![]() |
Kaka chukua basi huu mkono |

Hakika lilikuwa ni tukio lililosubiriwa kwa hamu kubwa sana na wapenzi wa kabumbu na wafuatiliaji wakubwa wa Ligi kuu ya soka nchini Uingereza maarufu kama Barclays Premier League(EPL).Swali lilikuwa ni Je,Anton Ferdinand ataukubali mkono wa John Terry katika pambano la mahasimu hao wa jiji la London katika mwendelezo wa EPL?Jibu lilikuwa ni HAPANA kwani chezaji Anton Ferdinand aliukataa mkono wa Jon Terry na hivyo kuonesha kuwa bado wachezaji hao wanachuki ya moja kwa moja.Lakini katika hatua nyingine ni kuwa beki huyo wa QPR aliukataa pia mkono wa mchezaji wa Chelsea Ashley Cole ambaye naye alikosana na Anton Ferdinand kwa kumuunga mkono moja kwa moja nahodha wake John Terry kuwa hakuusika na ubaguzi wa rangi kwa Anton Ferdinand.Ebu angalia picha hizi.
Katika pambano hilo lililopigwa Loftus Road ni kuwa QPR walilazimishwa sare ya bila kufungana na Chelsea
![]() | |
Anton Ferdinand akiukataa mkono wa Terry |
0 comments:
Post a Comment