
Katika maisha yangu ya ufuatiliaji soka nimebahatika kuwashuhudia wachezaji wengi bora ambao kwa hakika siyo mimi tu walinifanya niwe nawahi kuangalia mechi katika runinga,bali naamini kwa wapenzi wengi wa kabumbu hali ipo hivyo kuwa walikuwa/wapo tayari hata kuacha shughuli zao za msingi ili kupata kushuhudia baadhi ya mechi ambazo ziliwahusisha nyota kadha wa kadha.

Nimebahatika kuwaona wachezaji wengi uwanjani hapa duniani katika idara tofauti tofauti kama idara ya Ulinzi(magolikipa,mabeki),idara ya viungo na idara ya ushambuliaji.Katika idara hizo idara ya kiungo ndiyo imekuwa na mvuto sana kwa maana ya kwamba huwa inateka hisia za watu wengi sana.Dunia imepata kuwashuhudia viungo kama kina Sebastian Veron,Diego Semeon,Zinedine Zidane,Xavi,Iniesta,Roy Keane,Patrick Vieira,Stefan Effenberg na wengineo wengi.

Moja kati ya viungo katika idara hiyo ambayo hatosahaulika na wapenzi wengi wa kabumbu ni kiungo Michael Ballack ambaye amepata kuvichezea vilabu vingi tofauti kama Bayer 04 Levekusen,Bayern Munich,Chelsea na Chemnitz ikiwa ni timu yake ya utoto ametangaza kustaafu soka katika umri wake wa miaka 36.
Ballack ambaye alikuwa anasifika kwa uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali ametangaza uamuzi huo ikiwa ni miaka takribani 17 tangu aanze sok lake katika klabu ya Chemnitz iliyokuwa inatoka katika mji aliokulia wa Gorlitz.Hakika Dunia itamkumbuka Ballack kwa mengi lakini zaidi ni kumtakia mafanikio mema huko aendako.
0 comments:
Post a Comment