JUVENTUS-MAAJABU YA KIBIBI KIZEE KURUDI KATIKA UJANA
![]() |
Andrea Pirlo |
![]() |
Ernesto Bronzetti |
Mmoja wa mawakala wanaotambulika na FIFA Ernesto Bronzetti katika mahojiano yake na mtandao mmoja maarufu nchini Italia Tuttosport alisikika akitabiri kuwa Juventus wamerudi katika utawala wao kunako ligi ya Italia na haoni kama kuna timu za kuwazuia tena katika mbio zao za ubingwa msimu ujao.Bronzetti alitumia vigezo vifuatavyo katika kuthibitisha kauli yake.Namnukuu kwa maneno yake;
. “Juve are destined to dominate for the next few days,” Bronzetti told Tuttosport. “They have a stadium that is beginning to provide income, they put their hands on the best young players, and they have solid foundations, a great Coach and directors up to the task.” The way I see it, this side is even stronger than it was under Antonio Giraudo and Luciano Moggi.”Mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi wakala Bronzetti anazungumza kuwa Juventus wamejipanga kuanzia kwenye uongozi mpaka katika masuala ya ufundi uwanjani.Na hii inachagizwa na sera za sasa za klabu chini ya Rais Agnelli, uwanja wao mpya ambao waliutumia msimu uliopita katika ligi, na pia mshikamano wa mashabiki ambao kwa kipindi kirefu walivumilia shida za klabu mpaka sasa ambapo Juventus inaonekana kuanza kurudi katika zama zake za utawala katika soka la Italia.
Pia kwa kujifunza makosa ya viongozi waliopita nawazungumzia Alesio Seko,Giovanni Cobori Gigli Antonio Giraudo na wengineo,Juventus wameamua kutumia fedha kujenga kikosi chao lakini uwekezaji mkubwa ukifanywa katika kuwaibua vijana wenye vipaji na kuwapa nafasi ili waweze kuisaidia klabu hapo badaye.
Wengi wanakumbuka namna klabu ilivyowaacha bila kuwapa nafasi wachezaji vijana na wenye vipaji kama Sebastiani Giovinco na Antonio Nocerino kwenda vilabu vya Palermo na Parma na kuingiza majina makubwa ya kina Felipe Melo pamoja na Diego na mwisho wa siku wachezaji hao kushindwa kuonesha makali na kupelekea kuuzwa na kupelekwa kwa mkopo katika vilabu vya Werder Bremen(Ujerumani) na Galatasary(Uturuki).Na hivyo uongozi wa sasa chini ya Rais Agnelli pamoja na mtendaji mkuu Marrota kuamua kufanya mseto wa wachezaji vijana pamoja na wakongwe.
![]() |
Paul Pogba |
MATARAJIO
Ni kuiona Juventus ikija kwa kishindo kunako michuano mbalimbali kama mshindani makini na wa kweli katika Italian Serie A,Copa Di Italia na Klabu bingwa barani Ulaya hasa baada ya kuonekana dalili za kuanguka kwa vilabu vikongwe nchini Italia na jiji la Milan navizungumzia Inter na AC Milan.Hii inatokana na Juventus kuwa na miundo mbinu mizuri kama uwanja wake(Juventus Arena),benchi zuri la ufundi likiongozwa na kocha Antonio Conte bila kusahau nguvu pia ya kiuchumi pamoja na kuwa na kikosi kikubwa.
0 comments:
Post a Comment