
Mshambuliaji wa timu ya soka ya AC Milan Alex Pato amerudi katika kikosi hicho kwa kufanya mazoezi na wenzake mara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.Pato aliyejiunga na wenzake leo asubuhi alifanya mazoezi yote pamoja na wenzake na hivyo kumpa ahueni kocha Massimiliano Allegri hasa katika kuelekea katika pambano lao la watani wa jadi 'Derby Della Capitale' dhidi ya Inter Milan.
Ujio wa Pato utawapa nguvu Milan hasa katika sehemu ya ushambuliaji kwani ataungana na nyota wengine katika nafasi hiyo kama Bojan Krkic,Giampaolo Pazzini,Kevin Prince Boateng na wengineo
0 comments:
Post a Comment