

Unajua kupigana mtaani? Asikudanganye mtu ngumi za mtaaani
ni ngumu sana tofauti na za ulingoni ambazo sheria zaidi imezitawala katika
kumpata mshindi.Hata nakumbuka Dareck Chisola alishinda kwenye ngumi za mtaani
wakati ametoka kuchakazwa na Vitali
Kitschiko wakapishana maneno na David Haye na baadae kurushiana makonde mbele
ya waandishi wa habari lakini walipokuja ulingoni hakufua dafu alichakazwa vibaya sana. Unajua
ni kwa nini kwasabau ngumi za mtaani hazina mpangilio unacheza vile utakavyoona
itakusadia kushinda pambano na huyu ndiye Wayne Mark Rooney maarufu kama Wazza.Alipoulizwa kuhusu kipaji
cha Rooney wakati alipoifungia Everton mabao nane katika michezo nane kwenye
michuano ya vijana mtafuta vipaji wa Everton Bob Pandleton ambaye ndiye
aliyemleta Everton akiwa na umri wa miaka 9 tu anasema he is a street Fighter.
Mwongo mmoja katika ligi kuu ya premier pale uingereza akiwa
na umri wa miaka 26 ni kitu kikubwa sana na tayari ameshashinda karibu kila
kitu kwa United.Makombe manne ya ligi kuu ya premier Uingereza,amecheza fainali
tatu za klabu bingwa barani Ulaya na kuchukua moja ni kielelezo cha kutosha
kuonyesha ni mchezaji wa aina gani.Roho yake ya kipambanaji inabeba dhana nzima
ya Manchester United na ndio maana hata
kibabu Fergie anaonekana hafurukuti hapa.Hebu fikiria ni Ferguson yupi
unamwambia eti hapa hakuna mchezaji wa kariba yangu hapa united? hebu muulize Roy Keane
kilichomtokea baada ya kauli kama hii lakini Rooney ameambulia kuongezwa
mshahara na kufanywa mchezaji ghali kuliko wote Uingereza.Pale Old traford
wamepita watu kama Cristiano Ronaldo,Roy Keane kina David Beckham wakionekana
kama ndio nembo ya soka sio kwa United pekee lakini hata Uingereza kwa ujumla
waliondoka vibaya lakini sio Rooney. Hatari huyu mtu achiila mbali kwamba
anataka kuonekana mshindi wakati wote lakini pia hajali mbinu anayotumia
kushinda ndio maana kadi nyekundu na Rooney ni wamekuwa ni marafiki
walioshibana kweli kweli

Watu wanasema eti babu Fergie kapunguza ukali siku hizi
lakini mimi naona sio kweli hivi katika ulimwengu huu wa soka utampata wapi sio
Wayne Rooney tu lakini nyota anayelipwa 250,0000 kwa juma halafu yuko tayari
kucheza namba yoyote uwanjani? Amini usiamni leo hata Ronaldo na Messi wasajiliwe United huwezi
kukosa nafasi ya Rooney uwanjani. Wakati kama huu ambao sehemu ya kiungo ya
Uinited haina ubora sana utamuona sana Rooney akifanya ya Carrick na Scholes
halafu wanapata matokeo huyu jamaa ni tarajio la kila kocha. Mwenyewe anasema
anataka kumaliza soka yake akiwa kama mchezaji wa sehemu ya kiungo na hakika
kwenye upigaji wa pasi sahihi kwa wakati sahihi ni eneo ambalo limeongezeka
sana ubora kwa Rooney.Wakati Fulani Jose Mourinho aliposikia Rooney katangaza
anataka kuondoka United unakumbuka alichokisema?” Eti sina hakika sana kama ni
kweli ila kama ni kweli nimeacha simu yangu wazi Ferguson anipigie” Unakumbuka lile goli
la takribani mita 30 alilowafunga
Arsenal ni goli lake la kwanza ligi kuu ya premier pale uingereza wakati ule
yuko Everton? Unajua Wenger alisema nini?” Kwa miaka aliyokuwa nayo hakuna muingereza mwenye kipaji
kikubwa cha kwake hakika ni hazina kwa miaka mingi inayokuja”

Kwa wale waumini wa takwimu Rooney tayari ameshatupia
nyavuni magoli 181 katika michezo 371 aliyoichezea United na kwa uwiano tayari
anawaacha nyuma magwiji kama Sir Bobby Chalton,George Best,Andy Cole pamoja na
kocha wa sasa QPR Mark Hughes. Msimu uliopita amefunga jumla ya magoli 34 na
kusajiliwa kwa Van Persie tayari kumeibua maswali na minongo’no kwamba je atakubali kutoka eneo la ufungaji
lakini Rooney tayari ameshaanza kuonyesha kwa Van Persie kile kile
allichokionyesha kwa Cristiano Ronaldo miaka mitatu iliyopita.Hivi majuzi aliiongoza Uingereza katika mchezo wa
kufuzu fainali za kombe la duinia dhidi ya Poland akichukua nafasi ya Steven
Gerrard aliyekuwa anatumikaia Adhabu ya kadi. Na tayari mijadala mingi imeibuka
kwa je Rooney anatosha kuwa nahodha wa Uingereza? Dhambi ya utovu wa nidhamu
inamtafunaikisemekana ni mtu wa vimwana sana, mvuta bangi na hata akishutumiwa
kucheza kamali na yale ya John Terry hayatasahaulika kirahisi kwene vichwa vya
Wangereza na kubwa kabisa ni lile la kutoifungia timu yake ya taifa goli
hata moja katika fainali za kombe la dunia na labda Brazil imekuja wakati
muafaka kwake.
0 comments:
Post a Comment