Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, December 27, 2012

ANGOLA NA ZAMBIA ZAWA TIMU ZA KWANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI


 

Zikiwa zimebaki takribani wiki tatu kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini,timu za taifa za Angola na Zambia zimekuwa za kwanza kuwasili kwa ajili ya mashindano ya ya kombe hilo.Zambia walisafiri siku ya jana (Boxing Day) kwenda Afika Kusini na waliungana na timu ya Angola ambayo nayo imekwisha wasili nchini Afrika kusini.

Timu zote zimefikia katika jiji la Johanesburg na wanategemewa kuwepo hapo mpaka mashindano hayo yatakapoanza rasmi tarehe 19 mwezi Januari mwakani(2013).Kikosi cha Angola kilijumuisha wachezaji 20 pamoja na viongozi wachache huku kundi kubwa la wachezaji likiwa ni lile la wachezaji wanaochezaji Ligi ya ndani nchini Angola maarufu kama (GiraBola).Mchezaji Geraldo ambaye anachezea Ligi daraja la pili nchini Brazil bado hajawasili.Wachezaji saba toka Ulaya wataungana na kikosi hicho cha Angola na wanatarajiwa kuwepo kambini kabla ya Januari 5.


Wednesday, December 26, 2012

ROONEY KUWA NJE KWA WIKI TATU

 EPL; Wayne Rooney; Swansea City vs Manchester Utd
Mchezaji wa Man Uinted Wayne Rooney atakuwa nje kwa wiki tatu kocha wa Man United Sir Alex Ferguson amethibitisha hilo.Rooney ambaye alicheza mechi ya Ligi wiki iliyopita dhidi ya Swansea aliondolewa katika kikosi cha leo kilichocheza dhidi ya Newcastle United mara baada ya kugundulika kuwa ameumia katika shehemu ya mguu wake katika mazoezi ya timu hiyo jana.
Rooney ataungana na wachezaji wengine ambao ni majeruhi kama Ashley Young,Danny Welbeck na Phili Jones.

MAN UNITED,CHELSEA ZASHINDA EPL WAKATI MAN CITY AKIBANWA MBAVU

 Manchester United's Javier Hernandez beats Newcastle goalkeeper Tim Krul
Klabu ya Man United imejikita kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya soka nchini England kwa kuifunga timu ya Newcatstle United kwa jumla ya mabao 4-3 pambano likifanyika jijini Manchester kunako uwanja wa Old Trafford.Magoli ya United yaliwekwa kimiani na wachezaji Johny Evans  dakika ya 25,Evra 58,Van Persie dakika ya 71 na Chicharito katika dakika ya 90.Magoli kwa upande wa Newcastle yalifungwa na Perch dakika ya 4,goli la kujifunga la Johny Evans dakika ya 28 na Pappis Demba Cisse dakika ya 68.
Juan Mata shoots Chelsea ahead against Norwich at Carrow Road
Katika uwanja wa Carrow Road wenyeji Norwich City waliwakaribisha Chelsea katika pambano kali na la kusisimua na mwisho wa mchezo ni Chelsea kupitia kiungo wake mshambuliaji Juan Mata ambaye aliwahakikishia pointi tatu muhimu klabu hiyo ya darajani na hivyo pambano kumalizika kwa ushindi wa Chelsea wa goli moja kwa bila.
Adam Johnson
Kule uwanja wa mwanga (Stadium of Light) klabu ya Sunderland iliendeleza rekodi yake ya miaka mitatu kwa kutofungwa na klabu ya Man City nyumbani.Sunderland imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Man City goli lililofungwa na mchezaji wa zamani wa klabu ya Man City Adam Johnson.

Monday, December 24, 2012

PARDEW: AMEOBI HAENDI MATAIFA YA AFRIKA

 Shola Ameobi
Kocha wa timu ya soka ya Newcastle United ya nchini England  Allan Pardew amesema kuwa hatomruhusu mchezaji Shola Ameobi kwenda katika michuano ya mataifa ya Afrika inayojulikana kama 'African Cup Of Nations' nchini Afrika Kusini.Ameobi ambaye ameitwa katika kikosi cha wachezaji wa awali wa timu ya taifa ya Nigeria kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo anaweza kupata wakati mgumu wa kupata ruhusa toka kwa kocha huyo ambaye anasema kuwa Newcastle bado inamhitaji sana Ameobi.


WILLIAMS: SIKUDHAMILIA KUMUUMIZA VAN PERSIE

 EPL - Swansea City v Manchester United, Robin Van Persie and Ashley Williams
Beki wa klabu ya soka ya Swansea City ya nchini England na timu ya taifa ya Wales Ashley Williams amesema kuwa kitendo cha kumpiga na mpira Van Persie kichwani hakikuwa cha makusudi hivyo hasichukuliwe vibaya kama alifanya kitendo cha makusudi.Kitendo hicho cha Willliams kilimkasirisha kocha wa Man United Sir Alex Ferguson na kusema kuwa beki wa Swansea Ashley Williams angeweza kumuua Van Persie.Akijibu shutuma hizo za Ferguson,Williams anasema kuwa 'niliangalia kwenye TV(runinga) na Ferguson au mtu yoyote yule anaweza kuwa na maoni yake kuhusu kile kitendo hivyo hakinipi wasiwasi anasema Williams.

Baada ya mechi dhidi ya Man United beki huyo wa Swansea  aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa kitendo cha kumpiga na mpira kichwani Van Persie hakikuwa cha makusudi.

Monday, December 3, 2012

ARSENE BADO ATALITETEA KOMBE LA ARSENAL


Arsene Wenger

 Usicheke hiyo ndio hali halisi kwani sio  tangu kuanza kwa msimu huu na wa jana wala wajuzi na sasa ni kwaida sana.Historia inasema mwaka 1998 Arsenal baada ya michezo 15 walikuwa na point 4 zaidi ya za leo nab ado waliweza kuishika nafasi ya pili kwa hiyo bado wana nafasi kubwa ya kutetea kombe lao kama kawaida.Kwa kuziangalia takwimu hizi huwezi kuuliza kwamba kwa nini wachezaji hawajitumi kwani ni ukweli  usiopingika kwamba Poldoski na hata Santi Carzola wameshapewa mwongozo wa kazi na kile ambacho mwisho wa msimu bosi anataraji kutoka kwao.Hivi jiulize Swali dogo tu ni kwenye timu gani ya Premier  waweza kuupata muunganiko huu wa Arteta,Carzola na Wilshere jibu ni rahisi tu hakuna lakini kwasababu anajua atakachoulizwa mwisho wa msimu hawezi kujitoa kwa tone lao la mwisho.Ni ukweli usiopingika kwamba Arsenal kwa sasa hawanufaiki na uwezo wa mwisho wa wachezaji wao na tatizo ni wimbo ule ule ubinafsi wa Wenger na bodi yake.

Arsenal ni timu ambayo inategemea sana uimara wa sehemu ya kiungo kutokana na mfumo ambao timu inatumia wa 4-3-4 au 4-5-1.Kiungo ya Asrenal bado haijaiva na kuelewana vya kutosha na hatimaye kupiga pasi za haraka na kutengeneza nafasi za kutosha matokeo yake kwa asilimia kubwa ya mchezo mtu ambaye ameachwa mbele anakuwa ametengwa kwa mda wote wa mchezo. Kwa sasa mfumo wa 4-4-1-1 ungeweza sana kuisaidii timu kwa kuwa na ama Carzola na Walcott pembeni, Gervinho bado hawezi kuwa mchezaji Wenger  anamtegemea hata kidogo. Katikati Jack Wilshere na Arteta halafu mbele awepo Poldoski na Giroud mfumo huu sio tu unatukumbusha The Invicibles lakini pia utaleta balansi ya timu kwa hali ya sasa.
 We meet again: Arsenal will travel to Swansea
Mzee Ferguson amekuwa mjanja sana katika eneo hili msimu ulipoanza akianza na mfumo wa 4-2-3-1 mfumo huu nao kwa kiasi kikubwa unahitaji uimara wa sehemu ya kiungo sehemu ambayo United hawako vizuri sana hasa mfumo huo ukimtegemea sana Shinji Kagawa aliyepata majeraha.Kilichofanyika baadae akarudia mfumo wake wa kila siku wa 4-4-2 huu ukitegemea sana Winga sehemu ambayo pia United wako vizuri  huku akiendelea kupata matokeo lakini pia akisubiri kiungo yake kuimarika na kuutumia mfumo  anaokusudia.

Hakika mawazo ya watawala hapa sio ya mashabiki wala wachezaji utamskia mwenyekiti Peter Hill-Wood akikumabia baada ya miaka miwili Arsenal itakuwa moto wa kuotea mbali je wachezaji nyota wataweza kuvumilia? Au watafuta nyayo za wenzao walioshindwa kuvumilia? Kwa  kweli kama unataka uendeleee kufurahia maisha na wenzako usiwe na matarajio makubwa sana na Arsenal kwa sasa unatakiwa uishi kama bodi ya Arsenal na mzee Wenger wanavyotaka kwa sasa kwani hakikia watalitetea kombe lao.

PICHA YA SIKU

Camo king: Mario Balotelli seems to love camouflage, judging by his car, quad bike and now... his onesie