Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, August 9, 2012

SUPERCOPPA ITALIANA





Supercoppa Italiana ni mechi ya maandalizi ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Ni mechi pia inayohusisha kikombe ambayo hukutanisha mshindi wa Ligi ya Serie A na mshindi wa kombe la chama cha soka nchini Italia(FIGC) maarufu kama( Coppa Italia) wa msimu uliopita.
Ni mechi ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini Italia ambapo kihistoria tunaambiwa kuwa mechi hizi za ufunguzi zilianzishwa tangu mwaka 1988 ambapo wapenzi wa kabumbu ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia wakishuhudia mechi iliyokuwa kali na kusisimua kati ya AC Milan dhidi ya Sampdoria na Milan kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa moja magoli yakifungwa na Rijkaard, Marco Van Basten na Mannari wakati Gigi Vialli akifunga goli kwa Sampdoria.
Tangu mwaka huo wa 1988 hadi mwaka 2003  mechi hizo za ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini   Italia kwa maana ya Supercoppa Italiana zilikuwa zikifanyika katika viwanja mbalimbali ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia katika viwanja  kama Estadio Olimpico(Roma),San Siro(Milan),Dell Alpi(Turin),pia tulishuhudia kwa mara ya kwanza mechi hiyo ya Supercoppa Italiana ikichezwa nje ya Italia mwaka 1993 ambapo AC Milan wakiwafunga Torino pale Marekani katika uwanja wa Robert F.Kennedy Memorial Stadium.
Baada ya hapo tumeshuhudia mechi za Supercoppa Italiana zikichezwa katika nchi mbalimbali ndani ya mabara tofauti.Mwaka 2002 kwa mara ya kwanza mechi ya Supercoppa Italiana ilichezwa katika ardhi ya bara la Afrika ndani ya nchi ya Libya katika mji wa Tripoli ambapo wapenzi wa kabumbu walishuhudia mechi kati ya Juventus dhidi ya Parma ambapo Juventus waliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 la Parma kwa magoli mawili ya Del Piero na goli la kufutia machozi kwa upande wa Parma likifungwa na Marco Di Vaio.


Na mwaka 2003 Supercoppa Italiana ikahamia tena nchini Marekani ambapo kulikuwa na mechi ya kusisimua kati ya Juventus dhidi ya AC Milan pambano likifanyika katika uwanja wa uliojulikana kama Giants uliopo East Rutherford, New Jersey (New York Market).Katika pambano hilo klabu ya Juventus iliibuka na ushindi wa matuta kwa magoli 5 dhidi ya 3 ya AC Milan baada ya sare ya magoli moja moja katika muda wa kawaida.
Kuanzia mwaka 2009, mechi hiyo ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama serie A ilihamia katika bara la Asia ambapo mechi ya ufunguzi ilihusisha timu za SSC Lazio dhidi ya Inter Milan ambapo SSC Lazio waliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 kwa magoli ya Matuzalem na Rocchi kwa upande wa Lazio na Eto’o kwa upande wa Inter.Pambano hilo likifanyika uwanja wa taifa wa Beijing China maarufu kama Nets Bird au kiota cha ndege.
Bara la Asia na hasa nchi ya China kupitia jimbo la Beijing liliendelea kufaidi mechi za ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu nchini Italia kwani mwaka 2011 wakashuhudia tena mechi nyingine baada ya ile ya mwaka 2009 lakini safari hii pambano likihusisha timu za AC Milan dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Milan nawazungumzia Inter Milan. Pambano likimalizika kwa AC Milan kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 kwa magoli ya Zlatan Ibrahimovic na  Kevin Prince Boateng  huku lile la Inter likifungwa na Wesley Sneidjer.
Msimu huu wa 2012-13, pazia hilo la Serie A linatarajiwa kufunguliwa rasmi August 11 ya mwaka huu (2012) ikiwa ni wiki mbili kabla ya mechi za Serie A kuanza rasmi mnamo August 25 ya mwaka huu ukiwa ni msimu mpya kabisa wa Serie A.Pambano la mwaka huu la Supercoppa Italiana litashuhudia mechi kali na ya kusisimua kati ya mabingwa wa Escudetto Juventus dhidi ya SSC Napoli ambao ni mabingwa wa kombe la chama cha soka nchini Italia (FIGC) maarufu kama Coppa Di Italia.
Ni pambano zuri na la kusisimua na ambalo kwa shabiki yoyote wa soka asingependa kuikosa.Ni pambano linaloambatana na maswali kwa mfano;
Baada ya kufanya vizuri katika Serie A msimu uliopita, Je, Juventus ndiyo wameanza kurejea katika mafankiko yao waliyopata miaka ya nyuma?
Supercopa Italiana 2006
Wakisifiwa kwa soka zuri la kushambulia huku wakitumia staili ya kushambulia kwa kasi nzuri na ya kusisimua, Je, Napoli wataweza kuendeleza aina ya soka lao la kuvutia ambalo tumeliona kwa takribani miaka mitatu mfululizo chini ya kocha Walter Mazzari?
Vipi kuhusu usajiri wa wachezaji wapya waliosajiriwa na vilabu hivi kwa mfano Lucio,Pogba,Asamoah,Isla na Boakye kwa upande wa Juve wakati kwa upande wa Napoli kuna kina Gamberini,Verhami,Lorenzo Insigne pamoja na Bariti toka Vicenza.Je,wachezaji hao wapya wataweza kuzinufaisha vilabu vyao kwa msimu huu mpya wa 2012-13?
Je, kuondoka kwa Ezequel Lavezzi kutaweza kuiathiri Napoli katika staili ya uchezaji wao?
Haya ni maswali machache na mengine mengi ambayo wachunguzi wa mambo wangependa kupata majibu siku ya Jumamosi ya tarehe 11 August mwaka huu 2012.

IFUATAYO NI ORODHA YA MABINGWA WA SUPERCOPA ITALIANA TANGU KUANZISHWA MWAKA 1988 HADI SASA.
Club
Winners
Runners-up
Winning Years
Runners-Up
6
3
1988, 1992, 1993, 1994, 2004, 2011
1996, 1999, 2003
5
4
1989, 2005, 2006, 2008, 2010
2000, 2007, 2009, 2011
4
3
1995, 1997, 2002, 2003
1990, 1998, 2005
3
1
1998, 2000, 2009
2004
2
4
2001, 2007
1991, 2006, 2008, 2010
1
3
1999
1992, 1995, 2002
1
3
1991
1988, 1989, 1994
1
1
1996
2001
1
0
1990

0 comments:

Post a Comment