![]() |
Yaya Toure |
Mchezaji wa klabu ya Manchester City ya nchini England na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure amelazwa katika kliniki moja katika jiji la Abu Dhabi kwa matatizo ya homa.Mchezaji huyo bora wa Afrika hakuwepo katika ufunguzi wa mazoezi rasmi wa timu hiyo siku ya Jumapili katika uwanja wa Mohammed Bin Zayed chini ya kocha Sabri Lamouchi ambaye anaamini kuwa mchezaji huyo atapona haraka na kujiunga na wenzake katika maandalizi ya michuano ya Afrika mwaka huu.
Yaya yupo chini ya uangalizi wa jopo la madaktari wa timu na hakuna shaka anaweza kurudi mapema kabla ya mechi ya kujipima ubavu dhidi ya timu ya taifa ya Misri mnamo tarehe ya 14 mwezi huu.Nahodha wa timu hiyo Didier Drogba pia naye hakuweza kufanya mazoezi na wenzake kutokana na kuwa na maumivu ya kichwa.Timu ya Ivory Coast ilikutana jijini Paris Ufaransa kabla ya kuweka kambi yao kwa muda nchini Falme za Kiarabu katika mji wa Abu Dhabi.
0 comments:
Post a Comment