
Ni mpambano kati ya washika bunduki au washika mitutu wa
London Arsenal na watakatifu au the Saints
hawa sio wengine ni Southampton mchezo ukipigwa katika dimba la Emirates
siku ya Jumamosi majira ya saa 9:45 alasiri.Ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu
sana na mashabiki wote mwenyewe nikiwemo kwani ni mchezo unaohidi kila
viashiria vya soka safi na ya kuvutia kutokana na timu zote kupenda soka ya
kushambulia na ufundi mwingi. Kuna vitu vingi sana binafsi vinanivutia kuhusu
the Saints au watakatifu achilia mbali kwamba bado hawa japata pointi hata moja
lakini soka safi ya kujiamini hasa walipocheza na mabingwa watetezi Manchester
City na Manchster United ni ishara tosha ya aina mchezo unaoutarajia pale
Emirates.Katika michezo yote miwili walifika katika hali ya kuonekana
wanashinda mchezo lakini uzoefu ukwaadhibu wakipoteza kwa matokeo yanayofanana
ya 3-2 lakini bado nina imani watakatifu wamekuja na wataishi milele.
ARSENAL.

Arsenal kulekea katika mchezo huu wanachagizwa na ushindi wa
2-0 pale Anfield kabla ya wiki ya mechi za kimataifa shukrani ziwaendee Lukas
Poldoski na Santi Carzola kwani wote walifanikiwa kufungua akaunti zao Bacrays
pale kunako ligi kuu nchini Uingereza.
Lakini kikubwa cha kuvutia zaidi ni swali kwamba je Arsenal
wataendelea kulinda vyavu zao zisiguswe? Arsenal mpaka sasa wameshacheza
michezo mitatu ya kwanza ya ligi bila
kuruhusu goli hata moja nakuifikia
rekodi ya klabu baada ya miaka 88 na kama watamaliza mchezo huu bila kufungwa
watafikisha mchezo wa 4 bila kuruhusu wavu wao kuguswa na kutengeneza rekodi
mpya ya Arsenal.
Arsenal pia kuelekea mchezo huu ina wasiwasi wa kukosekana
kwa baadhi ya nyota wake kama Abou Diaby
na Theo Walcott ambao wamepata maumivu na timu zao za taifa laikini pia
itategemea na vipimo vya mwisho vitakavyosema.Majeruhi wa muda mrefu
wataendelea kukosekana kama Jack Wilshere,Thomas Rosicky na Bacary Sagna na
mchezaji pekee ambaye atarejea ni Wojciech Zscesny baada ya kupona maumivu ya
mgongo hivyo ikimaanisha atachukua nafasi ya Vito Mannone golini.
SOUTHAMPTON.

Kurudi kwa watakatifu katika daraja la ligi kuu la premier
nchini Uingereza kumeshuhudia wakitupwa katika shimo refu kabisa lenye timu
kama Manchester City, Manchester United na Arsenal kwa pamoja katika mechi zao
za ufunguzi wakiambulia pointi 0 mpaka sasa.Lakini Kocha wa Southampton Nigel
Adkins anasema wanayachukulia matokeo haya kwa mtazamo chanya na wanaimani kwa
uwezo walioonyesha katika michezo yote watabaki ligi kuu.Southampton wanaenda
London kusaka pointi yao ya kwanza ligi kuu japo wanakumbana na ukweli kwamba
timu nyingi amabazo zimepanda daraja na kupoteza mechi zao tatu za kwanza zimishuka daraja.
Alex-Oxlade Chamberlain na Theo Walcott ni mazao
yanayotokana na Shule ya soka ya Southampton lakini kutokana na Walcott kuumia
Chamberlain ndio mwenye nafasi kubwa ya kukutanana timu yake ya zamani.Nigel
Adkins kocha mkuu wa Southampton
anamuongelea the Ox anasema najivunia sana kuona maendeleo ya Alex tangu
ametuacha na kila mtu lazima ajivunie kwa sababu ametokana na mfumo wetu.Mara
zote ukimtazama unafurahi hatukufurahi alipoondoka na unataka afanye hivyo kwa
timu ya taifa ya Uingereza ila tunataka awe na siku mabaya tutakapokutana.
Mchezaji ambaye amevunja rekodi ya uhamisho kwao Gaston Ranirez amekamilisha taratibu zote
anaweza akapata nafasi katika mchezo huu.
UKWELI KUHUSU MECHI.
ARSENAL.
Arsenal hawajapoteza michezo 17 nyumbani wakicheza na
Southampton tangu wafungwe 1-0 mwezi Novemba 1987 na katika msimu wa mwisho
ambao Southamton walikuwa ligi kuu 2004/2005 mechi zote ziliisha kwa sare.
Arsenal hawajashinda michezo 4 ya ligi nyumbani ni mingi
zadi tangu wahamie Emirates kwa kipindi cha miaka 17 na mara ya mwisho walienda
michezo 5 ya ligi bila ushindi nyumbani
ilikuwa msimu wa 1994/1995.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Arsenal wameanza ligi
michezo mitatu bila kufungwa hata goli moja.Portsmouth ndio timu pekee ya ligi
kuu kwenda michezo 4 bila kufungwa hata goli moja msimu wa 2006/2007.
Wakati Theo Walcott anabaki kuwa mchezji mdogo kabisa kuwahi
kuiwakilisha Arsenal ligi kuu akiwa na umri wa miaka 16 na siku 143,Alex Oxlade
Chamberlain ameshaifungia Soputhampton magoli 9 katika michezo 36.
Santi Carzola ndio kiungo anayengoza kwa kupiga pasi sahihi
ligi kuu nchini Uingereza katika eneo la hatari la mpinzani zikiwa na usahihi
wa 88%.
KIKOSI CHAWEZA KUWA HIVI.
Sczcesny
Jenkinson, Vermaelen, Koscielny, Gibbs
Diaby, Arteta, Cazorla
Oxlade-Chamberlain, Giroud, Podolski
Jenkinson, Vermaelen, Koscielny, Gibbs
Diaby, Arteta, Cazorla
Oxlade-Chamberlain, Giroud, Podolski
SOUTHAMPTON.
Watakatifu ndio timu pekee ligi kuu mpaka sasa hawajapata
pointi hata moja wakiwa wameshapoteza michezo miwili kwa 3-2 katika michezo
mitatu ya mwanzo.
Huu ni msimu wa 13 katika 15 wameshindwa kupata ushindi
katika michezo yao mitatu ya mwanzo ya ligi na wameshapoteza michezo yao 4 ya
mwanzo ya ligi msimu wa 1998/1999 ambapo walimaliza ligi nafasi ya 17.
Waatakatifu walikuwa mabingwa wa ligi daraja la kwanza
nchini Uingereza maarufu kama Championship wakifunga magoli 85 lakini 4 tu ndio
yaliyofungwa nnje ya eneo la mita 18.
Japo wanashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi
lakini watakatifu wamefunga magoli mara 2 ya yale Arsenal 2.
KIKOSI CHAWEZA KUWA HIVI.
K Davis
Clyne, Hooiveld, Fonte, Fox
Schneiderlin, S. Davis, Ward-Prowse Puncheon, Lambert, Lallana
Clyne, Hooiveld, Fonte, Fox
Schneiderlin, S. Davis, Ward-Prowse Puncheon, Lambert, Lallana
0 comments:
Post a Comment