Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, December 27, 2012

ANGOLA NA ZAMBIA ZAWA TIMU ZA KWANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI


 

Zikiwa zimebaki takribani wiki tatu kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini,timu za taifa za Angola na Zambia zimekuwa za kwanza kuwasili kwa ajili ya mashindano ya ya kombe hilo.Zambia walisafiri siku ya jana (Boxing Day) kwenda Afika Kusini na waliungana na timu ya Angola ambayo nayo imekwisha wasili nchini Afrika kusini.

Timu zote zimefikia katika jiji la Johanesburg na wanategemewa kuwepo hapo mpaka mashindano hayo yatakapoanza rasmi tarehe 19 mwezi Januari mwakani(2013).Kikosi cha Angola kilijumuisha wachezaji 20 pamoja na viongozi wachache huku kundi kubwa la wachezaji likiwa ni lile la wachezaji wanaochezaji Ligi ya ndani nchini Angola maarufu kama (GiraBola).Mchezaji Geraldo ambaye anachezea Ligi daraja la pili nchini Brazil bado hajawasili.Wachezaji saba toka Ulaya wataungana na kikosi hicho cha Angola na wanatarajiwa kuwepo kambini kabla ya Januari 5.


0 comments:

Post a Comment