Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, January 2, 2013

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAI DANIEL STURRIDGE

 Daniel Sturridge
Majogoo wa jiji klabu ya Liverpool hatimaye imekamilisha usajili wa nyota wa zamani wa vilabu vya Chelsea,Bolton Wanderers na Manchester City Daniel Sturridge.Liverpool wametumia kiasi cha pauni za Uingereza 12milioni kumleta mchezaji huyo kutoka klabu ya Chelsea ambaye amecheza mechi moja tu tangu msimu huu uanze akiwa na labu ya Chelsea.Akizungumzia usajili wake,Danny anasema "nimesaini kuichezea klabu hii muda mrefu ili nipate nafasi ya kucheza mara kwa mara.Nipo katika klabu bora yenye wachezaji wa kiwango cha dunia na yenye mashabiki bora ulimwenguni.

Danniel Sturridge amezaliwa katika jiji la Birmigham nchini England na alianza maisha yake ya soka katika kituo cha kulea vijana kisoka cha Aston Villa amekabidhiwa jezi namba 15 katika klabu yake mpya ya Liverpool.

A.C MILAN ITARUDI TENA



Mnamo tarehe 16 Desemba 1899, Klabu ya A.C Milan ilianzishwa na raia wawili wa Uingereza Herbert Kilpin na Alfred Edwards ikihusisha mIchezo ya “football na cricket” Kutokana na mvutano uliosababishwa na sera ya usajili wa wachezaji wa kigeni mwaka 1908 iligawanyika na kuundwa klabu nyigine ya Inter Milan.
Katika kipindi cha nyuma ikiwa na wachezaji mahiri kama Franco Beresi, Paolo Maldini,Van Basten ,Inzaghi klabu ya AC Milan iliweza kushinda mataji mbalimbali kama UEFA Champions league, UEFA Super cup na mengineyo.Katika miaka ya karibuni A.C Milan imeshindwa kufanya vizuri katika michuano mbalimbali kitu ambacho kimechangiwa na vitu mbalimbali.
Kutowekeza katika soka la vijana,hili si tatizo kwa  Milan pekee bali vilabu vingi nchini italia.Vikosi vya vilabu hivi vimekuwa vikiundwa na wachezaji wenye umri mkubwa ,mfano katika kikosi kilichoanza na kutwaa ubingwa wa ulaya dhidi ya Liverpool mwaka 2007 ni wachezaji watatu tu ambao walikuwa chini ya miaka 30, Andrea Pirlo(27),Riccardo Kaka(25) na Gattuso(27) wachezaji wengine walikuwa wamevuka umri huo kama Maldini (39), Inzaghi (34) , Seedorf (31), Oddo (31) , Ambrosin (30) na Nesta (31)
Kuondoka kwa wakongwe ,mwanzoni mwa msimu huu 2012-2013 tumeshuhudia wakongwe kama Inzaghi, Nesta,Seedorf, Gattuso na Gianluca Zambrotta  wakiondoka.Hii imepelekea mabadiliko mengi katika safu mbalimbali hivyo itachukua muda kwa vijana waliopo kuunda kombinesheni bora kama ile ya Wa-Sweden Gunnar Gren, Gunnar Nordahl na  Nils Liedholm  miaka ya 1950 ama Ruud Gullit, Frank Rijkaard na Van Basten miaka ya 1980 kuondoka kwa wakongwe kumetoa nafasi kwa vijana kama Abate, El –Shaarawy, De-Sciglio , Acerbi na wengine.
Ukata wa fedha pia umepelekea Milan kuuza wachezaji wake nyota kam Zlatan Ibrahimovic na  Thiago Silva ambao wamejiunga na P.S.G.Hali hii imesababisha Milan kushindwa kununua wachezaji nyota kuziba nafasi  hizo, hivyo kuwa na safu mbovu ya mabeki wa kati huku katika ushambuliaji ikimtegemea zaidi Stephan El-Shaarawy.
Kushindwa kurudisha wachezaji nyota ambao Milan iliwatoa kwa mkopo kama vile Yoann Gourcuff aliyekuwa Girondins Bordeaux na baadae aliuzwa moja kwa moja .Wengi tuliamini kuwa angekuwa mbadala wa Ricardo Kaka aliyehamia Real Madrid.Pia makinda wengine kama Alexandre Merkel  aliyeko Genoa na Albert Paloschi (Chievo) nako kumeifanya klabu ya Milan iendelee na utamaduni wa kupoteza nyota wake wanaofanya vyema katika vilabu vingine(kwa mkopo) katika Serie A.
Katika kambi ya mazoezi Milanello vijana ndio wametawala hii inashiria kwamba klabu imedhamiria kuwekeza katika vijana hivyo tutarajie mafanikio siku zijazo.Klabu kama F.C Barcelona imepata mafanikio kutokana na kuwekeza katika soka la vijana hivyo kupata mafanikio kutokana na wachezaji  mazao ya academy zao.Kutoa nafasi kwa kina El-Shaarawy ,De sciglio, Acerb, Niang , Ganz na Bojan kutasaidia kuunda timu bora ya kiushindani. Hivyo naamini siku moja Milan itarudia makali yake.
Milan itarudi.
KEEP CALM & SUPPORT AC MILAN
Forza Milan
ANTONY MALIGANYA

INTER MILAN WAMNYEMELEA LAMPARD

 
Klabu ya soka ya Inter Milan ya nchini Italia nayo imeingia katika vita ya kupata sahihi ya kiungo wa timu ya soka ya Chelsea Frank Lampard Jr.Kiungo huyo ambaye hatma yake haijulikani mpaka sasa kunako klabu hiyo ya Chelsea ya nchini England anatakiwa na vilabu vingi katika bara la Ulaya na Amerika(Marekani).Lampard mwenye miaka 34 anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya darajani (Chelsea) endapo hatahakikishiwa mkataba mpya utakaomfanya aendelee kuwepo klabuni hapo.

Mkataba wa Lampard unaisha mwezi wa sita mwaka huu na hivyo kumfanya kuwa mchezaji huru pindi dirisha kubwa litakapofunguliwa mnamo mwezi wa saba mwaka huu.Lampard ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2001 anatakiwa pia na vilabu vya Lazio,LA Galaxy na PSG.Hii ni mara ya pili kwa klabu ya Inter Milan kumtaka kiungo Frank Lampard Jr kwani wamekwisha mtaka pia mwaka 2009 wakati Jose Mourinho akiwa kocha wa Inter milan.

Tuesday, January 1, 2013

ARSENAL YALAZIMISHWA SARE NA SOUTHAMPTON


Klabu ya AWelcome back: Alex Oxlade-Chamberlain (left) returned to his former club with Arsenal rsenal imelazimishwa sare na klabu ya Southampton katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya so soka nchni England.Pambano hilo lililopigwa katika uwanja wa St.Marys lilishuhudia timu hizo zikigawana pointi moja moja mara baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1.Southampton walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa kiungo wao Gaston Ramirez kabla ya mchezaji Guly Do Prado kujifunga mwenyewe kwa upande wa Southampton.Mpaka mwisho wa mchezo Southampton 1-1 Arsenal.

POULSEN ATANGAZA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOIVAA MOROCCO




WACHEZAJI 22 wameteuliwa na kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen kwa ajili ya kuingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kujiandaa na mechi za kirafiki dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

MAN CITY YAIFUNGA STOKE CITY KATIKA EPL

 Season's greetings: Dzeko was booked after showing a message which read 'HAPPY NEW YEAR'
Klabu ya Man City imeendelea kuwafukuzia vinara wa Ligi hiyo Man United katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya soka nchini England baada ya kuwafunga Stoke City kwa magoli 3-0.Magoli ya Man City yalifungwa na beki Pablo Zabaleta na washambuliaji Edin Dzeko pamoja na Sergio Kun Aguero kwa mkwaju wa penati mara baada ya kiungo David Silva kuangushwa katika eneo la penati.

CHICHARITO NA VAN PERSIE WAZIDI KUING'ARISHA MAN UNITED

 Going Dutch: Robin van Persie was central to everything good in United's play, and scored the second
Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea tena kwa mechi mbalimbali kupigwa katika viwanja mbalimbali huku macho ya wapenda kabumbu yakiwa zaidi katika viwanja vya DW uwanja unaomilikiwa na klabu ya Wigan pamoja na pale Etihad Stadium kunako jiji la Manchester.
Pounced: Hernandez was on hand to stroke in the opener midway the first half at the DW
Katika uwanja wa DW klabu ya Wigan iliikaribisha masheatani wekundu Man United.Katika pambano hilo kulikuwa na mandhari nzuri kwa kocha wa Man United Sir Alex Ferguson ambaye jana tarehe 31/12/2012 alitimiza umri wa miaka 71.Hongera sana kwa siku ya kuzaliwa Sir Alex Ferguson.Katika mechi hiyo Man United iliibuka na ushindi wa magoli 4-0 huku shukrani ziwaendee washambuliaji wa Man United Javier Hernandes 'Chicharito' aliyefunga magoli 2 na Robin Van Persie kufunga magoli 2 pia.