Usicheke hiyo ndio hali halisi kwani sio tangu kuanza kwa msimu huu na wa jana wala
wajuzi na sasa ni kwaida sana.Historia inasema mwaka 1998 Arsenal baada ya
michezo 15 walikuwa na point 4 zaidi ya za leo nab ado waliweza kuishika nafasi
ya pili kwa hiyo bado wana nafasi kubwa ya kutetea kombe lao kama kawaida.Kwa
kuziangalia takwimu hizi huwezi kuuliza kwamba kwa nini wachezaji hawajitumi
kwani ni ukweli usiopingika kwamba
Poldoski na hata Santi Carzola wameshapewa mwongozo wa kazi na kile ambacho
mwisho wa msimu bosi anataraji kutoka kwao.Hivi jiulize Swali dogo tu ni kwenye
timu gani ya Premier waweza kuupata
muunganiko huu wa Arteta,Carzola na Wilshere jibu ni rahisi tu hakuna lakini
kwasababu anajua atakachoulizwa mwisho wa msimu hawezi kujitoa kwa tone lao la
mwisho.Ni ukweli usiopingika kwamba Arsenal kwa sasa hawanufaiki na uwezo wa
mwisho wa wachezaji wao na tatizo ni wimbo ule ule ubinafsi wa Wenger na bodi
yake.
Arsenal ni timu ambayo inategemea sana uimara wa sehemu ya
kiungo kutokana na mfumo ambao timu inatumia wa 4-3-4 au 4-5-1.Kiungo ya
Asrenal bado haijaiva na kuelewana vya kutosha na hatimaye kupiga pasi za
haraka na kutengeneza nafasi za kutosha matokeo yake kwa asilimia kubwa ya
mchezo mtu ambaye ameachwa mbele anakuwa ametengwa kwa mda wote wa mchezo. Kwa
sasa mfumo wa 4-4-1-1 ungeweza sana kuisaidii timu kwa kuwa na ama Carzola na
Walcott pembeni, Gervinho bado hawezi kuwa mchezaji Wenger anamtegemea hata kidogo. Katikati Jack
Wilshere na Arteta halafu mbele awepo Poldoski na Giroud mfumo huu sio tu
unatukumbusha The Invicibles lakini pia utaleta balansi ya timu kwa hali ya
sasa.

Mzee Ferguson amekuwa mjanja sana katika eneo hili msimu
ulipoanza akianza na mfumo wa 4-2-3-1 mfumo huu nao kwa kiasi kikubwa unahitaji
uimara wa sehemu ya kiungo sehemu ambayo United hawako vizuri sana hasa mfumo
huo ukimtegemea sana Shinji Kagawa aliyepata majeraha.Kilichofanyika baadae
akarudia mfumo wake wa kila siku wa 4-4-2 huu ukitegemea sana Winga sehemu
ambayo pia United wako vizuri huku
akiendelea kupata matokeo lakini pia akisubiri kiungo yake kuimarika na
kuutumia mfumo anaokusudia.
Hakika mawazo ya watawala hapa sio ya mashabiki wala
wachezaji utamskia mwenyekiti Peter Hill-Wood akikumabia baada ya miaka miwili
Arsenal itakuwa moto wa kuotea mbali je wachezaji nyota wataweza kuvumilia? Au watafuta
nyayo za wenzao walioshindwa kuvumilia? Kwa kweli kama unataka uendeleee kufurahia maisha
na wenzako usiwe na matarajio makubwa sana na Arsenal kwa sasa unatakiwa uishi
kama bodi ya Arsenal na mzee Wenger wanavyotaka kwa sasa kwani hakikia
watalitetea kombe lao.
0 comments:
Post a Comment