
Beki wa klabu ya soka ya Swansea City ya nchini England na timu ya taifa ya Wales Ashley Williams amesema kuwa kitendo cha kumpiga na mpira Van Persie kichwani hakikuwa cha makusudi hivyo hasichukuliwe vibaya kama alifanya kitendo cha makusudi.Kitendo hicho cha Willliams kilimkasirisha kocha wa Man United Sir Alex Ferguson na kusema kuwa beki wa Swansea Ashley Williams angeweza kumuua Van Persie.Akijibu shutuma hizo za Ferguson,Williams anasema kuwa 'niliangalia kwenye TV(runinga) na Ferguson au mtu yoyote yule anaweza kuwa na maoni yake kuhusu kile kitendo hivyo hakinipi wasiwasi anasema Williams.
Baada ya mechi dhidi ya Man United beki huyo wa Swansea aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa kitendo cha kumpiga na mpira kichwani Van Persie hakikuwa cha makusudi.
0 comments:
Post a Comment