Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Friday, January 18, 2013

UNAZIBAJE PENGO LA CHIELLINI?


 
Pazia la usajili lilifunguliwa rasmi mano tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2013 huku kukiwa na heka heka za mabosi wa vilabu mbalimbali kupaa angani kutafuta wachezaji tofauti tofauti wakiongozwa na maskauti wao(waska vipaji).Katika Serie A,vilabu vimekuwa katika harakati hizo za usajili huku macho yakiwa sana kwa bingwa mtetezi klabu ya Juventus ambayo kwa hali iliyopo ya kikosi chake inawalazimu kuingia sokoni kutafuta baadhi ya wachezaji watakaoziba mashimo katika baadhi ya idara katika timu hiyo.

Sehemu kubwa inayoangaliwa zaidi ni idara ya ushambuliaji ambayo kwa kiasi kikubwa imekosa mshambuliaji mwenye uchu wa mabao ambaye anuwezo wa kufunga magoli 25 na zaidi kwa msimu.

Kocha Antoni Conte ameendelea na uchunguzi wake wa nani anaweza kujiunga na kikosi cha Bianconeri katika dirisha hili dogo la usajili huku macho yakienda zaidi kwa washambuliaji Fernando Llorente na Didier Drogba.Hapo kabla mshambuliaji Robin Van Persie alikuwa akitajwa sana lakini aliishia katika klabu ya Manchester United.Kwa sasa mshambuliaji David Villa naye amekuwa akitajwa kujiunga na miamba hiyo ya Turin.

Wachambuzi wa mambo,mashabikipamoja na wadau mbalimbali wanaweza wasiweke akili zao sana katika sehemu ya ushambuliaji bali macho yao yakaelekea zaidi katika eneo la ulinzi ambapo taarifa mbaya zilizotoka wiki chache zilizopita zilisema kuwa beki wa kutumainiwa wa kati wa klabu hiyo ya Juventus Giorgio Chiellin atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.Ni taarifa zilizowashtua wengi sana hasa benchi la ufundi la klabu hiyo pamoja na viongozi wa klabu na pia mashabiki.

Kuumia kwa mchezaji huyo mwenye umri wa mika 28 kumekuja wakati mmbaya ambapo klabu ya Juventus imeonekana dhairi kupwaya katika idara ya ulinzi na hivi karibuni kuwa na matokeo ya kushangaza kwa kufungwa nyumbani na klabu ya Sampdoria katika Serie A pale Juvents Arena pamoja na sare ya kufungana na klabu ya Parma katika uwanja wa Ernio Tardini.Pamoja na kuwa na mabeki wengine kama Andrea Balzagri,Leonardo Bonucci,,Martin Caceres na usajili mpya wa mkopo wa nyota Federico Peluso toka klabu ya Atalanta Bergamo bado Juventus wanaonekana kumkosa mno Giorgio Chiellini.

Uwepo wa akina Bonucci,Balzagri,Peluso pamoja na kinda Luca Marrone kunaweza kuipunguzia makali klabu hiyo lakini kuna haja ya klabu ya Juentus kuliangalia kwa umakini kabisa eneo la ulinzi kama sehemu nyeti ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu.Hakuna shaka kuwa Juve wanakosa kiongozi katika sehemu ya ulinzi kwani Giorgio ni kiongozi wa mfano na ni mchezaji anayejitoa kwa nguvu zake zote katika kuhakikisha kuwa anaipa ushindi klabu ya Juventus.

Ukiacha michuano ya Serie A,Juventus wana michuano mingine kama Klabu Bingwa Ulaya(UEFA Champions League) na kombe la chama cha soka nchini Italia maarufu kama Copa Di Italia.Hivyo kutokuwepo kwa Chiellini kunaweza kukawathiri Juventus katika michuano hiyo.

Natumai viongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi watafanya maamuzi mazuri wakati huu wa dirisha dogo la usajili likielekea ukingoni katika kuangalia namna ya kuziba pengo la Giorgio Chiellini.

0 comments:

Post a Comment