Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, January 29, 2013

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA COUTINHO

 New signing: Philippe Coutinho poses with a Liverpool shirt ahead of his move being officially being announced
Hatimaye mchezaji Phillipe Coutinho amejiunga rasmi na klabu ya Liverpool kwa ada ya euro milion nane akitokea klabu ya Inter Milan.

QPR YAIBANA MBAVU MAN CITY

 Farewell: Nelsen makes his way down the guard of honour... and Cesar applauds
Klabu ya QPR iliilazimisha sare ya bila kufungana klabu ya Manchester City kwa kutoka sare ya 0-0.Pambano hilo lililopigwa katika uwanja wa Loftus Road.

LAZIO YAITOA JUVENTUS COPA ITALIA

 Lazio celebrating (Coppa Italia, Getty Images)
Klabu ya soka ya Lazio jana iliweza kutinga fainali ya Copa Italia mara baada ya kuifunga klabu ya Juventus kwa magoli 2-1 katika pambano kali na la kusisimua lililopigwa katika uwanja wa Estadio Olimpico.Magoli ya Lazio yalifungwa na Alvaro Gonzales na Sergio Flocari wakati Arturo Vidal alifunga kwa upande wa Juventus

KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUKUTANA KESHO KUJADILI PINGAMIZI ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI


 
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo imepanga kukutana kwa mara kwanza kesho Jumatano, ili kupitia majina yote na pingamizi zilizowekwa kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za TFF.

Wagombea ambao wamewekewa pingamizi ni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, anayewania nafasi ya Bodi ya Ligi, Michael Wambura, anayetaka nafasi ya Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani anayewania Urais, Jamal Malinzi Urais, sambamba na Mugisha Garibona, Vedastus Lufano wanaowania nafasi ya Ujumbe, huku wakiwekewa pingamizi na Paul Mhangwa.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah, alisema Kamati ya Uchaguzi itapitia pingamizi zote zilizowekwa kwa wagombea hao.

Osiah alisema katika kikao hicho cha kujadili pingamizi kitakachoanza saa nne asubuhi, waombaji wote wa nafasi za uongozi na wale walioweka pingamizi wanatakiwa kufika katika tukio hilo.

“Wale walioweka pingamizi kwa wagombea na wanaowania nafasi za uongozi za TFF wote watashiriki kikao hicho cha kujadili pingamizi,” ilisema taarifa hiyo.

Uchaguzi wa TFF umepangwa kufanyika Februari 24 jijini Dar es Salaam, huku wadau mahiri wa michezo wakipigana vikumbo kuzitaka nafasi mbalimbali za Shirikisho hilo nchini.

Nafasi zote zimekuwa na ushindani wa aina yake, huku majina ya wadau kama vile Malinzi, Nyamlani kwa nafasi ya urais, bila kusahau Manji na Wambura wakipigania ubosi wa TFF katika Uchaguzi wa mwaka 2013.

Monday, January 28, 2013

PIRLO MCHEZAJI BORA ITALIA

Andrea Pirlo

Hatimaye kiungo nyota wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Andrea Pirlo amekumbukwa katika tuzo za wachezaji bora katika Ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Tuzo hizo zinazojulikana kama Gran Gara Del Calcio kutoka kujulikana kama Oscar Del Calcio zilishuhudia kura zaidi ya 600 zikipigwa na watu mbalimbali.

Mtiririko wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo.

Best Goalkeeper: Gianluigi Buffon (Juventus)
Best Right-back: Christian Maggio (Napoli)
Best Centre-backs: Thiago Silva (Milan/PSG) and Andrea Barzagli (Juventus)
Best Left-back: Federico Balzaretti (Roma)
Best Midfielders: Andrea Pirlo (Juventus), Antonio Nocerino (Milan), Claudio Marchisio (Juventus).
Best Forwards: Zlatan Ibrahimovic (Milan/PSG), Edinson Cavani (Napoli), Antonio Di Natale (Udinese).
Best Overall Player: Andrea Pirlo (Juventus)
Best Coach: Antonio Conte (Juventus)
Best Young Players in Serie A: Luis Muriel (Lecce/Udinese) and Stephan El Shaarawy (Milan)
Serie B revelations: Ciro Immobile (Genoa), Lorenzo Insigne (Napoli), Marco Verratti (PSG) – all were with Pescara
Best Club: Juventus
Best Referee: Nicola Rizzoli
Lifetime Achievement Award: Pippo Inzaghi

Sunday, January 27, 2013

JUVENTUS YAKAMILISHA USAJILI WA ANELKA

 
Klabu ya Juventus ya nchini Italia imefanikiwa kumnasa mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua Nicolas Anelka.Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Juventus,Anelak atalipwa mshahara wa kiasi cha fedha €600,000 kwa miezi mitano pamoja na bonasi katika mechi.

Saturday, January 26, 2013

YANGA KUANZA KIBARUA KESHO LIGI KUU VODACOM

 
Young Africans Sports Club Mabingwa wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya mechi itakayoanza majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es saalaam.
 
Mara baada ya kuweka kambi ya takribani wiki mbili katika mji wa Antalya nchini Uturuki kikosi cha Young Africans kimerejea kikiwa na morali ya hali ya juu, wachezaji na benchi la ufundi wakihitaji kushinda kila mchezo unaowakabli ili kujiweka katika hali nzuri ya kutwaa Ubingwa wa Vodacom.
 
Katik micheoz miwili ya kujipima nguvu  kabla ya kuanza kwa duru la pili la ligi kuu Young Africans ilishinda michezo yote, mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini kabla ya kushinda tena 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo ya Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika jijini Mwaza. 
 
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa kuwa na alama 29 alama tano zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 24, huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 25 na kufungwa mabao 10 tu katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom
 
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa katika dimba la uwanja wa Sokoine jijini Mbeya timu zilitoka sare ya bila kufungana mchezo ambao pia ulikuwa ni wa waufunguzi  katika araundi ya kwanza.
 
Kocha Mkuu Ernest Brandts amesema kikosi chake kimekamilika, kiakili, kiafya na kimorali hivyo anaamini vijana wake wataibuka na ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Prisons kutoka Mbeya.
 
Kikosi cha wachezaji 27 leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika uwnja wa mabatini kijitonyama huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri ya kimchezo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja. 
 
Timu imeingia kambini leo asubuhi katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani.