gorlitz.Hakika Dunia itamkumbuka Ballack kwa mengi lakini zaidi ni kumtakia mafanikio mema huko aendako.