A
|
lisher Burkhanovich Usmanov huyu jamaa ni mtu hatari sana.Mtoto wa aliyekuwa jaji wa zamaniTashkent Burkhanovich Usamanov nchini Uzbekistan zamani Uzbekrussia.Ni mtu wa tatu kwa utajiri nchini Russia na anashika nafasi ya 28 ulimwengini mbele ya rafii yake kipenzi Roman Abromovic mmiliki wa timu ya Chelsea na kwa sasa akiwa anamiliki takribani 29% ya hisa zote katika timu ya Arsenal nyuma ya tajiri wa kimarekani Stan Kroenke akiwa na 60% lakini uatajiri wake kwa ujumla unakadiriwa kuwa na kiasi cha paundi za kiingereza 19 billion.
![]() |
Usmanov |
Ahitimu shahada ya
kwanza kwenye masuala ya mahusianao ya kimataifa.Usmanov Chuoni hapo alibobea
na kukijkita zaidi kwenye sheria za kimataifa na baada ya hapo alianza
kujihusisha na masuala ya biashara za kimataifa akianza kutengeneza utajiri wake katika
biashara ya kutengeneza mabegi ya plastiki na baadae kuibukia katika biashara
ya vyuma akiwa na kampuini inayoitwa Mettaloinvestments ikimpatia umaarufu
mkubwa ikimiliki makampuni kama Mikhalovisky Gok,Moldavia metal ,pamoja na
Ormel,ogrsk iron ore company akimiliki 45% ya hisa yenye thamani ya #13bilions.
Usmanov amekuwa na nguvu sana mpaka
kwenye Duma na serikarini kwa ujumla.
kutokana na utajiri wake na baba yake kufanya kazi kwenye mahakama ya
Uzbekistan zamani ikijulikana kama
Uzbekrussia kwa mda mrefu amekuwa na urafiki na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini
Urussi na katika vipindi tofauti akiwasaidia hata baadhi kushika hatamu akiwemo
waziri wa zamani na Rais wa sasa wa Urussi
Vladimir Puttin.Usmanov kurinda urafiki wake na Puttin alimfukuza mhariri wa
moja ya magazeti yake akimtuhumu kuandika habari za uchochezi kumchafua.
Usmanov apigwa miaka sita jela 1980.Maisha
yake tangu utotoni yaligubikwa na utata na utukutu mwingi alilotaka yeye ndio aliolofanya hata kama
lillihatarisha maisha yake .Kujihusisha kwake na makundi ya kijasusi na bishara
haramu alijikuta akitiwa nguvuni kwenda kutumikia kifungo cha miaka sita jela.
Lakini baadae aliachiliwa huru kutokana na Rais wa wakati
huo Uzbekistan huo Kerimov kuwa na mahusiano mazuri na Rais wa kundi la
kijasusi na kuuza madawa haramu
anayeitwa Rakimov ambaye pia alikuwa na mahusiano mazuri na binti wa
Usmanov.
Usmanov na Arsenal anasema.”Arsenal
ndio timu ya kwanza kuiona kwenye televisheni na nikaipenda” Na moja kwa moja
nikatambulishwa kwa Arsenal legends Devid Dein na rafiki yangu na tangu hapo
nikatamani sana kuwekeza katika tmu hii kwa sababu wakati ule nilikuwa natafuta
timu ya kuwekeza kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Anunua hisa Arsenal. Mnamo mwaka
2007 Devid Dein akamuuzia Usmanov hisa zake 14% chini ya kampuni ya RED and
WHITES na kuondoka kwenye bodi baada ya
kutofautiana na viongozi wenzake.Baada ya kununua hisa Usmanov akampa shavu
Dein kuwa mwenyekiti wa kampuni ya RED and WHITES.Lakini baadae watu wakahoji
mapenzi yake na Arsenal kwamba ataitetea kampuni ambayo imenunua hisa na
imeingia mkataba na Arsenal ambayo sasa yeye ndo mwenyekiti au Arsenal? Mapenzi ya Dein na Arsenal sio ya kujificha akiwa kiongozi zaidi ya miaka 20 kuona hivyo akaamua kuachia ngazi
asiharibu uhusiano wake na mashabiki.Itaendelea……………………..
0 comments:
Post a Comment