Lucio: “UMRI NI NAMBA TU KAZI IPO PALEPALE”
Wachambuzi wa soka nchini Italia wanazungumza mengi kuhusu ujio wa Lucio kunako Juventus wakihusisha na kamari nyingine anayofanya mtendaji mkuu kunako klabu hiyo ya Juve namzungumzia Giusseppe Marrota mara baada ya kucheza kamari kama hiyo kwa moja kati wanaotajwa kuwa ni viungo bora kwa sasa duniani pamoja na umri kumtupa mkono namzungumzia “Ginger Maestro” au “Rejista” kama wataliano wamwitavyo Andrea Pirlo.
Kamari hii ya Marrota inakuja wakati ambapo Lucio akiichezea Inter Milan msimu uliopita wa 2011-12,aliweza kuruhusu pamoja na mabeki wengine Maicon,Chivu,Walter Samuel,Nagatomo,Jonathan pamoja na Andrea Ranocchia wakiongozwa na golikipa Julio Cesar jumla ya magoli 55 katika Seie A peke yake.
Swali; Je, Juventus wanamhitaji Lucio?
Kwa mtazamo wangu,ni kweli Juventus wanamhitaji beki aina ya Lucio ili kuongeza nguvu ya kikosi chao hasa katika idara ya ulinzi.Hapa simaanishi kuwa mabeki walioipa heshima na rekodi kubwa ndani ya Italia na ulaya kunako klabu ya Juve nawazungumzia Leonardo Bonnuci,Andrea Balzagri,Giorgio Chiellin,Stephen Litestcheiner,Paulo De Ceglie na Martin Caceres ni wabovu au hawana uwezo la hasha.Kwani ni mabeki haohao walioyoifanya Juve kuwa ni timu pekee iliyomaliza msimu uliopita wa ligi za ulaya pasipo kufungwa mechi yoyote ile ya ligi kuu nchini Italia.
Lucio ni mmoja kati ya mabeki wazoefu sana na ligi ya soka nchini Italia mana amekwishachezea klabu ya Inter Milan katika Serie A kwa misimu mitatu na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa na Inter ikiwemo ubingwa wa ligi Escudetto na Copa Di Italia.Faida nyingine ya Lucio mabayo inamwonesha kuwa ni tofauti na mabeki wengine wa Juve ni uzoefu katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu pamoja na timu ya taifa.Lucio ni mwanafainali mara mbili katika klabu bingwa Ulaya akiwa na vilabu viwili tofauti vya Bayer Lverkusen na Inter Milan na akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya akiwa na Inter Milan chini ya kocha Jose Mourinho msimu wa mwaka 2009-10.
Juventus wanashirki michuano mitatu mwaka huu(2012-13) kwa maana ya Serie A,Copa Di Italia na Klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama(UEFA Champions League).Hivyo ni dhairi kuwa Juve wanahitaji kuwa na kikosi kikubwa ili kuweza kushindana vyema na vilabu vingine ndani ya Italia na nje ya mipaka ya Italia.
SWALI LA 2; Lucio ataweza kuanza kikosi cha kwanza?
Jibu ni ndiyo.Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu,ni
mabeki wachache sana wamejaliwa kuwa na kila kitu katika mpira.Mfano uwezo wa
kuchezea mpira,uwezo wa kukaba nafasi au mtu,uwezo wa kuanzisha mashambulizi na
pia uwezo wa kuwa kiongozi uwanjani.Kati ya sifa hizo,Lucio amebarikiwa kuwa
nazo zote na hivyo kuwapa wakati mgumu mabeki visiki wa Juve nawazungumzia Leonardo Bonnuci na Andrea
Balzagri ambao wao wanakosa sifa moja tu ya uwezo wa kuanzisha mashambulizi
ambayo Lucio anayo kwa kiasi kikubwa na ameonesha hivyo akiwa na vilabu vya
Bayer Leverkusen,Bayern Munich pamoja na Inter Milan.Hivyo naiona nafasi ya
Lucio katika kikosi cha kwanza cha Juventus.ANGALIZO.
Bado mwalimu Antonio Conte anaweza kuendelea kuwatumia mabeki walewale waliozoeleka katika mfumo wake wa 3-5-2 kwa maana ya Leo Bonnuci,Balzagri pamoja Chiellin kwa kuwa tayari watu hao wameshatengeneza umoja(Chemistry) ulioipa Juve mafanikio makubwa sana msimu uliopita wa ligi ya Italia na kufika fainali ya kombe la Copa Di Italia.Ila uwepo wa Lucio ni chaguo jipya katika safu ya ulinzi kunako kikosi cha kwanza cha mwalimu Conte.
TUTEGEMEE MFUMO MPYA?
Bila shaka kwa maana ya mfumo wa 4-3-3, 4-2-3-1 au 3-4-3 kulingana na mazingira yafuatayo;
·
Wachezaji wanaopatikana katika kikosi cha sasa
cha Juventus
·
Majeruhi katika timu
·
Uamuzi wa mwalimu kwa namna anvyoiona timu
pinzani
Tukumbuke kuwa Juve wamesajili pia wachezaji
wengine katika idara ya kiungo hivyo kuleta chaguzi ya mifumo kwa mwalimu
Conte.
MATEGEMEO.
Juventus kuendelea kufanya vizuri katika michuano watakayoshiriki msimu ujao wa Ligi kuu ya soka nchini Italia(Serie A),Copa Di Italia pamoja na Klabu bingwa barani Ulaya(UEFA Champions League).
FORZA JUVE
0 comments:
Post a Comment