
Mnamo tarehe 16 Desemba 1899, Klabu ya A.C Milan ilianzishwa na raia wawili wa Uingereza Herbert Kilpin na Alfred Edwards ikihusisha mIchezo ya “football na cricket” Kutokana na mvutano uliosababishwa na sera ya usajili wa wachezaji wa kigeni mwaka 1908 iligawanyika na kuundwa klabu nyigine ya Inter Milan.
Katika kipindi cha nyuma ikiwa na wachezaji mahiri kama Franco
Beresi, Paolo Maldini,Van Basten ,Inzaghi klabu ya AC Milan iliweza kushinda mataji
mbalimbali kama UEFA Champions league, UEFA Super cup na mengineyo.Katika miaka
ya karibuni A.C Milan imeshindwa kufanya vizuri katika michuano mbalimbali kitu
ambacho kimechangiwa na vitu mbalimbali.
Kutowekeza katika soka la vijana,hili si tatizo kwa Milan pekee bali vilabu vingi nchini
italia.Vikosi vya vilabu hivi vimekuwa vikiundwa na wachezaji wenye umri mkubwa
,mfano katika kikosi kilichoanza na kutwaa ubingwa wa ulaya dhidi ya Liverpool
mwaka 2007 ni wachezaji watatu tu ambao walikuwa chini ya miaka 30, Andrea
Pirlo(27),Riccardo Kaka(25) na Gattuso(27) wachezaji wengine walikuwa wamevuka
umri huo kama Maldini (39), Inzaghi (34) , Seedorf (31), Oddo (31) , Ambrosin
(30) na Nesta (31)
Kuondoka kwa wakongwe ,mwanzoni mwa msimu huu 2012-2013 tumeshuhudia
wakongwe kama Inzaghi, Nesta,Seedorf, Gattuso na Gianluca Zambrotta wakiondoka.Hii imepelekea mabadiliko mengi
katika safu mbalimbali hivyo itachukua muda kwa vijana waliopo kuunda
kombinesheni bora kama ile ya Wa-Sweden Gunnar Gren, Gunnar Nordahl na Nils Liedholm
miaka ya 1950 ama Ruud Gullit, Frank Rijkaard na Van Basten miaka ya
1980 kuondoka kwa wakongwe kumetoa nafasi kwa vijana kama Abate, El –Shaarawy,
De-Sciglio , Acerbi na wengine.
Ukata wa fedha pia umepelekea Milan kuuza wachezaji wake nyota kam
Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva ambao
wamejiunga na P.S.G.Hali hii imesababisha Milan kushindwa kununua wachezaji
nyota kuziba nafasi hizo, hivyo kuwa na
safu mbovu ya mabeki wa kati huku katika ushambuliaji ikimtegemea zaidi Stephan
El-Shaarawy.
Kushindwa kurudisha wachezaji nyota ambao Milan iliwatoa kwa mkopo
kama vile Yoann Gourcuff aliyekuwa Girondins Bordeaux na baadae aliuzwa moja
kwa moja .Wengi tuliamini kuwa angekuwa mbadala wa Ricardo Kaka aliyehamia Real
Madrid.Pia makinda wengine kama Alexandre Merkel aliyeko Genoa na Albert Paloschi (Chievo)
nako kumeifanya klabu ya Milan iendelee na utamaduni wa kupoteza nyota wake
wanaofanya vyema katika vilabu vingine(kwa mkopo) katika Serie A.
Katika kambi ya mazoezi Milanello vijana ndio wametawala hii
inashiria kwamba klabu imedhamiria kuwekeza katika vijana hivyo tutarajie
mafanikio siku zijazo.Klabu kama F.C Barcelona imepata mafanikio kutokana na
kuwekeza katika soka la vijana hivyo kupata mafanikio kutokana na
wachezaji mazao ya academy zao.Kutoa
nafasi kwa kina El-Shaarawy ,De sciglio, Acerb, Niang , Ganz na Bojan
kutasaidia kuunda timu bora ya kiushindani. Hivyo naamini siku moja Milan
itarudia makali yake.
Milan itarudi.
KEEP CALM &
SUPPORT AC MILAN
Forza Milan
ANTONY MALIGANYA
0 comments:
Post a Comment