INTER MILAN NA MSIMU
MPYA 2012-13
 |
Claudio
Ranieri |
Hakuna shaka kuwa
unapotaja jina la klabu ya Inter Milan unakuwa unataja moja kati ya vilabu bora
na vikubwa barani ulaya sambamba na vilabu kama Manchester
United,Barcelona,Real Madrid,Bayern Munich,Arsenal nk
Kilichotokea msimu
uliopita wa Serie A kunako klabu hii kubwa duniani kiliwashangaza wengi mno
kiasi cha kuanza kufikiria labda zile dhama za utawala wa Inter Milan nchini
Italia,ulaya na duniani kwa ujumla zimeanza kupotea.Wengine wakasema kuwa bado
jinamizi la aliyekuwa kocha wa timu hiyo kwa kipindi cha miaka 3 linazidi
kuwaandama.Wengine nao hawakuwa nyuma kusema kuwa kurudi upya kwa klabu ya Juventus
ndiko kumeitimisha shangwe za Inter Milan na wengine wanahusisha na kufanya
vibaya kwa klabu hiyo na maamuzi yasiyokuwa na tija toka kwa Rais wa klabu hiyo
Massimo Moratti pamoja na kurugenzi yake ya ufundi inayoundwa na Ernesto Paollilo
pamoja na Marco Branca.
Haya yote yanakuja
kutokana na kufanya vibaya kwa klabu hiyo ya Milan msimu uliopita wa (2011-12)
katika Serie A kwani Inter Milan walishika nafasi ya 6 katika ligi hiyo maarufu
barani ulaya.
 |
Massimo Moratti |
Rafael Benitez, Leonardo,
Gian Piero Gasperini na Claudio
Ranieri wote hawa kwa
nafasi na muda wao walipita kunako klabu ya Inter Milan mara tu baada ya ya
kuondoka kocha aliyeipa Inter mafanikio makubwa sana namzungumzia Jose
Mourinho.Lakini makocha wote hao hawakuweza kurudisha zile nyakati nzuri kwa
mashabiki wa Inter zilizodumu kwa takribani miaka 3 chini ya kocha Mourinho na
mwisho wa siku kuambulia kufukuzwa na Rais wa klabu Massimo Moratti.
INTER
YA MSIMU 2012-13 ITAKUWAJE?
Wachambuzi wa mpira wa
miguu pamoja na mashabiki wa soka ulimwenguni wanajiuliza swali moja ya namna
Inter itakavyokuwa msimu ujao wa ligi ya Serie A (2012-13) hasa baada ya
kufanya vibaya msimu uliopita wa 2011-12.
Binafsi nategemea kuiona
Inter yenye mabadiliko makubwa sana kuanzia nje ya uwanja kwa maana ya uongozi
hasa katika maamuzi pamoja na ndani ya uwanja katika kufanya mabadiliko makubwa
sana ya kiufundi na kimbinu.
MABADILIKO NJE YA UWANJA
Hapa moja kwa moja
nazungumzia uongozi wa Inter Milan chini ya Rais wa klabu hiyo Massimo Moratti
pamoja na kurugenzi yake ikiwa na Ernesto Paollilo pamoja,Marco Branca na Piero
Ausilio.Hawa ni watu muhimu kwa mustakabali wa klabu Inter kwa msimu unaokuja na hata kwa mafanikio
ya klabu ya Inter hapo mbeleni.
Moja ya sababu ya kufanya
vibaya kwa Inter msimu uliopita ni maamuzi yasiyokuwa na tija,macho wala maono
yaliyofanywa na viongozi hao wa Inter Milan.Mfano ni kuuzwa kwa kiungo aliyetokea
kuwa mhimili katika klabu hiyo namzungumzia Thiago Motta.Hakika kuuzwa kwa
Motta tena dirisha dogo la usajiri mnamo mwezi januari kuriidhoofisha mno timu
hiyo katika harakati za ubingwa wa Escudetto,Copa Di Italia pamoja ma michuano
ya ulaya.
 |
Wesley Sneidjer |
Inter walionekana dhahiri
kuwa na mapungufu sehemu ya kiungo pamoja na uwepo wa viungo shupavu kama
Estaban Cambiasso na viungo wapya waliosajiriwa dirisha dogo mwezi huo huo wa
januari mwaka huu 2012 nawazungumzia Fredy Guarin(Porto),Andrea
Poli(Sampdoria),Angelo Palombo(Sampdoria) na wengine kama Ricky Alvarez,Dejan
Stankovic na Wesley Sneidjer ambaye hakuwa msimu mzuri uliopita kwa sababu ya
majeruhi na kufanya idara hiyo ya kiungo
kushindwa kuisaidia Inter kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa
ulaya mwakani ukiachilia mbali ubingwa wa Escudetto.
Tayari Rais wa klabu
Massimo Moratti pamoja na ile bodi yake ya wakurugenzi ambayo kwa kiasi kikubwa
imejaa ukoo wa Moratti kwa sababu Inter Milan ni timu inayomilikiwa na familia
kwa muda mrefu sasa tangu enzi za baba Angelo Moratti ambaye amepewa heshima katika
uwanja wa mazoezi wa Inter kuitwa jina lake ukifahamika kama Angelo Moratti
Sports Centre.
Viongozi hao wameamua kutotumia
sana fedha wakati huu kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita ili kubana matumizi na
kuhakikisha wachezaji vijana wanapewa
nafasi ya kucheza msimu ujao wa ligi na mashindano mengine kama Copa Di
Italia.Uamuzi wa uongozi wa Inter ni kuhakikisha kuwa timu inajengwa upya na
hasa wachezaji chipukizi wakipewa nafasi kunako kikosi cha Inter Milan.Na hiyo
ndo sababu ya Rais wa klabu kuamua kumpa majukumu aliyekuwa kocha wa vijana wa
klabu ya Inter Milan Andrea Stramaccioni ili kuweza kukisuka upya kikosi hicho
cha Inter.
MABADILIKO NDANI YA
UWANJA.
Tayari Inter wameshamsajiri
mshambuliaji Rodrigo Palacios katika kujiimarisha ndani ya uwanja na
kukiongezea nguvu kikosi kwani kuna hatihati ya kuondoka kwa baadhi ya nyota
kama Giampaoro Pazzin, Maicon na Mauro Zarate kwenda kwa vilabu vya Juventus, Chelsea
pamoja na Lazio.Tukumbuke kuwa tayari Diego Forlan ameshaondoka na kujiunga na
klabu ya Internacional (Brazil) wakati kukiwa na wasiwasi kama kiungo
mchezeshaji Wesley Sneidjer kama atabaki na klabu hiyo msimu ujao.
 |
Rodrigo Palacios |
Na dalili zinaonesha kuwa
bado timu itaendela kusajili baadhi ya wachezaji na majina yao yakihusishwa na
kuhamia klabu hiyo ya Lombard katika jiji la Milan.Majina hayo ni pamoja na
Lucas Moura(Sao Paulo),Mattia Destro(Siena),Edinson Cavani(Napoli) na David
Astori(Cagriali).
Kuondoka na kuwasili kwa
baadhi ya wachezaji wakisajiliwa ama kurudi toka kwa mkopo kunako vilabu
mbalimbali katika klabu hiyo ya Inter kama nyota chipukizi
aliyekuwa ligi ya Hispania msimu uliopita akiichezea klabu ya Espanyol kunaweza
kumfanya kocha Andrea Stramaccioni
kubadili mfumo uliozoeleka wa 4-3-1-2 au 4-3-3
na kuja na mfumo mpya kulingana na aina ya wachezaji waliopo Inter
Milan.
Swali; Je tutegemee mfumo
gani kwa Inter Milan msimu ujao?
NI MUDA WA VIJANA KUPEWA
NAFASI
Mashabiki wengi wa soka
duniani wanajiuliza kuwa wapo wapi wachezaji chipukizi kunako timu hiyo ya
Inter Milan na mbona hawapewi nafasi?
Ukweli ni kuwa klabu ya
Inter imejaliwa kuwa na wachezaji wengi vijana ambao wengine tayari wameshaanza
kuonesha uwezo mkubwa katika timu hiyo.Wachezaji hao ni pamoja na Joel Obi,Luc
Castaignoc, Marco Faraoni, Berretti, Alliezi Nazionali na Giovanissimi
Nazionali, Lorenzo Crisetig na bila kumsahau mshambuliaji Samuele Longo.Hao wote kwa kiasi kikubwa
inabidi wapewe nafasi taratibu ili kuzoea mafunzo ya mwalimu Stramaccioni
pamoja na mifumo na falsafa ya mwalimu.
 |
Javier
Zaneti |
Uwepo wa wachezaji vijana
hao pamoja na nyota wengine kunako klabu hiyo kama Estaban Cambiasso,Javier
Zaneti,Yuto Nagatomo,Fredy Guarin pamoja na wachezaji wapya kama Samir
Handanovic,Rodrigo Palacios na nyota wengine watakaokuja kutaifanya klabu hiyo
kuwa na kikosi kikubwa ambacho kitaleta ushindani kunako ligi ya Serie A.
Sitegemei makosa ya nyuma
yatajirudia kwa Inter kuwauza nyota wake chipukizi pasipokuwatumia na kuona
namna gani wanawezainufaisha klabu sasa na siku zijazo kama walivyofanya hapo
nyuma kwa kuwauza Mario Balloteri na David Santon ambao binafsi nilitegemea
wangekuwa na msaada mkubwa sana katika klabu hiyo hapo badae.
KILA LA KHERI INTER MILAN