Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, January 22, 2013

YANGA YAWASILI MWANZA KUCHEZA NA LEOPARDSS

 
Timu Young Africans Sports Club tayari imewasili salama jijini Mwanza asubuhi ya leo tayari kabisa kwa mchezo wake wa kirafiki hapo kesho dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini mchezo utakaochezwa katika dimba la Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10 jioni.
Msafara wa watu 37, wachezaji 27 na viongozi 10 uliwasili majira ya saa 2 kamili asubuhi kwa shirika la ndge la Fast Jet ambapo leo jioni timu inatarajiwa kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Young Africans inacheza mchezo huo wa marudiano dhidi ya timu ya Black Leopard ikiwa ni mchezo wa pili wa kirafiki wa kujipima uwezo kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwishoni wa wiki,Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Black Leopard huku mabao yake yakifungwa na Jerson Tegete mawili na Frank Domayo.

Black Leopard amabyo inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya PSL nchini Afrika Kusini iliomba kupata mchezo mwingine wa kirafiki ambapo kampuni ya Prime Time Promotions walioandaa ziara ya timu hii walikubaliana na Yanga mchezo huu ufanyike jijini Mwanza ili kutoa fursa kwa wakazi wa kanda ya ziwa kuweza kupata burudani ya soka kutoka kwa timu hizi mbili.
Viiongillio vya mnchezo ni Tsh 10,000/= kwa Jukwaa Kuu na Tsh 3,500/= kwa mzunguko.

Sunday, January 20, 2013

SNEIDJER AJIUNGA NA GALATASARAY


 

Hatimaye kiungo nyota kunako klabu ya Inter Milan Wesley Sneidjer amejiunga rasmi na klabu ya Galatasaray kwa mkataba wa miaka mitatu mara baada ya kufuzu vipimo katika klabu hiyo.Akizungumza katika mtandao wa klabu hiyo Sneidjer alisema"nafuraha kujiunga na klabu hii na sitosubiri kuvaa jezi za timu hii ya Galatasaray".Sneidjer alikuwa katika wakati mgumu katika timu ya Inter Milan mara baada ya kukataa kukatwa mshahara wake kama wa euro milioni 6 kwa mwaka.

Friday, January 18, 2013

KAKA KUELEKEA AC MILAN






Klabu ya AC Milan ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mkopo wa kiungo mshambuliaji Ricardo Kaka.Mchezaji huyo aliye katika wakati mgumu katika klabu ya Real Madrid atajiunga kwa mkopo wa miaka miwili mpaka mwezi juni mwaka 2015.Katika mkataba wa sasa wa Kaka mpaka mwishoni mwa msimu huu,Kaka atakuwa akipokea kiasi cha euro milioni 3 ila kwa msimu ujao atapokea kiasi cha euro milioni 6 kwa mwaka.Tayari kocha Massimiliano Allegri ameshapewa baraka zote na viongozi wa Milan katika kukamilisha usajili huo.

UNAZIBAJE PENGO LA CHIELLINI?


 
Pazia la usajili lilifunguliwa rasmi mano tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2013 huku kukiwa na heka heka za mabosi wa vilabu mbalimbali kupaa angani kutafuta wachezaji tofauti tofauti wakiongozwa na maskauti wao(waska vipaji).Katika Serie A,vilabu vimekuwa katika harakati hizo za usajili huku macho yakiwa sana kwa bingwa mtetezi klabu ya Juventus ambayo kwa hali iliyopo ya kikosi chake inawalazimu kuingia sokoni kutafuta baadhi ya wachezaji watakaoziba mashimo katika baadhi ya idara katika timu hiyo.

Sehemu kubwa inayoangaliwa zaidi ni idara ya ushambuliaji ambayo kwa kiasi kikubwa imekosa mshambuliaji mwenye uchu wa mabao ambaye anuwezo wa kufunga magoli 25 na zaidi kwa msimu.

Kocha Antoni Conte ameendelea na uchunguzi wake wa nani anaweza kujiunga na kikosi cha Bianconeri katika dirisha hili dogo la usajili huku macho yakienda zaidi kwa washambuliaji Fernando Llorente na Didier Drogba.Hapo kabla mshambuliaji Robin Van Persie alikuwa akitajwa sana lakini aliishia katika klabu ya Manchester United.Kwa sasa mshambuliaji David Villa naye amekuwa akitajwa kujiunga na miamba hiyo ya Turin.

Wachambuzi wa mambo,mashabikipamoja na wadau mbalimbali wanaweza wasiweke akili zao sana katika sehemu ya ushambuliaji bali macho yao yakaelekea zaidi katika eneo la ulinzi ambapo taarifa mbaya zilizotoka wiki chache zilizopita zilisema kuwa beki wa kutumainiwa wa kati wa klabu hiyo ya Juventus Giorgio Chiellin atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.Ni taarifa zilizowashtua wengi sana hasa benchi la ufundi la klabu hiyo pamoja na viongozi wa klabu na pia mashabiki.

Kuumia kwa mchezaji huyo mwenye umri wa mika 28 kumekuja wakati mmbaya ambapo klabu ya Juventus imeonekana dhairi kupwaya katika idara ya ulinzi na hivi karibuni kuwa na matokeo ya kushangaza kwa kufungwa nyumbani na klabu ya Sampdoria katika Serie A pale Juvents Arena pamoja na sare ya kufungana na klabu ya Parma katika uwanja wa Ernio Tardini.Pamoja na kuwa na mabeki wengine kama Andrea Balzagri,Leonardo Bonucci,,Martin Caceres na usajili mpya wa mkopo wa nyota Federico Peluso toka klabu ya Atalanta Bergamo bado Juventus wanaonekana kumkosa mno Giorgio Chiellini.

Uwepo wa akina Bonucci,Balzagri,Peluso pamoja na kinda Luca Marrone kunaweza kuipunguzia makali klabu hiyo lakini kuna haja ya klabu ya Juentus kuliangalia kwa umakini kabisa eneo la ulinzi kama sehemu nyeti ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu.Hakuna shaka kuwa Juve wanakosa kiongozi katika sehemu ya ulinzi kwani Giorgio ni kiongozi wa mfano na ni mchezaji anayejitoa kwa nguvu zake zote katika kuhakikisha kuwa anaipa ushindi klabu ya Juventus.

Ukiacha michuano ya Serie A,Juventus wana michuano mingine kama Klabu Bingwa Ulaya(UEFA Champions League) na kombe la chama cha soka nchini Italia maarufu kama Copa Di Italia.Hivyo kutokuwepo kwa Chiellini kunaweza kukawathiri Juventus katika michuano hiyo.

Natumai viongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi watafanya maamuzi mazuri wakati huu wa dirisha dogo la usajili likielekea ukingoni katika kuangalia namna ya kuziba pengo la Giorgio Chiellini.