Akifanya ziara yake kwa mara ya kwanza nchini Urusi
baada ya kipindi cha muda mrefu, hatimaye ziara ya aliyekuwa waziri mkuu na
mmiliki wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi imeonesha kuzaa matunda.Akiwa
Urusi alimtembelea rafiki yake wa muda mrefu Vladimir Putin ambaye ndiye Rais
wa nchi ya Urusi na kufanikiwa kuzungumza naye mambo kadha wa kadha ikiwepo
kuomba uwekezaji wa makampuni na hata matajiri watakaoweza kuwekeza katika
klabu ya AC Milan.
Tetesi zinasema kuwa tayari kampuni ya Gazprom iliyopo
nchini Urusi ambayo inashughulika na uchimbaji wa gesi na mafuta imekubali
kuwekeza katika klabu hiyo kwa kutoa mkwanja wa takribani hela za ulaya (euro
mil 180) kwa kuanzia.Taarifa hizi zimetoka katika chombo kimoja cha habari
nchini Hispania kinachojulikana kama AS ambacho kinataarifu pia serikali ya
Urusi ndiyo wamiliki wa kampuni hiyo ya Gazprom tangu mwaka 1989.
Kampuni ya Gazprom ilianzishwa mwaka 1989 katika
nchi iliyojulikana kama Soviet Union ambayo ilikuja kumeguka na kupatikana nchi ya Urusi.Ni kampuni inayomilikiwa kwa kiasi
kikubwa na serikali ya Urusi kwa 50%.Kampuni hiyo inasadikiwa kuwa ina utajiri
wa dola za kimarekani billion 44.6(US $44.6 bil).
Lakini kwa taaifa yako tu wewe mpenzi wa soka ni
kuwa kampuni hiyo ya Gazprom ndiyo wadhamini wa klabu za Zenith St.Petersburg ya
nchini Urusi pamoja na klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani.
Forza Milan kwa udhamini huo.
0 comments:
Post a Comment