
Arsenal baada ya kupoteza mchezo wao kwa wa wapinzani wao wa
jiji la London msimu huu dhidi ya Chelsea katika uwanja Emirates wanataka
kujirejesha katika nafasi ya kuhesabiwa kama mabingwa ifikapo mwezi wa tano
mwaka huu. Mchezo dhidi ya West Ham ni mchezo wa pili katika michezo mitano
ambayo Arsenal itacheza msimu huu dhidi ya wapinzani wake wa jiji la
London.Mchezo huu unaahidi kuwa mgumu kweli kweli achilia mbali ukweli kwamba
West Ham nao wanatoka London pia wanashika nafasi 7 na pointi zake 11 na Arsenal
nafasi ya 8 na pointi zake 9 lakini mchezo wa Arsenal dhidi ya kocha wa West
Ham Big Sam haukuwahi kuwa rahisi wakishinda mechi 2 tu katika mechi 9.

West Ham wamenza
vizuri ligi msimu huu sio vizuri kuliko Arsenal pekee bali kuliko timu zote
ambazo zimepata nafasi ya kushiriki ligi kuu ya premier nchini Uingereza msimu
huu.Aina ya mchezo wa West Ham na Sam Allardyce’s ni michezo ile ile ya wakina
Stoke City na mbinu ambayo inahitahi watu wenye nguvu juu na chini na mbinu
ambayo haimpi shida Arsenal peke yake
bali timu nyingi ligi kuu ya premier pale Uingereza. Na ni mbinu hii ndio
imewahakikishia Stoke City maisha marefu ligi kuu ya Premier pale Uingereza
tangu wamepanada na hakika wataendelea
kuishi milele na naona West Ham wanataka
kupita njia hii.

Lakini mchezo huu ni mchezo ambao Arsenal kwa kiasi
kikibwa inatarajiwa kuibuka na ushindi hasa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Chelsea
lakini pia mchezo dhdi ya Olimpiacos ambao arsenal iliibuka na ushindi wa 3-1
umeweza kuwarudisha Arsenal katika hali ya kawaida kisaikolojia na kuondoa hofu
hasa kwa mabeki Thomas Vermaleen na Laurent Koscielny.
Kevin Nolan amekuwa anaiongoza West Ham kwa mfano mpaka sasa
kwana anauwezo mkubwa wa kuituliza timu pale inapohitaji na Ricardo Vaz te hakika amekuwa akifanya kazi
ya kuvutia na kutoa ubunifu West Ham inaohitaji hasa akicheza nyuma ya Carton
Cole au Andy Carroll.

Mzee wenger anasema ni kawaida kwa Arsenal kuwabadilisha
wachezaji wa pembeni kuwa wachezaji wa kati kama alivyofanya kwa Thiery Henry
na Robin Van Persie na sasa kawa Gervinho na Walcott ila atanishangaza sana
kama atamtumia Gervinho katikati leo hasa kutokana na aina ya mchezo wa West
Ham wanaoucheza ambao unahitaji nguvu zaidi.

Sehemu ya kiungo ni sehemu muhimu sana kwa upande wa Arsenal
hasa kutokana na aina ya mchezo waocheza wa pasi fupi na za haraka ukijulikana
hasa kama mpira Wenger na wanabahati sana mpaka sasa kwamba baada ya kuwepo kwa
wasi wasi kukosekana kwa Mikel Artea dhidi ya Olimpiacos katikati ya wiki
lakini yuko fiti.

UKWELI KUULEKEA MCHEZO HUU
Achilia mbali ukweli kwamba Arsenal ndio wafalme wa London
lakini mpaka sasa West Ham wameshinda mechi zote dhidi ya wapinzani wake jijini
London wakishinda mechi dhidi ya Fulham na QPR.
Japo West Ham hawajapoteza mchezo wowote katika mji wa London lakini pia usisahau kwamba
hawajawahi kuifunga Arsenal tangu 2007.
Baada ya kuona hizi takwimu nilizitegemea sana kutokana na
mchezo wanaocheza kwani West Ham ndio timu iliyopata kadi nyingi 15 kuliko timu
yoyote katika premier Ligi ya Uingereza.
Arsenal wanajivunia ukuta mzuri katika ligi mkuu mpaka sasa
wakiwa wamefungwa goli moja tu mpaka sasa.
Kama Arsenal wataibuka na ushindi katika mchezo wa leo
utakuwa ni ushindi wa 350 tangu Arsenal Wenger ateuliwe kuwa kocha wa Arsenal.
Vikosi vyaweza kuwa hivi.
WEST HAM
Jaaskelainen
Demel, Tomkins, Collins, Taylor
Noble, Diame
Vaz Te, Nolan, Jarvis na
Carroll
Jaaskelainen
Demel, Tomkins, Collins, Taylor
Noble, Diame
Vaz Te, Nolan, Jarvis na
Carroll
ARSENAL
Mannone
Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs
Arteta, Ramsey, Cazorla, Podolski
Gervinho na Giroud
Mannone
Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs
Arteta, Ramsey, Cazorla, Podolski
Gervinho na Giroud
0 comments:
Post a Comment