Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Sunday, September 2, 2012

UDINESE CALCIO













Udinese na msimu mpya wa Serie A 2012-13



Mpaka sasa mashabiki wa klabu ya soka ya Udinese ya nchini Italia  au waweza kuwaita Pundamilia wadogo(Zebrette) au Bianconerri(nyeupe na nyeusi) kutokana na jezi zao kuwa na rangi nyeusi na nyeupe  hawaamini kama timu yao imeweza kumaliza katika nafasi za juu za ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama serie A na pia kupata nafasi ya kushiriki hatua za awali za michuano ya klabu bingwa barani ulaya maarufu kama(UEFA Champions League) kwa msimu wa mwaka 2012-13.
Wakishika nafasi ya tatu nyuma ya vilabu vikongwe Italia  vikiongozwa na bingwa Juventus pamoja na makamu bingwa AC Milan,Udinese waliendelea kuwashangaza wapenda kabungu wengi ulimwenguni pamoja na mashabiki wake kwani pamoja na timu hiyo kuwa na historia ya kuondokewa na nyota wake mara kwa mara kwa kujiunga na vilabu vikubwa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimeifanya klabu ya Udinese kuwa kama chimbo au soko la kununua nyota wanaowika katika klabu hiyo ya Friuli-Venezia nchini Italia,Udinese walivishinda vilabu kama Inter Milan,Lazio,AS Roma na Napoli katika mbio za kuwania nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa ulaya msimu wa 2012-13.
Hakuna asiyejua kuwa klabu ya Udinese imewatoa nyota  wengi mno ambao waling’aa sana wakiwa na klau hiyo.Wachezaji wengi bora kama  Nestor Sensini, Oliver Bierhoff, Marcio Amoroso, Vincenzo Iaquinta, David Pizarro, Martin Jørgensen na bila kuwasahau Sulley Muntari, Fabio Quagliarella, Antonio Di Natale, Felipe, Cristián Zapata, Simon Pepe,Gökhan Inler, Alexis Sánchez na wengine wengi wakipitia klabu hii na kuifanya kuwa moja kati ya vilabu vikubwa na vyenye nguvu nchini Italia.
Msimu uliopita ulikuwa wa kampeni nzito kwa kocha Francesco Guidollin na timu yake ya Udinese Calcio mana ulihusisha ushindani toka kwa vilabu vikubwa kwa maana kama Juventus,Inter Milan,Napoli,Roma bila kusahau vilabu vingine shiriki katika  serie A kama Genoa,Chievo,Atalanta,Parma,Siena na vilabu vyote shiriki katika serie A msimu uliopita 2012.
Lakini walikuwa ni pundamilia hao wadogo ambapo ilibaki kidogo tu nao waandike historia ya kuutwaa ubingwa wa serie A msimu uliopita kama kusingekuwa na umakini kwa vilabu vya Juventus na AC Milan.
Msimu huu tena kama ilivyoada tutawakosa baadhi ya nyota kunako klabu hiyo kwani familia ya Pozzo ambayo ndiyo wamiliki wa klabu hiyo wameendelea na utaratibu wao wa kuuza nyota na kuingiza nyota wapya katika klabu hiyo.Nyota kama  Kwadwo Asamoah,Mauricio Isla,Antonio Floro Flores,Gabriel Toje na Damiano Ferronetti pamoja na Samir Handanovic hawataonekana katika viwanja vya Friuli kutokana na kuuzwa katika vilabu vya Juve,Inter na wengine mikataba yao kuisha au kupelekwa kwa mkopo katika vilabu vingine kama Granada.
Pia kukiwa na tetesi za kuondoka kwa baadhi ya nyota kama Pablo Armero na Danilo,klabu ya Udinese kwa mshangao wa wengi haionekani kutetereka na ndiyo kwanza maisha ndani ya Friuri-Venezia Giulia  yakiendelea kama kawaida.
Embu tuiangalie Udinese kiufundi,Je kuondoka kwa nyota kama Handanovic,Kwadwo Asamoah na Isla kunaweza kuigharimu Udinese msimu huu wa 2012-13?tuanze na nafasi ya golikipa
Nafasi ya Golikipa.
Hakuna shaka kuwa Samir Handanovic ni mmoja wa makipa bora sana kwa sasa barani ulaya. Na nawapongeza Inter Milan kwa kumchukua golikipa huyu kwani ataongeza ‘clean sheet’au uimara katika sehemu ya  ulinzi wa Inter Milan msimu ujao.Kuondoka kwake Udinese kunatoa nafasi ya kurudi kwa kipa  Zelijko Brkic aliyekuwa kwa mkopo kunako klabu ya Siena.Brkic alikuwa na msimu mzuri sana pale Siena kwani aliweza kuiongoza vyema ngome ya Siena ikiwa na mabeki Roberto Vitiello, Cristiano Del Groso na Claudio Terzi.Hivyo kurudi kwa Brkic kunaondoa mashaka kidogo kwa nafasi ya golikipa katika klabu ya Udinese.
Nafasi ya ulinzi (mabeki wa kati na pembeni).
Kwa bahati nzuri sehemu hii nyeti haijaguswa kabisa.Tumeshuhudia kuondoka kwa Asamoah,Isla na wengineo ambao wanacheza katika nafasi za viungo na ushambuliaji lakini si kwa nafasi ya ulinzi ambayo ilifanya vizuri sana msimu uliopita na kuna kila dalili safu ya ulinzi ya Udinese ya msimu uliopita ikawepo tena msimu huu.Hapa nawazungumzia Mehdi Benatia,Danilo na Maurizo Domizzi ambao naamini watakuwepo katika klabu hiyo msimu ujao.Mabeki hao watasaidiwa naAndrea Coda,Joel Ekstrand mchezaji mpya Thomas Hertaux ambaye ametokea klabu ya Caen ya nchini Ufaransa.Hivyo kwa kiasi kikubwa sehemu ya ulinzi ya Udinese inaonekana kuwa na usalama mkubwa.
 

Nafasi ya mabeki wa pembeni (ambao hucheza kama ma ‘wing backs’).
Sehemu hii ilikuwa na umuhimu mkubwa sana katika mtindo au staili ya uchezaji ya klabu ya Udinese.Ikiongozwa na mserbia Dusan Basta pamoja na Pablo Armero hakika Udinese walikuwa hatari sana msimu uliopita.Kama Armero hataondoka, basi Udinese watatisha sana wakiendelea kuwa na hawa ma ‘wing backs’Basta na Armero,Sehemu hii imeongezewa nguvu na ujio wa Marco Faraoni toka klabu ya Inter Milan na mfaransa Jean Alain Fanchome bila kumshau Giovanni Pasquale ambaye alikuwa na msimu bora kabisa wa serie A wa mwaka jana.
Nafasi ya kiungo.                                                                                                
Hakuna mpenda kabumbu asiyejua unyeti wa idara hii kwani ndiyo inayotufanya wapenzi wengi wa soka kupenda kuangalia mpira.Hapa ndipo tuliwaona na tunaendelea kuwaona kina Zidane,Vieira,Wilshere,Redondo,Effenberg,Pirlo,Iniesta,Scholes,Xavi nk.Uwepo wa kiungo mpambanaji Giampiero Pinzi na kuja kwa kiungo mchapakazi mwingine Willians maarufu kama(Pitbull) utazidi kuimarisha klabu ya Udinese hasa katika sehemu ya kiungo.Ni nafasi pia kwa mwafrika Emanuel Badu kuweza kung’aa  pamoja na chipukizi wengine kama Robert Pereyra na Christian Battochio kuweza kufanya vizuri kwa msimu unaokuja wa ligi.
Trequartista au unaweza kumwita mshambuliaji wa pili.
Ni eneo la kujidai ambalo vijana wengi wa mjini wanapenda kuliita ‘shimoni’ ambalo kwa kiasi kikuubwa ndilo tumepata kuwashuhudia wachezaji kama Del Piero,Baggio,Totti na sasa tunamshuhudia Cassano.Pia wachezaji kama Messi,Thomas Muller wakijidai mno katika sehemu hiyo maarufu kama Trequartista.Ni eneo ambalo walipata nalo shida mno Udinese msimu uliopita kwani hakupatikana mtu sahihi katika eneo hili ambaye angekuwa akicheza sambamba na mshambuliaji Antonio Di Natale.
Lakini kwa msimu huu mpya wa ligi, mchezaji Diego Fabbrini ameonekana kufiti vizuri sana katika eneo hilo hasa katika mechi za maandalizi ya msimu mpya unaokuja (pre-season).Uwepo wa Fabbrini na ujio wa nyota mpya Mbrazili Maicosuel toka klabu ya Hoffenheim(Ujerumani) utaongeza nguvu katika eneo hilo na sehemu ya ushambuliaji kwa ujumla.





Nafasi ya ushambuliaji (Forwards)
Hakuna shaka kuwa Antonio Di Natale anabaki kuwa legendary kunako klabu hiyo ya Friuri pamoja na serie A kwa ujumla.Atakuwa akiangaliwa kwa kiasi kikubwa katika ushambuliaji.Nguvu imeongezeka katika sehemu hiyo ya ushambuliaji baada ya kuwasili kwa mchezaji anayekuja juu kwa sasa Luis Muriel akitokea kwa mkopo kunako klabu ya Lecce. Uwepo wa Di Natale na Muriel pamoja na viungo washambuliaji kama Maicosuel utaiongezea nguvu klabu ya Udinese katika ushambuliaji na hivyo kukifanya kikosi cha kocha Francesco Guidolin kutikisa msimu ujao.

 

 

 

 

 

 

 

NI GIAMPAOLO PAZZIN AC MILAN

Ilikuwa shangwe pale Stadio Renato Dall'Ara ambapo vijana ya Rosoneri AC Milan waliwapigisha kwata vijana wa Bologna kwa kuwafunga magoli 3-1.Pambao hilo liliokuwa kali na la kusisimua lilimshuhudia mshambuliaji mpya wa timu ya AC Milan Giampaolo Pazzin akifunga magoli matatu peke yake maarufu kama hat-trick.

Katika pambano hilo kiungo mpya wa timu ya AC Milan Nigel De Jong alicheza kwa mara ya kwanza katika timu hiyo akiingia kipindi cha pili.
Matokeo mengine ni:
Pale Stadio Olimpico Di Torino vijana wa Torino waliifunga timu ya Pescara magoli 3-0.Magoli ya Torino yalifungwa na Alessandro Sgrigna dk 34,Matheo Brighi dk 58 na Rolando Bianchi dk 62.

Giampaolo Pazzini - Milan
Pazzin

CHELSEA KUMTWAA FALCAO JANUARY


Target: Chelsea are interested in bringing Radamel Falcao in
Klabu ya Chelsea inaweza kufanya kufuru kwa kumsajiri mshambuliaji wa Atletico Madrid Radamel Falcao katika kipindi cha dirisha dogo la usajiri january.Dili hilo litasimamiwa na wakala maarufu Jorge Mendes ambaye ndiye wakala wa mchezaji huyo Radamel Falcao.Roman Abrahamovich anataka kila kitu kimalizwe mapema ili Falcao aweze kutua darajani kwa kwa pauni milion 48 ingawa Atletico De Madrid wanataka zaidi ya hiyo hela kwani katika mkataba wake Radamel Falcao anatakiwa kuuzwa si chini ya pauni milioni 60.Swali je ujio wa Falcao na uwepo wa Fernando Torres utaifanya Chelsea iwe tishio katika EPL nchini Uingereza??toa maoni yako katika hilo.
Daddy: Michael Essien with Jose Mourinho
Baba na mwana-Essien na kocha wake mpya Jose Mourinho

MAN CITY WAIFUNGA QPR KATIKA EPL

Klabu ya Manchester City imeifunga timu ya QPR magoli 3-1.Magoli ya Man City yalifungwa na Yaya Toue dk 16,Edin Dzeko dk 61 na Carlos Tevez likiwa goli lake la tatu katika ligi hiyo msimu huu dk ya 90+3.Goli la QPR lilifungwa na Boby Zamora dk 59.

Going ahead: Manchester City's Yaya Toure scored for City in the first half



Man City: Hart, Zabaleta (Toure 74), Kompany, Lescott, Kolarov, Silva (Milner 81), Toure, Rodwell, Nasri (Razak 89), Tevez, Dzeko.
Subs Not Used: Pantilimon, Sinclair, Clichy, Balotelli.

Booked: Kolarov, Rodwell.
Goals: Toure 16, Dzeko 61, Tevez 90.
QPR: Green, Bosingwa, Ferdinand (Onuoha 67), Nelsen, Da Silva, Wright-Phillips, Granero (Cisse 85), Park, Faurlin (Dyer 72), Zamora, Johnson.
Subs Not Used: Murphy, Derry, Mackie, Hoilett.
Booked: Zamora.
Goals: Zamora 59.
Referee: Chris Foy

Matukio mengine ya EPL katika picha.


Starting well: Mousa Dembele scores for Tottenham on his debut


Argy bargy: Yacob vies for the ball with Nikica Jelavic


Making an impact: Michu (third right) outjumps the Sunderland defence to nod home the equlaiser


Flying start: Kevin Nolan rattled in West Ham's opener with just under a minute on the clock

Saturday, September 1, 2012

DORTMUND WABANWA KATIKA BUNDESLIGA

Alikuwa ni Jakob Blaszczykowski'au anajulikana pia kwa jina la KUBA ambaye aliwaokoa Borrusia Dortmund katika mwendelezo wa Bundesliga.Katika mechi hiyo Dortmund walilazimishwa sare ya goli 1-1 na klabu ya Nurnberg.Goli la Nurnberg lilifungwa na Tomas Pekhart.
Matokeo mengine ni kama yafuatavyo:

KUTOKA UPTON PARK:WEST HAM DHIDI YA FULHAM

Dk ni ya 20 katika uwanja wa Upton Park na tayari klabu ya West Ham inaongoza kwa goli 1 dhidi ya Fulham.Goli la West Ham limefungwa na Kevin Noran Dk ya 1.
DK ya 29.West Ham wanapata goli la 2 likifungwa na Reid
DK ya 41.West Ham wanapata goli la 3 likifungwa na Martin Taylo
FULL TIME WEST HAM 3-FULHAM 0
Local duel: West Ham host Fulham in a London derby to open the weekend's Premier League action
Kevin Nolan vs Damian Duff

"NO FALCAO NO PARTY"

Klabu ya Atletico De Madrid ilitangazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la UEFA Supercup baada ya kuifunga timu ya Chelsea katika pambano lililopigwa uwanja wa Estadio Louis 11 katika jiji la Monaco.Shujaa wa pambano hilo alikuwa ni Radamel Falcao ambaye aliondoka na mpira mara baada ya kufunga magoli matatu mguuni kwa maana ya Hat-Trick.Pambano hilo lilikuwa ni kiashiria cha kufunguliwa kwa pazia la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Europa Ligi ambayo kwa pamoja itaanza mwezi huu wa tisa kuanzia tarehe 18-2012.Ilikuwa ni hat-trick ya 2 kwa Falcao ndani ya siku 5.Falcao aliweka rekodi yake nyingine ya  kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick tangu miaka 35 ipite ambapo mchezaji wa Liverpool Terry Mc Dermot afanye hivyo mwaka 1977 wakati Liverpool wakiwafunga Hamburg magoli 6-0 katika Super Cup nyingine iliyofanyika mwaka 1977.
http://news.bbcimg.co.uk/media/images/62614000/jpg/_62614156_falcao_getty.jpg