Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, December 26, 2012

MAN UNITED,CHELSEA ZASHINDA EPL WAKATI MAN CITY AKIBANWA MBAVU

 Manchester United's Javier Hernandez beats Newcastle goalkeeper Tim Krul
Klabu ya Man United imejikita kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya soka nchini England kwa kuifunga timu ya Newcatstle United kwa jumla ya mabao 4-3 pambano likifanyika jijini Manchester kunako uwanja wa Old Trafford.Magoli ya United yaliwekwa kimiani na wachezaji Johny Evans  dakika ya 25,Evra 58,Van Persie dakika ya 71 na Chicharito katika dakika ya 90.Magoli kwa upande wa Newcastle yalifungwa na Perch dakika ya 4,goli la kujifunga la Johny Evans dakika ya 28 na Pappis Demba Cisse dakika ya 68.
Juan Mata shoots Chelsea ahead against Norwich at Carrow Road
Katika uwanja wa Carrow Road wenyeji Norwich City waliwakaribisha Chelsea katika pambano kali na la kusisimua na mwisho wa mchezo ni Chelsea kupitia kiungo wake mshambuliaji Juan Mata ambaye aliwahakikishia pointi tatu muhimu klabu hiyo ya darajani na hivyo pambano kumalizika kwa ushindi wa Chelsea wa goli moja kwa bila.
Adam Johnson
Kule uwanja wa mwanga (Stadium of Light) klabu ya Sunderland iliendeleza rekodi yake ya miaka mitatu kwa kutofungwa na klabu ya Man City nyumbani.Sunderland imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Man City goli lililofungwa na mchezaji wa zamani wa klabu ya Man City Adam Johnson.

0 comments:

Post a Comment