Wapi atakuwepo Aquilan msimu ujao wa
2012-13?
![]() |
Alberto Aquilan |
Akiingia
kucheza sambamba na Daniele De Rossi ambaye tayari alishawafunga Torino goli 1
katika mechi hiyo, Aquilan alionesha kipaji kilichomtabiria kuja kuwa moja kati
ya mastaa wa badaye wa klabu hiyo ya Serie A pamoja na Ulaya kwa ujumla.
Akiwa
na Roma,Aquilan amefanikiwa kutwaa mataji mbalimbali kama Supercopa Italiana
mwaka 2006 na Copa Di Italia mwaka 2007.Mnamo mwaka 2009,aliyekuwa kocha wa
Liverpool Rafael Benitez alimsajili Aquilan kwa hela za ulaya(EURO) MILION 17
kujiunga na Liverpool.
Lakini
tangu aondoke katika jiji hilo takatifu la Roma, Aquilani anaelekea kusahaulika
kunako medani ya soka.Hii inatokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo
yamekuwa yakimwandama mchezaji huyo. Mshindi huyo wa Copa Di Italia mwaka 2007
na klabu ya Roma pamoja na ngao ya jamii maarufu nchini Italia kama
SupercopaItaliana ameweza kucheza mechi 30 katika msimu mmoja tu kati ya misimu
sita iliyopita akiwa na klabu za Liverpool na Ac Milan.
Na
sasa ni msimu mpya wa Ligi mbalimbali za Ulaya unakaribia kuanza huku kuiwa na
mashaka ya kuwa ni wapi mchezaji Alberto Aquilan atacheza msimu wa mwaka
2012-2013.
KILA LA KHERI AQUILAN
0 comments:
Post a Comment