
Saturday, September 1, 2012
"NO FALCAO NO PARTY"
Posted on 12:25 AM by Unknown
Klabu ya Atletico De Madrid ilitangazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la UEFA Supercup baada ya kuifunga timu ya Chelsea katika pambano lililopigwa uwanja wa Estadio Louis 11 katika jiji la Monaco.Shujaa wa pambano hilo alikuwa ni Radamel Falcao ambaye aliondoka na mpira mara baada ya kufunga magoli matatu mguuni kwa maana ya Hat-Trick.Pambano hilo lilikuwa ni kiashiria cha kufunguliwa kwa pazia la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Europa Ligi ambayo kwa pamoja itaanza mwezi huu wa tisa kuanzia tarehe 18-2012.Ilikuwa ni hat-trick ya 2 kwa Falcao ndani ya siku 5.Falcao aliweka rekodi yake nyingine ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick tangu miaka 35 ipite ambapo mchezaji wa Liverpool Terry Mc Dermot afanye hivyo mwaka 1977 wakati Liverpool wakiwafunga Hamburg magoli 6-0 katika Super Cup nyingine iliyofanyika mwaka 1977.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment