Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, July 31, 2012

PSG NA UTAWALA MPYA LIGI KUU UFARANSA


PSG: Sababu 5 za kwanini PSG wanapaswa kuogopwa na klabu nyingine za Ulaya kwa msimu ujao wa ligi

 

Uzoefu wa kocha Ancelloti

Carlo Ancelloti
Ni dhahiri kuwa msimu uliopita hakuwa mzuri kama ambavyo kocha Carlo Ancelloti angependa uwe.Akiichukua timu kutoka kwa mwalimu Antoine Kambouare,Ancelloti alikuwa na matokeo yafuatayo katika mechi zake 10 za mwanzo na PSG;5-5-0,kwa maana ya kushinda mechi 5,kutoka sare mechi 5 na kutopoteza mechi katika mechi 10 za mwanzo.Mechi 9 nyingine kwa klabu ya PSG katika ligi ya Ufaransa maarufu kama (Le Champione au French Ligue 1) zilikuwa kwa mfumo wa  6-1-2  kwa maana ya kushinda mechi 6,kutoka sare mechi 1 na kupoteza mechi 2.Tafsiri ya mechi zote hizo ni kuwa PSG walishindwa kushindana na timu ya Monperier ambayo baadaye ilitangazwa kuwa bingwa mpya wa Ligi kuu ya soka nchini Ufaransa.

Tukumbuke kuwa PSG pia walipoteza mechi dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ligi hiyo klabu ya Olimpic Lyon.Ukichangaya na rekodi mbalimbali alizoweka akiwa na vilabu vya AC Milan na Chelsea, Hakuna shaka kuwa Ancelloti ataipa mafanikiwa klabu hiyo ya PSG kutokana na uzoefu wake katika michuano mikubwa na mechi za kimataifa hasa za Ligi ya mabingwa Ulaya ambapo mara ya mwisho PSG walishiriki ilikuwa ni mwaka 2003.

Kuwepo kwa wachezaji wazoefu.

Thiago Motta
Kama ilivyo kwa timu nyingine mbalimbali za Ulaya,PSG nayo imebarikiwa kuwa na wachezaji wazoefu ambao jukumu lao kubwa ni kuwaongoza wachezaji chipukizi.Mfano wa wachezaji hao ni Thiago Motta, Mohamed Sissoko, Maxwell, Diego Lugano na Alex.Pia ujio wa nyota wapya kama  Zlatan Ibrahimovic,Ezequel Lavezzi kutazidi kuimarisha timu hiyo.
Pia kuna kundi la wachezaji kama Sylvain Armand, Nene, Mathieu Bodmer, Zoumana Camara na  Nicholas Douchez ambao hawajacheza klabu kubwa zaidi ya PSG lakini wanauzoefu mkubwa na Ligi kuu ya Ufaransa na mchango wao mkubwa sana kwa PSG.

Wachezaji chipukizi

Mamadou Sakho
Wakati PSG wakijivunia kuwepo kwa wachezaji wakongwe,pia wanajivunia uwepo wa chipukizi wazuri kunako klabu hiyo. Na hapa bila shaka litakuja jina la Javier Pastore ingawa watu wanasahau kuwa kuna kundi kubwa sana la wachezaji chipukizi wenye uwezo mkubwa na ambao wana mchango mkubwa sana kwa klabu ya PSG.
Embu waangalie wachezaji chipukizi kama Jeremy Menez, Salvatore Sirigu, Kevin Gameiro, Blaise Matiudi na Mamadou Sakho wakiunda kundi la wachezaji nyota wenye matarajio na matumaini ya kufanya vyema kama wachezaji na timu yao ya PSG.Tukumbuke kuwa wachezaji hawa vijana wana uzoefu na mechi za kimataifa.




 

Usajiri mpya

 

Majina makubwa yataendelea kuja kunako klabu hii ya PSG kama walivyohaidi wamiliki wa timu hiyo kina Sheikh Makhtour wakiongozwa na mkurugenzi wa ufundi kunako klabu hiyo Leonardo.
Tayari wameshamchukua  Ezequiel Lavezzi toka (Napoli),Zlatan Ibrahimovic,Thiagi Silva toka (AC  Milan) pamoja Marco Verrati toka klabu iliyopanda daraja msimu h kunako ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.Usajiri wa Lavezzi na Ibrahimovic  utawahakikishia PSG kuwa na safu nzuri sana ya ushambuliaji ambao  watashirikiana na kina Kevin Gameiro pamoja na Anderson Nene.

 

Tatizo la klabu katika ushambuliaji lapata suluhu

Sehemu ya ushambuliaji msimu uliopita kunako klabu ya Paris Saint-German haikiuwa na makali sana kwani ilikosa kuwa na mwendelezo chanya kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa msimu na hivyo kuwagharimu PSG katika mbio zao za ubingwa wa Ligue 1.
Pamoja na kupata huduma za washambuliaji Kevin Gameiro na Guillaume Hoarau, PSG hawakupata mshambuliaji aliyekuwa na mwendelezo mzuri wa ufungaji magoli na hivyo kuifanya PSG kupoteza points nyingi sana katika Ligue 1.
Hivyo kuja kwa wachezaji Lavezzi na Ibrahimovic kutaimarisha nakuiongezea nguvu mpya safu ya ushambuliaji ya PSG kwa kuwa wachezaji hao wana uwezo mzuri pamoja na uzoefu mkubwa.


0 comments:

Post a Comment