NGAO YA JAMII
NI
MAN CITY DHIDI YA CHELSEA,TUTARAJIE NINI NGAO YA JAMII?
KWA NINI INAITWA NGAO YA JAMII?
Sababu kuu ya kuitwa ngao ya jamii ni
mapato yatokanayo na mechi hii ambayo hugawiwa kwa taasisi za kijamii, mapato
ya getini pamoja na mapato yanayotokana na mauzo ya haki zote za mechi hii
husambazwa kwa vilabu 124 vilivyoshiriki katika kombe la FA kuanzia raundi ya
kwanza na kuendelea kwa dhumuni kubwa la kusambaza katika ‘projects’ au miradi
mbalimbali ya kijamii. Mechi ya kwanza ya ngao hii ilichezwa msimu wa 1908/09 ikiwakutanisha Manchester United kama
bingwa wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Queens Park Rangers kama bingwa wa
Southern league ambapo Man U iliibuka na ushindi wa 4-0 baada ya mechi ya
kwanza kuisha 1-1 ndani ya uwanja wa Stamford Bridge.
Ngao ya jamii, wakati huo ngao ya hisani
ilianza mwaka 1898/99 ikijulikana kama Sherriff of London Charity Shield
ikwakutanisha wanataaluma (Proffessionals) na wasio na taaluma (Amateurs).
Lengo kuu la hili ilikuwa ni kumkaribisha Sheriff mpya wa jiji la London. Mfumo
mpya ulianza mwaka 1908 ukiwakutanisha bingwa wa ligi daraja la kwanza na wa
Southern league (Man U Vs QPR).
Mfumo wa mashindano haya umeendelea
kubadilika siku hadi siku: mwaka 1913 ilikuwa ni baina ya wanataaluma na wasio
na taaluma, mwaka 1921 ilikuwa ni baina ya bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la
FA kwa mara ya kwanza. Mfumo huu uliendelea kubadilika mpaka miaka ya 1920 kwa
Proffessionals na amateurs kukutana lakini mnamo mwaka 1930 mfumo wa bingwa wa
ligi na wa kombe la FA ukarudi tena mpaka leo hii.
![]() |
Add caption |
NINI MVUTO WA MECHI HII BASI
Mechi hii huashiria ufunguzi wa msimu mpya
wa ligi na mashabiki hupata fursa ya kuona wachezaji wapya, jezi pamoja na
mfumo mpya utakaotumiwa na timu zao, hivyo basi wadau wengi wa soka wakiwa
wamekaa takriban miezi mitatu wanapata fursa ya kuangalia timu zao kwenye
mashindano mbalimbali.
VIPI MSIMU HUU?
Kama utakuwa na kumbukumbu Manchester Utd
ndiyo mabingwa watetezi wa ngao hii walioipata kwa kuwalaza wapinzani wao
Manchester city 3-2 mnamo tarehe 7 agasti 2011. Mwaka huu tutapata fursa ya
kushuhudia miamba miwili, Manchester city wakiwa mabingwa wa Ligi kuu ya
Premier(EPL) dhidi ya Chelsea wakiwa mabingwa wa FA na UEFA champions league
jumapili ya tarehe 12 mwezi huu wa nane katika uwanja wa Villa Park, jijini
Birmingham. Manchester city inacheza ikiwa bila kuwa na usajili wowote mkubwa
kama ilivyozoeleka huku wengi
wakiongelea suala la usajili kusinzia akiwamo kocha wao Roberto Manchini,
pamoja na hilo bado kuna wachezaji wa kuogopwa kama Silva, Yaya Toure na Aguero. Kwa upande wa pili mambo ni tofauti
kidogo, naweza kudiriki kusema Chelsea ni timu yenye safu ya kiungo bora kabisa
ligi kuu ikiwaunganisha wachezaji wapya kama Oscar, Marko Marin na Eden Hazard
na wa zamani kama Malouda, Ramires, Lampard, Mikel na Essien. Nadhani utakua
umepata picha ni jinsi gani mechi hii itakuwa na mvuto tofauti na miaka kadhaa
iliyopita.
Mwaka huu wa 2012, Community Shield au ngao
ya jamii itachezwa tofauti na Wembley na Millenium kwa sababu ya viwanja hivyo
kutumika kwa mashindano ya Olympics. Kuna uwezekano mkubwa kwa mechi hii
kupigwa katika viwanja vya Sports Direct Arena (Newcastle), lakini zaidi ni
Villa Park huko Birmingham.
VIKOSI TARAJIO
Man City: Hart, Zabaleta, Clichy, Coates,
Company, Yaya, Barry, Silva, Nasri, Tevez, Aguero
Chelsea: Cech, A.Cole, Luiz, Terry,
Ivanivic, Mikel, Lampard, Marin, Ramires, Hazard, Torres
JE WAJUA?
·
Timu yenye mafanikio zaidi kwa
mashindano haya ni Manchester United ikiwa imechukua mara 15 ikifuatiwa na
Liverpool mara 10, Arsenal 12, Everton 9 na Spurs 7.
·
Mechi ilyotoa magoli mengi ni
kati ya Manchester Utd iliyoifunga Swindon Town 8-4 mwaka 1911.
·
Everton inashikilia rekodi ya
kushinda mfululizo (4) toka mwaka 1984-1987 na Man U inashikilia rekodi ya kuwa
timu iliyocheza mara nyingi mfululizo kuanzia mwaka 1998-2001.
·
Pat Jennings (Spurs) ni kipa wa
kwanza kufunga goli na akiwa katika eneo lake la penati dhidi ya Man U.
·
Leicester city na Brighton ni klabu pekee
zilizochukua ngao hii bila kuwa mabingwa wa aidha ligi au FA cup.
IFUATAYO NI ORODHA YA TIMU ZILIZOFANIKIWA
KUITWAA NGAO HII.
Manchester United 19
Liverpool 15
Arsenal 12
Everton 9
Tottenham Hotspur 7
Chelsea 4
Wolves 4
Manchester City 3
Leeds United 2
Burnley 2
Ni nani ataibuka mbabe mwaka huu?jumapili
ya tarehe 12 mwezi wa nane, Villa Park, Manchester City Vs Chelsea.
0 comments:
Post a Comment