
Katika tukio la kustaajabisha kweli kweli mchezo wa ligi kuu nchini Hispania maarufu kama Primiera La Liga baina ya Real Madrid na Rayo Volcano ilibidi uahirishwe baada ya taa za uwanja Estadio de Vallecas nyumbani kwa Rayo Volcano kushindwa kuwaka. Taa za uwanja huo zilishidwa kuwaka baada ya kusadikika kwamba kuna watu wamekata waya zinazounganisha mawasiliano ya taa za uwanjani hapo na polisi wanalifanyia uchunguzi suala hilo.Rais wa Rayo Volcano Raul Martini Presa amechukua hatua kwa kuwaomba msamaha mashabiki waliosafiri kwenda kuutazama mchezo huo na tarehe ya kurudiwa
itatangazwa hapo baadae
0 comments:
Post a Comment