Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, January 31, 2013

POULSEN ATANGAZA KIKOSI CHA STARS DHIDI YA CAMEROON


 



KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.

“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam).

Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Katika kikosi hiki, Poulsen hajamuita Jerry Tegete ambaye siku za karibuni amefufua makali yake wakati ameita washambuliaji halisi wawili tu, Ulimwengu na Samatta.  

Nyota wa timu ya taifa ya Cameroon wanaotarajiwa kuja ni pamoja na:

 Charles Itandje, Mayebi Joslain, Allan Nyom, Benedict Angbwa, Benoît Assou Ekotto, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Armel Kana Biyick, Bouba Aminou, Joel Matip, Alexandre Song, Nguemo Landry, Pierre Wome Nlend, Hervé Tchami, Fabrice Olinga Essono, Achille Emana, Eloundou Charles, Jean Makoun II, Samuel Eto'o Fils, Vincent Aboubakar, Jean Paul Yontcha

Tuesday, January 29, 2013

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA COUTINHO

 New signing: Philippe Coutinho poses with a Liverpool shirt ahead of his move being officially being announced
Hatimaye mchezaji Phillipe Coutinho amejiunga rasmi na klabu ya Liverpool kwa ada ya euro milion nane akitokea klabu ya Inter Milan.

QPR YAIBANA MBAVU MAN CITY

 Farewell: Nelsen makes his way down the guard of honour... and Cesar applauds
Klabu ya QPR iliilazimisha sare ya bila kufungana klabu ya Manchester City kwa kutoka sare ya 0-0.Pambano hilo lililopigwa katika uwanja wa Loftus Road.

LAZIO YAITOA JUVENTUS COPA ITALIA

 Lazio celebrating (Coppa Italia, Getty Images)
Klabu ya soka ya Lazio jana iliweza kutinga fainali ya Copa Italia mara baada ya kuifunga klabu ya Juventus kwa magoli 2-1 katika pambano kali na la kusisimua lililopigwa katika uwanja wa Estadio Olimpico.Magoli ya Lazio yalifungwa na Alvaro Gonzales na Sergio Flocari wakati Arturo Vidal alifunga kwa upande wa Juventus

KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUKUTANA KESHO KUJADILI PINGAMIZI ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI


 
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo imepanga kukutana kwa mara kwanza kesho Jumatano, ili kupitia majina yote na pingamizi zilizowekwa kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za TFF.

Wagombea ambao wamewekewa pingamizi ni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, anayewania nafasi ya Bodi ya Ligi, Michael Wambura, anayetaka nafasi ya Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani anayewania Urais, Jamal Malinzi Urais, sambamba na Mugisha Garibona, Vedastus Lufano wanaowania nafasi ya Ujumbe, huku wakiwekewa pingamizi na Paul Mhangwa.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah, alisema Kamati ya Uchaguzi itapitia pingamizi zote zilizowekwa kwa wagombea hao.

Osiah alisema katika kikao hicho cha kujadili pingamizi kitakachoanza saa nne asubuhi, waombaji wote wa nafasi za uongozi na wale walioweka pingamizi wanatakiwa kufika katika tukio hilo.

“Wale walioweka pingamizi kwa wagombea na wanaowania nafasi za uongozi za TFF wote watashiriki kikao hicho cha kujadili pingamizi,” ilisema taarifa hiyo.

Uchaguzi wa TFF umepangwa kufanyika Februari 24 jijini Dar es Salaam, huku wadau mahiri wa michezo wakipigana vikumbo kuzitaka nafasi mbalimbali za Shirikisho hilo nchini.

Nafasi zote zimekuwa na ushindani wa aina yake, huku majina ya wadau kama vile Malinzi, Nyamlani kwa nafasi ya urais, bila kusahau Manji na Wambura wakipigania ubosi wa TFF katika Uchaguzi wa mwaka 2013.

Monday, January 28, 2013

PIRLO MCHEZAJI BORA ITALIA

Andrea Pirlo

Hatimaye kiungo nyota wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Andrea Pirlo amekumbukwa katika tuzo za wachezaji bora katika Ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Tuzo hizo zinazojulikana kama Gran Gara Del Calcio kutoka kujulikana kama Oscar Del Calcio zilishuhudia kura zaidi ya 600 zikipigwa na watu mbalimbali.

Mtiririko wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo.

Best Goalkeeper: Gianluigi Buffon (Juventus)
Best Right-back: Christian Maggio (Napoli)
Best Centre-backs: Thiago Silva (Milan/PSG) and Andrea Barzagli (Juventus)
Best Left-back: Federico Balzaretti (Roma)
Best Midfielders: Andrea Pirlo (Juventus), Antonio Nocerino (Milan), Claudio Marchisio (Juventus).
Best Forwards: Zlatan Ibrahimovic (Milan/PSG), Edinson Cavani (Napoli), Antonio Di Natale (Udinese).
Best Overall Player: Andrea Pirlo (Juventus)
Best Coach: Antonio Conte (Juventus)
Best Young Players in Serie A: Luis Muriel (Lecce/Udinese) and Stephan El Shaarawy (Milan)
Serie B revelations: Ciro Immobile (Genoa), Lorenzo Insigne (Napoli), Marco Verratti (PSG) – all were with Pescara
Best Club: Juventus
Best Referee: Nicola Rizzoli
Lifetime Achievement Award: Pippo Inzaghi

Sunday, January 27, 2013

JUVENTUS YAKAMILISHA USAJILI WA ANELKA

 
Klabu ya Juventus ya nchini Italia imefanikiwa kumnasa mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua Nicolas Anelka.Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Juventus,Anelak atalipwa mshahara wa kiasi cha fedha €600,000 kwa miezi mitano pamoja na bonasi katika mechi.