Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, July 31, 2012

NI MSIMU MPYA KWA INTER MILAN


INTER MILAN NA MSIMU MPYA 2012-13

Claudio Ranieri
Hakuna shaka kuwa unapotaja jina la klabu ya Inter Milan unakuwa unataja moja kati ya vilabu bora na vikubwa barani ulaya sambamba na vilabu kama Manchester United,Barcelona,Real Madrid,Bayern Munich,Arsenal nk
Kilichotokea msimu uliopita wa Serie A kunako klabu hii kubwa duniani kiliwashangaza wengi mno kiasi cha kuanza kufikiria labda zile dhama za utawala wa Inter Milan nchini Italia,ulaya na duniani kwa ujumla zimeanza kupotea.Wengine wakasema kuwa bado jinamizi la aliyekuwa kocha wa timu hiyo kwa kipindi cha miaka 3 linazidi kuwaandama.Wengine nao hawakuwa nyuma kusema kuwa kurudi upya kwa klabu ya Juventus ndiko kumeitimisha shangwe za Inter Milan na wengine wanahusisha na kufanya vibaya kwa klabu hiyo na maamuzi yasiyokuwa na tija toka kwa Rais wa klabu hiyo Massimo Moratti pamoja na kurugenzi yake ya ufundi inayoundwa na Ernesto Paollilo pamoja na Marco Branca.
Haya yote yanakuja kutokana na kufanya vibaya kwa klabu hiyo ya Milan msimu uliopita wa (2011-12) katika Serie A kwani Inter Milan walishika nafasi ya 6 katika ligi hiyo maarufu barani ulaya.
Massimo Moratti
Rafael Benitez, Leonardo, Gian Piero Gasperini na Claudio Ranieri wote hawa kwa nafasi na muda wao walipita kunako klabu ya Inter Milan mara tu baada ya ya kuondoka kocha aliyeipa Inter mafanikio makubwa sana namzungumzia Jose Mourinho.Lakini makocha wote hao hawakuweza kurudisha zile nyakati nzuri kwa mashabiki wa Inter zilizodumu kwa takribani miaka 3 chini ya kocha Mourinho na mwisho wa siku kuambulia kufukuzwa na Rais wa klabu Massimo Moratti.

INTER YA MSIMU 2012-13 ITAKUWAJE?                                                     
Wachambuzi wa mpira wa miguu pamoja na mashabiki wa soka ulimwenguni wanajiuliza swali moja ya namna Inter itakavyokuwa msimu ujao wa ligi ya Serie A (2012-13) hasa baada ya kufanya vibaya msimu uliopita wa 2011-12.
Binafsi nategemea kuiona Inter yenye mabadiliko makubwa sana kuanzia nje ya uwanja kwa maana ya uongozi hasa katika maamuzi pamoja na ndani ya uwanja katika kufanya mabadiliko makubwa sana ya kiufundi na kimbinu.

MABADILIKO NJE YA UWANJA
Hapa moja kwa moja nazungumzia uongozi wa Inter Milan chini ya Rais wa klabu hiyo Massimo Moratti pamoja na kurugenzi yake ikiwa na Ernesto Paollilo pamoja,Marco Branca na Piero Ausilio.Hawa ni watu muhimu kwa mustakabali wa klabu  Inter kwa msimu unaokuja na hata kwa mafanikio ya klabu ya Inter hapo mbeleni.
Moja ya sababu ya kufanya vibaya kwa Inter msimu uliopita ni maamuzi yasiyokuwa na tija,macho wala maono yaliyofanywa na viongozi hao wa Inter Milan.Mfano ni kuuzwa kwa kiungo aliyetokea kuwa mhimili katika klabu hiyo namzungumzia Thiago Motta.Hakika kuuzwa kwa Motta tena dirisha dogo la usajiri mnamo mwezi januari kuriidhoofisha mno timu hiyo katika harakati za ubingwa wa Escudetto,Copa Di Italia pamoja ma michuano ya ulaya.
Wesley Sneidjer
Inter walionekana dhahiri kuwa na mapungufu sehemu ya kiungo pamoja na uwepo wa viungo shupavu kama Estaban Cambiasso na viungo wapya waliosajiriwa dirisha dogo mwezi huo huo wa januari mwaka huu 2012 nawazungumzia Fredy Guarin(Porto),Andrea Poli(Sampdoria),Angelo Palombo(Sampdoria) na wengine kama Ricky Alvarez,Dejan Stankovic na Wesley Sneidjer ambaye hakuwa msimu mzuri uliopita kwa sababu ya majeruhi na kufanya  idara hiyo ya kiungo kushindwa kuisaidia Inter kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya mwakani ukiachilia mbali ubingwa wa Escudetto.
Tayari Rais wa klabu Massimo Moratti pamoja na ile bodi yake ya wakurugenzi ambayo kwa kiasi kikubwa imejaa ukoo wa Moratti kwa sababu Inter Milan ni timu inayomilikiwa na familia kwa muda mrefu sasa tangu enzi za baba Angelo Moratti ambaye amepewa heshima katika uwanja wa mazoezi wa Inter kuitwa jina lake ukifahamika kama Angelo Moratti Sports Centre.
Viongozi hao wameamua kutotumia sana fedha wakati huu kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita ili kubana matumizi na kuhakikisha wachezaji vijana wanapewa  nafasi ya kucheza msimu ujao wa ligi na mashindano mengine kama Copa Di Italia.Uamuzi wa uongozi wa Inter ni kuhakikisha kuwa timu inajengwa upya na hasa wachezaji chipukizi wakipewa nafasi kunako kikosi cha Inter Milan.Na hiyo ndo sababu ya Rais wa klabu kuamua kumpa majukumu aliyekuwa kocha wa vijana wa klabu ya Inter Milan Andrea Stramaccioni ili kuweza kukisuka upya kikosi hicho cha Inter.

MABADILIKO NDANI YA UWANJA.
Tayari Inter wameshamsajiri mshambuliaji Rodrigo Palacios katika kujiimarisha ndani ya uwanja na kukiongezea nguvu kikosi kwani kuna hatihati ya kuondoka kwa baadhi ya nyota kama Giampaoro Pazzin, Maicon na Mauro Zarate kwenda kwa vilabu vya Juventus, Chelsea pamoja na Lazio.Tukumbuke kuwa tayari Diego Forlan ameshaondoka na kujiunga na klabu ya Internacional (Brazil) wakati kukiwa na wasiwasi kama kiungo mchezeshaji Wesley Sneidjer kama atabaki na klabu hiyo msimu ujao.
Rodrigo Palacios
Na dalili zinaonesha kuwa bado timu itaendela kusajili baadhi ya wachezaji na majina yao yakihusishwa na kuhamia klabu hiyo ya Lombard katika jiji la Milan.Majina hayo ni pamoja na Lucas Moura(Sao Paulo),Mattia Destro(Siena),Edinson Cavani(Napoli) na David Astori(Cagriali).
Kuondoka na kuwasili kwa baadhi ya wachezaji wakisajiliwa ama kurudi toka kwa mkopo kunako vilabu mbalimbali  katika  klabu hiyo ya Inter kama nyota chipukizi aliyekuwa ligi ya Hispania msimu uliopita akiichezea klabu ya Espanyol kunaweza kumfanya kocha  Andrea Stramaccioni kubadili mfumo uliozoeleka wa 4-3-1-2 au 4-3-3  na kuja na mfumo mpya kulingana na aina ya wachezaji waliopo Inter Milan.
Swali; Je tutegemee mfumo gani kwa Inter Milan msimu ujao?

NI MUDA WA VIJANA KUPEWA NAFASI
Mashabiki wengi wa soka duniani wanajiuliza kuwa wapo wapi wachezaji chipukizi kunako timu hiyo ya Inter Milan na mbona hawapewi nafasi?
Ukweli ni kuwa klabu ya Inter imejaliwa kuwa na wachezaji wengi vijana ambao wengine tayari wameshaanza kuonesha uwezo mkubwa katika timu hiyo.Wachezaji hao ni pamoja na Joel Obi,Luc Castaignoc, Marco Faraoni, Berretti, Alliezi Nazionali na Giovanissimi Nazionali, Lorenzo Crisetig na bila kumsahau mshambuliaji Samuele Longo.Hao wote kwa kiasi kikubwa inabidi wapewe nafasi taratibu ili kuzoea mafunzo ya mwalimu Stramaccioni pamoja na mifumo na falsafa ya mwalimu.
Javier Zaneti
Uwepo wa wachezaji vijana hao pamoja na nyota wengine kunako klabu hiyo kama Estaban Cambiasso,Javier Zaneti,Yuto Nagatomo,Fredy Guarin pamoja na wachezaji wapya kama Samir Handanovic,Rodrigo Palacios na nyota wengine watakaokuja kutaifanya klabu hiyo kuwa na kikosi kikubwa ambacho kitaleta ushindani kunako ligi ya Serie A.
Sitegemei makosa ya nyuma yatajirudia kwa Inter kuwauza nyota wake chipukizi pasipokuwatumia na kuona namna gani wanawezainufaisha klabu sasa na siku zijazo kama walivyofanya hapo nyuma kwa kuwauza Mario Balloteri na David Santon ambao binafsi nilitegemea wangekuwa na msaada mkubwa sana katika klabu hiyo hapo badae.
KILA LA KHERI INTER MILAN

0 comments:

Post a Comment