Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, August 11, 2012

NGAO YA JAMII-NI MAN CITY DHIDI YA CHELSEA



NGAO YA JAMII



 NI MAN CITY DHIDI YA CHELSEA,TUTARAJIE NINI NGAO YA JAMII?
Ngao ya jamii ya chama cha soka nchini  Uingereza ni mechi ambayo hukutanisha mabingwa wa premier league na mabingwa wa FA katika uwanja utakaochaguliwa na chama cha FA nchini Uingereza.. Ni mechi ambayo kama bingwa wa ligi ikitokea akawa bingwa wa FA pia, timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye ligi inapata fursa ya kushiriki katika mchezo huo na bingwa wa vikombe vy FA na Ligi kuu. Mara nyingi mechi hii inachukuliwa kama ya kirafiki iliyo na mvuto wa kipekee unaotumika zaidi kuonyesha wachezaji wapya wa timu shiriki na wakati huohuo timu iliyo chini kidogo ya ligi kuu na FA na kufahamika zaidi kama. Hii inathibitishwa na kauli aliyoitoa kocha wa Manchester united Sir Alex Furguson kabla ya mechi mwaka 2008 akisema “Siku zote hii ni mechi ambayo hatuchezi kufa na kupona, tunaitumia kama kipimo cha kikosi”
KWA NINI INAITWA NGAO YA JAMII?
Sababu kuu ya kuitwa ngao ya jamii ni mapato yatokanayo na mechi hii ambayo hugawiwa kwa taasisi za kijamii, mapato ya getini pamoja na mapato yanayotokana na mauzo ya haki zote za mechi hii husambazwa kwa vilabu 124 vilivyoshiriki katika kombe la FA kuanzia raundi ya kwanza na kuendelea kwa dhumuni kubwa la kusambaza katika ‘projects’ au miradi mbalimbali ya kijamii. Mechi ya kwanza ya ngao hii ilichezwa msimu wa  1908/09 ikiwakutanisha Manchester United kama bingwa wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Queens Park Rangers kama bingwa wa Southern league ambapo Man U iliibuka na ushindi wa 4-0 baada ya mechi ya kwanza kuisha 1-1 ndani ya uwanja wa Stamford Bridge.
IMETOKEA WAPI?
Ngao ya jamii, wakati huo ngao ya hisani ilianza mwaka 1898/99 ikijulikana kama Sherriff of London Charity Shield ikwakutanisha wanataaluma (Proffessionals) na wasio na taaluma (Amateurs). Lengo kuu la hili ilikuwa ni kumkaribisha Sheriff mpya wa jiji la London. Mfumo mpya ulianza mwaka 1908 ukiwakutanisha bingwa wa ligi daraja la kwanza na wa Southern league (Man U Vs QPR).
Mfumo wa mashindano haya umeendelea kubadilika siku hadi siku: mwaka 1913 ilikuwa ni baina ya wanataaluma na wasio na taaluma, mwaka 1921 ilikuwa ni baina ya bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la FA kwa mara ya kwanza. Mfumo huu uliendelea kubadilika mpaka miaka ya 1920 kwa Proffessionals na amateurs kukutana lakini mnamo mwaka 1930 mfumo wa bingwa wa ligi na wa kombe la FA ukarudi tena mpaka leo hii.
Add caption
Mnamo mwaka 1971, Arsenal ikawa ni timu ya pili kuchukua mara mbili mfululizo tokea lianzishwe na mwaka 1974 Katibu mkuu wa FA, Ted Croker akatengeneza mfumo mpya wa mechi zote kuchezwa katika uwanja wa Wembley ukijumuisha bingwa wa ligi kuu na bingwa wa FA Cup.
NINI MVUTO WA MECHI HII BASI
Mechi hii huashiria ufunguzi wa msimu mpya wa ligi na mashabiki hupata fursa ya kuona wachezaji wapya, jezi pamoja na mfumo mpya utakaotumiwa na timu zao, hivyo basi wadau wengi wa soka wakiwa wamekaa takriban miezi mitatu wanapata fursa ya kuangalia timu zao kwenye mashindano mbalimbali.
VIPI MSIMU HUU?
Kama utakuwa na kumbukumbu Manchester Utd ndiyo mabingwa watetezi wa ngao hii walioipata kwa kuwalaza wapinzani wao Manchester city 3-2 mnamo tarehe 7 agasti 2011. Mwaka huu tutapata fursa ya kushuhudia miamba miwili, Manchester city wakiwa mabingwa wa Ligi kuu ya Premier(EPL) dhidi ya Chelsea wakiwa mabingwa wa FA na UEFA champions league jumapili ya tarehe 12 mwezi huu wa nane katika uwanja wa Villa Park, jijini Birmingham. Manchester city inacheza ikiwa bila kuwa na usajili wowote mkubwa kama ilivyozoeleka  huku wengi wakiongelea suala la usajili kusinzia akiwamo kocha wao Roberto Manchini, pamoja na hilo bado kuna wachezaji wa kuogopwa kama Silva, Yaya Toure na  Aguero. Kwa upande wa pili mambo ni tofauti kidogo, naweza kudiriki kusema Chelsea ni timu yenye safu ya kiungo bora kabisa ligi kuu ikiwaunganisha wachezaji wapya kama Oscar, Marko Marin na Eden Hazard na wa zamani kama Malouda, Ramires, Lampard, Mikel na Essien. Nadhani utakua umepata picha ni jinsi gani mechi hii itakuwa na mvuto tofauti na miaka kadhaa iliyopita.
Mwaka huu wa 2012, Community Shield au ngao ya jamii itachezwa tofauti na Wembley na Millenium kwa sababu ya viwanja hivyo kutumika kwa mashindano ya Olympics. Kuna uwezekano mkubwa kwa mechi hii kupigwa katika viwanja vya Sports Direct Arena (Newcastle), lakini zaidi ni Villa Park huko Birmingham.









VIKOSI TARAJIO
Man City: Hart, Zabaleta, Clichy, Coates, Company, Yaya, Barry, Silva, Nasri, Tevez, Aguero
Chelsea: Cech, A.Cole, Luiz, Terry, Ivanivic, Mikel, Lampard, Marin, Ramires, Hazard, Torres
JE WAJUA?
·         Timu yenye mafanikio zaidi kwa mashindano haya ni Manchester United ikiwa imechukua mara 15 ikifuatiwa na Liverpool mara 10, Arsenal 12, Everton 9 na Spurs 7.
·         Mechi ilyotoa magoli mengi ni kati ya Manchester Utd iliyoifunga Swindon Town 8-4 mwaka 1911.
·         Everton inashikilia rekodi ya kushinda mfululizo (4) toka mwaka 1984-1987 na Man U inashikilia rekodi ya kuwa timu iliyocheza mara nyingi mfululizo kuanzia mwaka 1998-2001.
·         Pat Jennings (Spurs) ni kipa wa kwanza kufunga goli na akiwa katika eneo lake la penati dhidi ya Man U.
·          Leicester city na Brighton ni klabu pekee zilizochukua ngao hii bila kuwa mabingwa wa aidha ligi au FA cup.
IFUATAYO NI ORODHA YA TIMU ZILIZOFANIKIWA KUITWAA NGAO HII.
Manchester United       19
Liverpool                            15
Arsenal                                               12
Everton                                               9
Tottenham Hotspur       7
Chelsea                                               4
Wolves                                4
Manchester City              3
Leeds United                    2
Burnley                                               2
Ni nani ataibuka mbabe mwaka huu?jumapili ya tarehe 12 mwezi wa nane, Villa Park, Manchester City Vs Chelsea.

Friday, August 10, 2012

MANENO YA JOSE MOURIHNO KWA WACHEZAJI WAKE BAADA YA KIPIGO CHA GOLI 5 DHIDI YA BARCELONA


Ilikuwa ni tarehe 29 mwezi Novemba mwaka 2010 pale Camp Nou (Barcelona) majira ya sa 4 hivi usiku kwa saa za Afrika Mashariki wapenzi wa soka duniani walipata kushuhudia moja kati ya mechi zinazotajwa kuwa na mvuto mkubwa duniani na zenye upinzani wa hali ya juu kati ya Fc Barcelona dhidi ya Real Madrid.
Ni mechi inayotambulika kama ‘EL CLASSICO’ pindi timu hizi zinapokutana.Leo katika sports galla namleta kwenu Jerzy Dudek ambaye anatuambia katika kitabu chake kinachoitwa ‘under pressure’ namna hali ilivyokuwa baada ya mechi na hasa maneno ya Mourinho kwa wachezaji wa Madrid baada ya mechi dhidi ya wapinzani wao Barcelona pale Camp Nou.Namnukuu;
It was “chaos in the locker room. Some players were crying, others were arguing, some looked to the ground. Mourinho then entered the locker room. He knew what had happened was awful for the team.
"We looked at him and he said, ‘I know this hurts you. Perhaps for most of you it is the worst loss of your entire career. They are happy now and seem to have won the championship, but have only won one game. This is just the beginning. There is still a long way to get the title.
"'Tomorrow I will give you the day off, but do not stay in your houses. Go with your families, children or friends for a walk around the city. Let people see that you can overcome this. Perhaps people talk about the significance of this defeat, but do not hide behind it. You must show your manhood. After this defeat, we must fight for the title.'"mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi Mourinho aliwaambia wachezaji wake wakale bata kama kawaida pamoja na familia zao,marafiki,ndugu au watu wa karibu wa wachezaji hao na wala wasiogope au kuona aibu kwa kipigo walichopewa dhidi ya Barcelona.Kwa kuimaanisha kauli yake,Mourinho aliwapa mapumziko siku iliyofuata wachezaji wote wa Real Madrid.
Swali; Je ni makocha wangapi wanaweza fanya hivyo kwa kuwaruhusu wachezaji wao kula bata mara tu timu inapofungwa na wapinzani wao wakubwa?


Thursday, August 9, 2012

SUPERCOPPA ITALIANA





Supercoppa Italiana ni mechi ya maandalizi ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Ni mechi pia inayohusisha kikombe ambayo hukutanisha mshindi wa Ligi ya Serie A na mshindi wa kombe la chama cha soka nchini Italia(FIGC) maarufu kama( Coppa Italia) wa msimu uliopita.
Ni mechi ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini Italia ambapo kihistoria tunaambiwa kuwa mechi hizi za ufunguzi zilianzishwa tangu mwaka 1988 ambapo wapenzi wa kabumbu ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia wakishuhudia mechi iliyokuwa kali na kusisimua kati ya AC Milan dhidi ya Sampdoria na Milan kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa moja magoli yakifungwa na Rijkaard, Marco Van Basten na Mannari wakati Gigi Vialli akifunga goli kwa Sampdoria.
Tangu mwaka huo wa 1988 hadi mwaka 2003  mechi hizo za ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini   Italia kwa maana ya Supercoppa Italiana zilikuwa zikifanyika katika viwanja mbalimbali ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia katika viwanja  kama Estadio Olimpico(Roma),San Siro(Milan),Dell Alpi(Turin),pia tulishuhudia kwa mara ya kwanza mechi hiyo ya Supercoppa Italiana ikichezwa nje ya Italia mwaka 1993 ambapo AC Milan wakiwafunga Torino pale Marekani katika uwanja wa Robert F.Kennedy Memorial Stadium.
Baada ya hapo tumeshuhudia mechi za Supercoppa Italiana zikichezwa katika nchi mbalimbali ndani ya mabara tofauti.Mwaka 2002 kwa mara ya kwanza mechi ya Supercoppa Italiana ilichezwa katika ardhi ya bara la Afrika ndani ya nchi ya Libya katika mji wa Tripoli ambapo wapenzi wa kabumbu walishuhudia mechi kati ya Juventus dhidi ya Parma ambapo Juventus waliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 la Parma kwa magoli mawili ya Del Piero na goli la kufutia machozi kwa upande wa Parma likifungwa na Marco Di Vaio.


Na mwaka 2003 Supercoppa Italiana ikahamia tena nchini Marekani ambapo kulikuwa na mechi ya kusisimua kati ya Juventus dhidi ya AC Milan pambano likifanyika katika uwanja wa uliojulikana kama Giants uliopo East Rutherford, New Jersey (New York Market).Katika pambano hilo klabu ya Juventus iliibuka na ushindi wa matuta kwa magoli 5 dhidi ya 3 ya AC Milan baada ya sare ya magoli moja moja katika muda wa kawaida.
Kuanzia mwaka 2009, mechi hiyo ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama serie A ilihamia katika bara la Asia ambapo mechi ya ufunguzi ilihusisha timu za SSC Lazio dhidi ya Inter Milan ambapo SSC Lazio waliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 kwa magoli ya Matuzalem na Rocchi kwa upande wa Lazio na Eto’o kwa upande wa Inter.Pambano hilo likifanyika uwanja wa taifa wa Beijing China maarufu kama Nets Bird au kiota cha ndege.
Bara la Asia na hasa nchi ya China kupitia jimbo la Beijing liliendelea kufaidi mechi za ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu nchini Italia kwani mwaka 2011 wakashuhudia tena mechi nyingine baada ya ile ya mwaka 2009 lakini safari hii pambano likihusisha timu za AC Milan dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Milan nawazungumzia Inter Milan. Pambano likimalizika kwa AC Milan kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 kwa magoli ya Zlatan Ibrahimovic na  Kevin Prince Boateng  huku lile la Inter likifungwa na Wesley Sneidjer.
Msimu huu wa 2012-13, pazia hilo la Serie A linatarajiwa kufunguliwa rasmi August 11 ya mwaka huu (2012) ikiwa ni wiki mbili kabla ya mechi za Serie A kuanza rasmi mnamo August 25 ya mwaka huu ukiwa ni msimu mpya kabisa wa Serie A.Pambano la mwaka huu la Supercoppa Italiana litashuhudia mechi kali na ya kusisimua kati ya mabingwa wa Escudetto Juventus dhidi ya SSC Napoli ambao ni mabingwa wa kombe la chama cha soka nchini Italia (FIGC) maarufu kama Coppa Di Italia.
Ni pambano zuri na la kusisimua na ambalo kwa shabiki yoyote wa soka asingependa kuikosa.Ni pambano linaloambatana na maswali kwa mfano;
Baada ya kufanya vizuri katika Serie A msimu uliopita, Je, Juventus ndiyo wameanza kurejea katika mafankiko yao waliyopata miaka ya nyuma?
Supercopa Italiana 2006
Wakisifiwa kwa soka zuri la kushambulia huku wakitumia staili ya kushambulia kwa kasi nzuri na ya kusisimua, Je, Napoli wataweza kuendeleza aina ya soka lao la kuvutia ambalo tumeliona kwa takribani miaka mitatu mfululizo chini ya kocha Walter Mazzari?
Vipi kuhusu usajiri wa wachezaji wapya waliosajiriwa na vilabu hivi kwa mfano Lucio,Pogba,Asamoah,Isla na Boakye kwa upande wa Juve wakati kwa upande wa Napoli kuna kina Gamberini,Verhami,Lorenzo Insigne pamoja na Bariti toka Vicenza.Je,wachezaji hao wapya wataweza kuzinufaisha vilabu vyao kwa msimu huu mpya wa 2012-13?
Je, kuondoka kwa Ezequel Lavezzi kutaweza kuiathiri Napoli katika staili ya uchezaji wao?
Haya ni maswali machache na mengine mengi ambayo wachunguzi wa mambo wangependa kupata majibu siku ya Jumamosi ya tarehe 11 August mwaka huu 2012.

IFUATAYO NI ORODHA YA MABINGWA WA SUPERCOPA ITALIANA TANGU KUANZISHWA MWAKA 1988 HADI SASA.
Club
Winners
Runners-up
Winning Years
Runners-Up
6
3
1988, 1992, 1993, 1994, 2004, 2011
1996, 1999, 2003
5
4
1989, 2005, 2006, 2008, 2010
2000, 2007, 2009, 2011
4
3
1995, 1997, 2002, 2003
1990, 1998, 2005
3
1
1998, 2000, 2009
2004
2
4
2001, 2007
1991, 2006, 2008, 2010
1
3
1999
1992, 1995, 2002
1
3
1991
1988, 1989, 1994
1
1
1996
2001
1
0
1990

LUCIO-UMRI NAMBA TU KAZI IPO PALEPALE


Lucio: “UMRI NI NAMBA TU KAZI IPO PALEPALE”

Akiwa na miaka 34,hakuna aliyeamini na anayeamini  kuwa Lucio angeweza kusajiliwa na klabu ya Juventus kwa msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A wa 2012-13.Si Rais wa klabu aliyotoka namzungumzia Massimo Morrati wala ile bodi ya wakurugenzi ya Inter Milan  ikiongozwa na mtendaji mkuu  Ernesto Paulilo na Mkurugenzi wa Ufundi Marco Branca na pia wapenzi na wafuatiliaji wa soka la Italia.
Wachambuzi wa soka nchini Italia wanazungumza mengi kuhusu ujio wa Lucio kunako Juventus wakihusisha na kamari nyingine anayofanya mtendaji mkuu kunako klabu hiyo ya Juve namzungumzia Giusseppe Marrota mara baada ya kucheza kamari kama hiyo kwa moja kati wanaotajwa kuwa ni viungo bora kwa sasa duniani pamoja na umri kumtupa mkono namzungumzia “Ginger Maestro” au “Rejista” kama wataliano wamwitavyo Andrea Pirlo.
Kamari hii ya Marrota inakuja wakati ambapo Lucio akiichezea Inter Milan msimu uliopita wa 2011-12,aliweza kuruhusu pamoja na mabeki wengine Maicon,Chivu,Walter Samuel,Nagatomo,Jonathan pamoja na Andrea Ranocchia wakiongozwa na golikipa Julio Cesar jumla ya magoli 55 katika Seie A peke yake.
Swali; Je, Juventus wanamhitaji Lucio?
Kwa mtazamo wangu,ni kweli Juventus wanamhitaji beki aina ya Lucio ili kuongeza nguvu ya kikosi chao  hasa katika  idara ya ulinzi.Hapa simaanishi kuwa mabeki walioipa heshima na rekodi kubwa ndani ya Italia na ulaya kunako klabu ya Juve nawazungumzia Leonardo Bonnuci,Andrea Balzagri,Giorgio Chiellin,Stephen Litestcheiner,Paulo De Ceglie na Martin Caceres ni wabovu au hawana uwezo la hasha.Kwani ni mabeki haohao walioyoifanya Juve  kuwa ni timu pekee iliyomaliza msimu uliopita wa ligi za ulaya pasipo kufungwa mechi yoyote ile ya ligi kuu nchini Italia.
Lucio ni mmoja kati ya mabeki wazoefu sana na ligi ya soka nchini  Italia mana amekwishachezea klabu ya Inter Milan katika Serie A kwa misimu mitatu na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa na Inter ikiwemo ubingwa wa ligi  Escudetto na Copa Di Italia.Faida nyingine ya Lucio mabayo inamwonesha kuwa ni tofauti na mabeki wengine wa Juve ni uzoefu katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu pamoja na timu ya taifa.Lucio ni mwanafainali mara mbili katika klabu bingwa Ulaya akiwa na vilabu viwili tofauti vya Bayer Lverkusen na Inter Milan na akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya akiwa na Inter Milan chini ya kocha Jose Mourinho msimu wa mwaka 2009-10.
Juventus wanashirki michuano mitatu mwaka huu(2012-13) kwa maana ya Serie A,Copa Di Italia na Klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama(UEFA Champions  League).Hivyo ni dhairi kuwa Juve wanahitaji kuwa na kikosi kikubwa ili kuweza kushindana vyema na vilabu vingine ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia.
SWALI LA 2; Lucio ataweza kuanza kikosi cha kwanza?
Jibu ni ndiyo.Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu,ni mabeki wachache sana wamejaliwa kuwa na kila kitu katika mpira.Mfano uwezo wa kuchezea mpira,uwezo wa kukaba nafasi au mtu,uwezo wa kuanzisha mashambulizi na pia uwezo wa kuwa kiongozi uwanjani.Kati ya sifa hizo,Lucio amebarikiwa kuwa nazo zote na hivyo kuwapa wakati mgumu mabeki visiki wa Juve  nawazungumzia Leonardo Bonnuci na Andrea Balzagri ambao wao wanakosa sifa moja tu ya uwezo wa kuanzisha mashambulizi ambayo Lucio anayo kwa kiasi kikubwa na ameonesha hivyo akiwa na vilabu vya Bayer Leverkusen,Bayern Munich pamoja na Inter Milan.Hivyo naiona nafasi ya Lucio katika kikosi cha kwanza cha Juventus.
ANGALIZO.
Bado mwalimu Antonio Conte anaweza kuendelea kuwatumia mabeki walewale waliozoeleka katika mfumo wake wa 3-5-2 kwa maana ya Leo Bonnuci,Balzagri pamoja Chiellin kwa kuwa tayari watu hao  wameshatengeneza umoja(Chemistry) ulioipa Juve mafanikio makubwa sana msimu uliopita wa ligi ya Italia na kufika fainali ya  kombe la Copa Di Italia.Ila uwepo wa Lucio ni chaguo jipya katika safu ya ulinzi kunako kikosi cha kwanza cha mwalimu Conte.
TUTEGEMEE MFUMO MPYA?
Bila shaka kwa maana ya mfumo wa 4-3-3, 4-2-3-1 au 3-4-3 kulingana na mazingira yafuatayo;
·         Wachezaji wanaopatikana katika kikosi cha sasa cha Juventus
·         Majeruhi katika timu
·         Uamuzi wa mwalimu kwa namna anvyoiona timu pinzani
Tukumbuke kuwa Juve wamesajili pia wachezaji wengine katika idara ya kiungo hivyo kuleta chaguzi ya mifumo kwa mwalimu Conte.




 MATEGEMEO.
Juventus kuendelea kufanya vizuri katika michuano watakayoshiriki msimu ujao wa Ligi kuu ya soka nchini Italia(Serie A),Copa  Di Italia pamoja na Klabu bingwa barani Ulaya(UEFA Champions  League).
FORZA JUVE

Wednesday, August 8, 2012

UWEKEZAJI MPYA AC MILAN


UWEKEZAJI MPYA AC MILAN
Akifanya ziara yake kwa mara ya kwanza nchini Urusi baada ya kipindi cha muda mrefu, hatimaye ziara ya aliyekuwa waziri mkuu na mmiliki wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi imeonesha kuzaa matunda.Akiwa Urusi alimtembelea rafiki yake wa muda mrefu Vladimir Putin ambaye ndiye Rais wa nchi ya Urusi na kufanikiwa kuzungumza naye mambo kadha wa kadha ikiwepo kuomba uwekezaji wa makampuni na hata matajiri watakaoweza kuwekeza katika klabu ya AC Milan.
Tetesi zinasema kuwa tayari kampuni ya Gazprom iliyopo nchini Urusi ambayo inashughulika na uchimbaji wa gesi na mafuta imekubali kuwekeza katika klabu hiyo kwa kutoa mkwanja wa takribani hela za ulaya (euro mil 180) kwa kuanzia.Taarifa hizi zimetoka katika chombo kimoja cha habari nchini Hispania kinachojulikana kama AS ambacho kinataarifu pia serikali ya Urusi ndiyo wamiliki wa kampuni hiyo ya Gazprom tangu mwaka 1989.
Kampuni ya Gazprom ilianzishwa mwaka 1989 katika nchi iliyojulikana kama Soviet Union ambayo ilikuja kumeguka na kupatikana  nchi ya  Urusi.Ni kampuni inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya Urusi kwa 50%.Kampuni hiyo inasadikiwa kuwa ina utajiri wa dola za kimarekani billion 44.6(US $44.6 bil).
Lakini kwa taaifa yako tu wewe mpenzi wa soka ni kuwa kampuni hiyo ya Gazprom ndiyo wadhamini wa klabu za Zenith St.Petersburg ya nchini Urusi pamoja na klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani.
Forza Milan kwa udhamini huo.

Tuesday, August 7, 2012

NI KWELI USMANOV ANA DHAMIRA YA KURUDISHA MAKOMBE EMIRATES?


A

lisher Burkhanovich Usmanov huyu jamaa ni mtu hatari sana.Mtoto wa aliyekuwa jaji wa zamaniTashkent Burkhanovich Usamanov nchini Uzbekistan zamani Uzbekrussia.Ni mtu wa tatu kwa utajiri nchini Russia na anashika nafasi ya 28 ulimwengini mbele ya rafii yake kipenzi Roman Abromovic mmiliki wa timu ya Chelsea na kwa sasa akiwa anamiliki takribani 29% ya hisa zote katika timu ya Arsenal nyuma ya tajiri wa kimarekani Stan Kroenke akiwa na 60% lakini uatajiri wake kwa ujumla  unakadiriwa kuwa na kiasi cha paundi za kiingereza 19 billion.

Usmanov
Usmanov amezaliwa mnamo  tarehe 9/9/1953 huko nchini Ukraine  japo amekulia sana Uzbekistan kutokana na shughuili za kikazi za baba yake.Baadae akapata elimu yake katika chuo cha masuala ya mahusiano ya kimataifa kijulikanacho kama Moscow state institutes of international relations akihitimu katika shahada ya masuala ya sheria za kimataifa  na mnamo mwaka 1992 akavuta jiko akimuuoa bibi Irina Viner wa kabila la wajewish.

Ahitimu  shahada ya kwanza kwenye masuala ya mahusianao ya kimataifa.Usmanov Chuoni hapo alibobea na kukijkita zaidi kwenye sheria za kimataifa na baada ya hapo alianza kujihusisha na masuala ya biashara za kimataifa  akianza kutengeneza utajiri wake katika biashara ya kutengeneza mabegi ya plastiki na baadae kuibukia katika biashara ya vyuma akiwa na kampuini inayoitwa Mettaloinvestments ikimpatia umaarufu mkubwa ikimiliki makampuni kama Mikhalovisky Gok,Moldavia metal ,pamoja na Ormel,ogrsk iron ore company akimiliki 45% ya hisa yenye thamani ya #13bilions.

Usmanov amekuwa na nguvu sana mpaka  kwenye Duma na serikarini kwa ujumla. kutokana na utajiri wake na baba yake kufanya kazi kwenye mahakama ya Uzbekistan  zamani ikijulikana kama Uzbekrussia kwa mda mrefu amekuwa na urafiki na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini Urussi na katika vipindi tofauti akiwasaidia hata baadhi kushika hatamu akiwemo waziri wa zamani  na Rais wa sasa wa Urussi Vladimir Puttin.Usmanov kurinda urafiki wake na Puttin alimfukuza mhariri wa moja ya magazeti yake akimtuhumu kuandika habari za uchochezi kumchafua.
Arsenal Miaka ya Mafanikio
.
Usmanov apigwa miaka sita jela 1980.Maisha yake tangu utotoni yaligubikwa na utata na utukutu mwingi  alilotaka yeye ndio aliolofanya hata kama lillihatarisha maisha yake .Kujihusisha kwake na makundi ya kijasusi na bishara haramu alijikuta akitiwa nguvuni kwenda kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Lakini baadae aliachiliwa huru kutokana na Rais wa  wakati  huo Uzbekistan huo Kerimov kuwa na mahusiano mazuri na Rais wa kundi la kijasusi na kuuza madawa haramu  anayeitwa Rakimov ambaye pia alikuwa na mahusiano mazuri na binti wa Usmanov.

Usmanov na Arsenal anasema.”Arsenal ndio timu ya kwanza kuiona kwenye televisheni na nikaipenda” Na moja kwa moja nikatambulishwa kwa Arsenal legends Devid Dein na rafiki yangu na tangu hapo nikatamani sana kuwekeza katika tmu hii kwa sababu wakati ule nilikuwa natafuta timu ya kuwekeza kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Anunua hisa Arsenal. Mnamo mwaka 2007 Devid Dein akamuuzia Usmanov hisa zake 14% chini ya kampuni ya RED and WHITES  na kuondoka kwenye bodi baada ya kutofautiana na viongozi wenzake.Baada ya kununua hisa Usmanov akampa shavu Dein kuwa mwenyekiti wa kampuni ya RED and WHITES.Lakini baadae watu wakahoji mapenzi yake na Arsenal kwamba ataitetea kampuni ambayo imenunua hisa na imeingia mkataba  na Arsenal  ambayo sasa yeye ndo mwenyekiti au Arsenal?  Mapenzi ya Dein na Arsenal sio  ya kujificha akiwa kiongozi zaidi ya miaka 20 kuona hivyo akaamua kuachia ngazi asiharibu uhusiano wake na mashabiki.Itaendelea……………………..

Wednesday, August 1, 2012

KUTOKA NELSON VIVAS MPAKA ROBIN VAN PERSIE NI MISIMU SABA SASA ARSENAL BILA KOMBE




N
akumbuka wakati Fulani nipo chuoni pale chimwaga jengo Fulani maarufu wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wanalifahamu sana baadhi ya vipindi au[ lectures] na mihadhara mbalimbali inafanyika pale kuna kozi flani hivi kila ikiisha wanafunzi wanahisi kuchanganyikiwa.
 Nikamuuliza mwalimu wangu wa somo hilo akaniambia  usishangae sana ukiona kuna kitu nimekufundisha  halafu ukahisi kama unakaribia kuchanganyikiwa hivi ujue unakaribia kuelewa kwasababu wakati wa kuchanganyikiwa ndo wakati wa ubongo kuchambua kipi cha kuelewa na kufuata na kipi sio kitu cha msingi na kuachana nacho.

Nao wahenga wana msemo wao wanasema ukijua tatizo  ujue unakaribia kulipatia jawabu  ndo kitu kinakaribia kutokea pale kwenye viwanja vya London Colney na Emirates kwa pamoja.

Ukitua uwanja wa Emirates leo kitu unachokutana nacho mara moja ni sanamu za watu watatu huyu ni Arsene wenger kocha anayetajwa kuwa ndo mwalimu mwenye mafanikio kuliko wote pale Arsenal na mchango wake kwenye soka la Uingereza haupingiki,akifuatwa na mfaransa mwenzake mfumania nyavu bora wa Arsenal na ligi kuu pale Uingereza Thiery henry pembeni kidogo  ni Toni Adams moja kati ya mabeki wakati bora kabisa pale Arsenal na England.

Hizi ni nembo za ushindi na ushujaa pale Emirates na kwa pamoja huu ni utambulisho kwa mashabiki, makinda wanaochipukia pamoja na wachezaji wapya wanaosajiliwa kujionea moja kati ya vitu vizuri vilivyowahi kutokea katika historia ya timu yao.Ukienda popote vilabu vyenye mafanikio makubwa katika soka watu hawa wana nafasi kubwa sana  lakini si Arsenal ukija hapo mambo ni tofauti kidogo hapa utaishia kuambulia mikanda ya video na simulizi tu hakika ukiwa kama mpenzi wa hii timu hakika nilazima utahisi kuchanganyikiwa.

Hapa majuzi dirisha dogo la mwezi January tulimshuhudia Thiery henry akirudi Arsenal na ukiacha Van persie huyu jamaa ni miongoni mwa watu waliochangia kwa kiasi kikubwa Arsenal kugeuza msimamo waligi ya  premier pale Uingereza kuitoa Arsenal katika kile kinachoaminnika ni kuanza msimu vibaya ambako hakujawahi kushuhudiwa katika historia ya timu hiyo.Huyu alikuwa mtu muhimu sana pale eamirates  ukitoa mzee Wenger, kuanzia London Colney mpaka kwenye vyumba vya kubadilihia nguo,hata wale wachezaji makinda ambao walipata kumuona kupitia luninga zao ama kwenya mikanda ya video hakika iliwaongezea kitu cha ziada.

Hakika anayewza kurishuhudia kwa uzuri kabisa  ni kinda mwenye kipaji cha hali ya Chamberlain anasema” nilipomwona kwa mara ya kwanza nilimshangaa sana nilimuona kama si mchezji kama mimi lakini baada ya kufanya naye mazoezi ndo nikahisi naye mtu”wakati wa mechi na Manchester pale Emirates akasema “wakati tunakimbia naye aliniambia uwezo wangu na amesesma vitu ambavyo naweza kufanya na akanisisitiza niendelee kufanya hivyo.Hivi ndo vitu ambavyo vinaweza kumtofautisha Benick Afobe na Dan Welback ambaye kila siku anafanya mazoezi na watu ambao wamefanya vitu vikubwa na klabu kama kina Ryan Giggs na Paul Scholes sasa Henry  yupo zake marekani lazima uhisi kuna kuchanganyikiwa kama kweli una mapenzi na timu yako.

Nakumbuka wakati ule kuelekea msimu  mpya miaka nane sasa imeepita Arsenal wakianza msimu kama mabingwa watetezi ni kipindi cha kuwaongezea  mikataba Thiery henry,Patric Vieira na Denis Bergkamp huku mikataba yao ikiwa imebaki miaka mitatu na mchezaji pekee anayeuzwa ni Nelson Vivas kama ni leo timu ikiwa Uchina ikijindaa na msimu mpya ungesikia taarifaa za  kuuzwa kwa Sebastiani Squilacci, Maroune Chmakh na imeshaandaa mikataba minono kwa kina Fabregas,Nasri,Walcott pamoja na Vanpersie lakini siku hizi mambo yamebadilika sana wanaotakiwa kubaki ndo wanaondoka wanaotakiwa kuondoka ndo wanabaki katika mazingira haya kama una moyo wenye nyama kama wangu lazima uhisi kuna kuchanganyikiwa.

Arsene wenger na Arsenal wanammisi sana mtu anayeitwa Devid Dein huyu alikuiwa ni zaidi ya makamu mwaenyekiti alikuwa  yuko kwaajili ya kumfanya kila mtu sio tu anafanya kazi bali pia kuifurahia na kuifanya Arsenal pahala pazuri kila mtu angetamani kuishi.Sasa mtu huyu ameondoka na kila kitu pale  kuanzia makombe mpaka mastaa wa timu Van persie ndo anamalizikia katika kile kizazi ambacho kilipokea tuzo ya kuwa timu bora kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka ishirini ya uhai wa Bacrays English Premier League.

Kitu pekee alichobakiziwa ni mpira Wenger na ndo hi ndo jeuri pekee ya mashabiki  kwenye vibanda vya kuangalizia mpira pale Shimo la udongo  jamaa achilia mbali kwamba ndo aliyempa shavu wenger akimtoa Japan huko vichakani Nagoya Grumpus 8 lakini pia ndiye aliyekuwa msaada mkubwa katika kuwaleta nyota kibao Emirates kina Denis,Thiery henry alikuwa ni kama Pini Zahavi wa Arsensal manake alikuwa anazijua fitina kwelikweli.

Huyu jamaa alikuwa ni zaidi ya kiongozi zaidi ya miaka 20 kunzia London Colney mapaka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo angefurahi na kulia na mashabiki pale Old Trafford kwenye kile kipigo cha 8-2 toka kwa mashetani wekundu. Leo kuna kundi la wafanya biashara kundi la wachuuzi wamarekani hawa kina Stan Kroenke hawa unachowaza ndugu yangu Mayenje sio wao wanachowaza wapo kimfuko zaidi kifaida furaha yako sio furaha yao wakati wewe ukilia msimu wa saba hujashanglia kombe wao wako visiwa vya Berbados wanafungua shampeini lazima utahisi kuchanganyikiwa ila kwa mujibu wa mwalimu wangu mambo ndo yanakaribia kukaa vizuri.

 Ukimuona mzee wenger katikati ya pambano pale Wembley anasimama anakaa kama kuna mtu anamchezesha hivi anakunywa maji anatema anatupa chupa yenyewe kabisa kachanganyikiwa  na unaweza kusema ni mtu wa jabu sana au ndo yale ya kuficha mchele mpaka siku ya krismas au IDD huku watu wanakufa njaa manake jinsi ya kumaliza miviga.

 Anajua manake ameshaozesha watoto na ana wajukuuu,achana na sera na mvurugano uliopo kati ya watu wawili wanaohodhi hisa nyingi Stan Kroenke pamoja na Ulshar Usmanov unamuacha vipi Dennis Bergkamp ajiunge na Ajax au Patrick Viera ajiunge kama mkrugenzi wa maendeleo ya michezo huku ukiwahitaji kwa kiasi kikubwa ,fikiria kueleke mchezo Fulani wa ligi na labda Manchester city pale uwanja wa Ethadi huku Fabregas akiwa na mawazo kuelekea mchezo huo akicheki pembeni kuna Patrick Viera akitabasamu nakumuelezea jinsi walivyompiga City nje ndani katika ule msimu anamaliza vita kama ilivyoanza ni msimu ambao Arsenal wanamaliza wakiwa hwajapoteza mchezo wowote sio Highbury wala Oldtraford.
Kuna wakati Fabregas mahesabu yalikuwa hayaendi kabisa kama kachanganyikiwa hivi anatamani kumwambia kitu mzee Wennger anashindwa akicheki pembeni anamwona Craig Eastmond na Watt Sanchez juu kabisa hapo anakutana na lile kundi la machinga kutoka marekani wao lillowaleta mjini ndo haswa wanalifanya kwa asilimia mia moja unachowaza ndugu yangu shimo la Udongo pale sio wao wanachowaza lazima uhisi kama unachanganyikiwa hivi.

Fabregas kwake  ni kama kukabidhiwa jezi huku akiwa mchezo hujaulewa alipewa jukumu la kuwa baba wakati na yeye alikuwa mtoto aliyehitaji kulelewa alitamani sana lile somo la ziada ambalo Messi,Iniesta,Xavi wanalipata toka kwa akina Guardiola mwisho unajua alisema nini “wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu akitoka baba yangu aliyelala na mama yangu nikazaliwa mimi wewe ndo unafuata” lakini sina budi kusema usiku mwema kama ambavyo Van persie anamwambia leo lazima uhisi kunyanganyikiwa kama kweli una mapenzi ya ukweli na timu yako.

Arsenal ni moja kati ya vijiji ambavyo havina wazee na ndio maana mpaka sasa ni msimu wa saba sasa Wanacheza soka ambalo imekuwa ndo kielelezo cha soka bora ulimwenguni kwa sasa lakini bado hawajaonja vikombe na wameishia kuskia nderemo,vifijo na  na vigelegele kwenye kijiji cha wenzao hapohapo kaskazini mwa LONDON yani Chelsea.

Wako wapi kina Toni Adams,yuko wapi Yule mwanaume wa shoka aliyekuwa tayari kuitumikia Arsenal bila hata senti  pale katikati ya dimba kumpa somo la ziada ndugu yangu Abou Diaby jinsi ya kupata pointi tatu muhimu hata pale inapoonekana zingepotea,yuko wapi Sol Campbell ammpe somo la ziada Laurent Cocilienly anapolala siku ya mviga pale Wimbley,wapi Dennis Bergkapm ampe Vanpersie somo la ziada kwamba sio kila mahali atakuta nyasi za kijani sio kila mahali watamuimba “he scores when he wants”  kama ilivyo sasa kwenye mitaa na barabara za Brayantwoods,Gillesple hakika ukiyawaza haya lazima uhisi unachanganyikiwa.

Ujenzi wa moja kati ya viwanja vizuri  Ulaya uliogharimu takribani pauni za kiingereza million 500 ni kati ya vitu Wenger anapigiwa upatu kuwa nyuma ya mafanikio yake.Malengo ya kujenga  uwanja ni yale yale kuendelea kuifanya Arsenal kuwa moja kati ya timu kubwa Ulaya.

 Na kitu pekee ambacho kimeiangusha mpaka sasa ni jinsi ya kulipa deni la uwanja na kuendelea kulinda heshima yake kama timu kubwa pale Uingereza na Ulaya kwa ujumla.Njia walizochagua ni pamoja na kutegemea mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupandisha tiketi za kuingilia uwanjani na kupunguza mishahara ya wachezaji  ambacho kinamuondoa Van Persie japo anajaribu kukanusha vikali.

 Msimu huu tiketi zinonekana kupunguzwa kwa kiasi kikubwa hasa kwa mechi za nyumbani pamoja na kuuzwa kwa wachezaj nyota na kununua wale wa bei rahisi washindane na timu ambazo zina mashuga dady kama vile Chelsea pamoja na Manchester city hakika ukiyawaza haya lazima uhisi kuchanganyikiwa kama kweli ni shabiki wa ukweli.

Japo Arsenal imekuwa ikishuhudia kuondokewa na nyota wake miaka ya hivi karibuni. Kwa mfano 2007 Thiery henry, 2008 Hleb na Flamini,2009 Adebayor na Kolo Toure,2010 Eduerdo,2011 Fabregas na Nasri,2012 Van persie naye ameshatangaza kutoongeza mkataba.Arsenal imeonekana kutoathirika sana. Mathalani msimu uliopita ikimaliza nafasi moja juu ya wakati wa Fabregas na Nasri.Hata Thiery hivi karibuni anasema nanukuu “ kama shabiki wa Arsenal ningependa kuona VanPersie anabaki lakini hata kama akiondoka Arsenal itaendelea kuwa imara”.Anaendelea wakati ule mimi nilipooondoka kila mtu alilia lakini baada ya hapo Arsenal ilimaliza poits nane zaidi ya msimu niliokuwepo.

Japo ndani ya misimu saba sasa hawajachukua kikombe chochote lakini bado imeendelea kulinda hadhi yake ulaya ikifuzu mala 16 ni nyingi zaidi kuliko pengine kuliko timu yoyote ya premier na chini ya Wenger haionekani kutofanya hivyo hivi karibuni na zaidi kukaribia kabisa zile siku ambazo Vanpersie na mashabiki wanazitoa.