Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, October 2, 2012

RATIBA YA KULITEMBEZA KOMBE LA UEFA YAENDELEA

Bologna opens arms to trophy tour
Fabrizio Ravanelli na Gianluca Pagliuca
 Likifanya ziara katika miji mbalimbali Ulaya,Kombe la Klabu Bingwa Ulaya(UEFA Champions League Trophy) limeendelea tena na sasa ikiwa ni zamu ya nchi ya Italia ambapo jiji la Bologna limepata nafasi hiyo ya kutembelewa na kombe hilo.Katika ziara hiyo kivutio kikubwa kilikuwa ni nyota kadha wa kadha waliohusika kulipokea kombe hilo katika jiji la Bologna.

Nyota hao walikuwa ni pamoja na Fabrizio Ravanelli na Gianluca Pagliuca.Ravanelli ambaye alishinda taji hilo akiwa na klabu ya Juventus ya nchini Italia mwaka 1996 alionekana akiwa na furaha sana mara baada ya kulishika kombe hilo la Ulaya.Kwa upande wa Pagliuca ambaye ni balozi wa jiji la Bologna kupitia kampuni ya Unicredit naye alikuwa ni mwenye furaha nyingi mno.

Tukumbuke Pagliuca alifika fainali akiwa na klabu ya Sampdoria mwaka 1992 ambapo fainali walifungwa na klabu ya Barcelona

0 comments:

Post a Comment