
Wachezaji Ryan Shawcross,Fraser Forster na Kieran Gibbs wameitwa na kocha Roy Hodgson katika maandalizi ya mechi za makundi kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino na Poland.Akitangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari,kocha Roy amesema kuwa anatumai beki wa kati wa wa klabu ya Soke City Ryan Shawcross ataongeza nguvu hasa katika kipindi hiki ambacho aliyekuwa nahodha wa timu hiyo John Terry akitangaza kustahafu.

Katika kikosi hicho pia ametajwa kipa wa klabu ya Celtic ya nchini Scotland Fraser Forster.Forster ameitwa kwa mara ya kwanza na hivyo ataungana na makipa wengine kama John Ruddy(Norwich City) na Joe Hart wa Man City.Yumo pia kinda Kieran Gibbs ambaye naye alikwishaichezea Uingereza hapo kabla lakini kutokana na majeruhi amekuwa akikosa kuitwa mara kwa mara atakuwemo katika kikosi hicho akiungana na mabeki kama Leington Baines,Ashley Cole na wengineo.
Kikosi kamili ni pamoja na:
Magolikipa: Fraser Forster, Joe Hart, John Ruddy.
Mabeki: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Kieran Gibbs, Phil Jagielka, Glen Johnson, Joleon Lescott, Ryan Shawcross, Kyle Walker.
Viungo: Michael Carrick, Tom Cleverley, Steven Gerrard, Adam Johnson, Aaron Lennon, Frank Lampard, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott.
Washambuliaji: Andy Carroll, Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Welbeck
0 comments:
Post a Comment